Friday, 6 November 2015

39. Yearning for life



How do we change bad situations? Why is it so tough to tackle Sustainable Development Goals, even when everyone seems on the same side? Allow me a little diversion to illustrate the difficulty … then persevere through the serious bits, because the conclusion not only illustrates why the Women’s Group ‘Tushikamane’ project is necessary, but casts an explanatory beam or two on how we might make Earth a better planet.

But to begin with the diversion:
Common chicory is a woody perennial found on the roadsides of Europe. Being one of the few roadside plants which is not poisonous to humans, it has found its way in various forms into our diet in times of need. In times of positively desperate need, in fact, because it tastes like a woody perennial found on roadsides.





 One such time of desperate need was in 1876 in India, when Gordon Highlanders sat around the camp fire gagging for a nice cup of wet after a hard day’s colonising. Coffee was more popular than tea in the early Victorian era, but coffee in the military field of combat was not to be had. Victorian Britain may have had plenty of colonies that produced the bean, but they also had plenty of other fields of combat, as they endeavoured to subsume the Canadians, Afghans, Chinese, Sikhs, Maoris, Hottentots, Ashantees, Zulus, Egyptians, Sudanese, Boers, Mexicans, Malays, Australian Aborigines, Caucasians, Ugandans, Tanganyikans, Persians, Bolivians, Nagas, Abyssinians, Burmese, Greeks, Crimeans, Japanese, West Africans, Ceylonese, Somalis, and of course, the Irish.

Then someone back home in Scotland had the brilliantly parsimonious idea to add chicory to coffee to bulk it out. Or, to be more precise, to add a tiny touch of coffee to chicory. The resulting brew is called ‘Camp’, and has been popular in every war ever since. Indeed, for many, it continued to be the chosen stimulant right up until the end of rationing in 1954.



Here’s the rub: my mum was brought up on the stuff, and so you would have thought that she would dream of the day when she could get an extra-hot-skinny-latte whenever the whim took her. Not so. Camp carried on being her tipple for another five decades after proper coffee became available. Why? Why do people carry on doing what they have always done, even when it includes drinking something that looks and tastes like mud?

Is the answer this: that awfulness is preferable to possibility? Or rather, that comfortable, predictable, secure, stable, in-your-control, familiar awfulness is more appealing to the human condition than uncomfortable, unpredictable, insecure, unstable, out-of-your-control, unfamiliar possibility?

Is this really true? If you do not like philosophy, you can stop reading now, but if you do, then get yourself a Grande Cappuccino, a comfy seat on an old leather sofa, an exorbitantly-priced two-centimetre-square piece of flapjack made of three seeds and a sultana, and read my take on this fundamentally vital topic:

Imagine a bubble village, where each house represents one of us:




For most of us, we make the inside of our bubble comfortable, predictable, secure, stable, and in-our-control. Indeed, so strong are these instincts, that we persuade ourselves that everything within the bubble is as it should be. Self-deception is at the heart of obstinacy. In this process, Knowledge and Reason are laid carefully in a bottom drawer, to be accessed only when called for. (We commonly use Reason not to modify what we want or believe, but to justify it.) The internal environment of our bubble may not be healthy, but we get used to it. We develop habits. We grow accustomed. We do what we always did. And we pretend to ourselves that this is How Things Should Be.

Then someone arrives with Information, or Reasons, or ‘Help’, or Instructions, and tries to break into our bubble – to persuade us, for instance, to stop smoking; to eat less cholesterol; to be nice to people we don’t like; to exercise more; to be more client-friendly; to be more spiritual; to be less traditionalist; and to be more reliable when told to buy some more bread next day even when she only told you in passing at midnight when you’d already had two glasses of wine, and anyway why didn’t she buy the bread when she was at the shops herself that very day; etc. Of course then when someone tries to break into your house, you bolt the boor, bar the windows, and hide behind the settee.

Others of us, (the more enlightened?), spend most of the time out of our own cocoon, pestering people by trying to break into theirs. But to give unwanted information is simply nagging; unwanted rationalisation is spurious; unwanted help is imposition; and unwanted instruction is oppression.

To make the whole situation more complicated, the entire bubble-village is itself within a bubble, and what applies singly to the individual, also applies collectively to the community and the culture. The bubble-villagers like things just the way they are, thank you. The truly enlightened, by this metaphor, will be outside all bubbles, exhausting themselves going from village to village, bashing their ideas on the outer walls. (Oscar Wilde was one such wanderer, whose quote, “Whenever people agree with me, I always feel I must be wrong”, laid the foundation for 21st century Democracy.) 



(It must have been a nightmare living with someone who only talks in quotes: 
You: "Good morning, Oscar. Cup of tea?"
Him: "I can resist everything except temptation!"
You: "So is that a yes?"
Him: "Selfishness is not living as one wishes to live, it is asking others to live as one wishes to live."
You: "So you do want one, then?"
Him: "I have the simplest tastes. I am always satisfied with the best."
You: "So you mean you want a cup?"
Him: "There are only two tragedies in life: one is not getting what one wants, and the other is getting it."
You: "So you'd like a cup of tea?"
Him: "If you are not too long, I will wait here for you all my life."
You: "OK, I'll make you a cup. I am a pretty good tea-maker!"
Him: "Consistency is the last refuge of the unimaginative."
You: "I'm just saying I've always made a good cup of tea!"
Him "Experience is simply the name we give our mistakes."
You: "I can't stand this! I'm going to make myself a cup of tea."
Him: "Moderation is a fatal thing. Nothing succeeds like excess."
You: "That's it! You're not getting a cup of tea."
Him: "Illusion is the first of all pleasures."
You: "I'm getting tired of this. I let you lie in, and then come up and offer you a cup of tea, and all I get is quotes!"
Him: "A dreamer is one who can only find his way by moonlight, and his punishment is that he sees the dawn before the rest of the world.
You: "Right! I'm chucking yours out of the window!"
Him: "We are all in the gutter, but some of us are looking at the stars."
You: "Make your own, you sad ... !"
Him: "True friends stab you in the front."
You: "I'm off."
Him: "Some cause happiness wherever they go; others whenever they go.")


Anyway, where were we?
Oh yes! Let's come down with a bump back into musing on what makes people resist change.

Collective normality, it seems, is the ultimate determinant of our behaviour, and within those collective norms, we mainly sit in our bubbles and make our own delusions. And so it is that if a plane crashes in Russia with no survivors; or a Tsunami kills a quarter of a million; or your next-door neighbour develops aggressive cancer; or you develop chronic bronchitis; or you get put in prison with a tolerable enough room-mate; or the planet slowly overheats; or your country goes to war; or someone’s sister bleeds to death in childbirth on the floor of a mud-hut; that life goes on. You have your morning cuppa, and watch Coronation Street on Wednesdays.




Why do we behave in this way? Why do most of us live in a cocoon, within a cocoon-village? And what can we do about it? Maybe our carry-on-as-we-are mentality comes from feeling that when we lose what we are familiar with, we lose a bit of who we are, and that is scary. 

It should not be surprising, then, that change is so hard: To change the way things are, you have to change people. But you cannot change people - they can only change themselves. They have to take the chain off the door of the cocoon, have a peep outside, be lured to step out into uncertain reality ... and to become someone slightly different.

What might lure them - or us - to do this?! To change not just what we are familiar with, but actually to change something of who we are? Information, reasons, instructions are not enough. In fact, they can simply be intrusive. To get people to do something as radical as embrace change, things have to be yearned for. Indeed, I could go so far as to say this: without actual yearning, no sustainable change is possible. 

We cannot just tell people what they need. We cannot just pitch up with our ready-made solutions. Our stock-in-trade must be questions, rather than answers. We must listen. And to do this, we must give a voice to those who most need it - the women and children of remote villages for whom the death toll of life is so high. 




Such women have become accustomed to the awfulness of normality. They may feel powerless in the face the weary blocks that impede sustained development: inertia, opposition, vested interest, self-interest, partisan groups, intolerance, corruption, resentment, and ambition.

All of these, however, relate to the collective mentality, and when that collective thinking is a yearning for things to be different, then they will be.

And so to Tushikamane, the project which is trying to reduce tragic death of mothers and babies in the villages of Tunguli, in rural Tanzania. This month, the Tushikamane team leaders are visiting the MaiMwana project, to experience amazing examples of this collective determination in action. 



http://www.maimwana.org/

Later in the month I will be going out to Tunguli, to be involved in the final week of team training. Thereafter, the team will begin the process of mobilising community participation and women’s voices in each of six hamlets deep in the Tanzanian bush.

Working from the manuals and materials kindly supplied by Women & Children First, we have produced a full set of materials, and have translated the key ones into Swahili for use by our front-line staff. All these resources are now posted on this blog. For those who like detail, they give a blow-by-blow account of how Tushikamane intends to reduce death of mothers and babies.

The bottom line is this: telling people what to do does not produce sustainable change. Even if the people are asking “Why must we do it?”, it means that they are still in the cocoon.

When they are asking “How can we do it?”, however, and yearning for the answer, it means that they are on the way to a new destiny, and for some, a new life.






Monday, 2 November 2015

For reference: KIONGOZI CHA TUSHIKAMANE - Kiswahili Manual

KIONGOZI CHA TUSHIKAMANE

YALIYOMO
Majukumu   na wajibu wa Mwezeshaji wa Tushikamane
Maarifa ya Mwezeshaji wa Tushikamane juu ya Afya ya Mama
            na Mtoto    Mchanga
Kuwa Mwezeshaji
Stadi za kufanya kazi na  vikundi
Mzunguko wa Mikutano ya  Tushikamane
Kuandaa ripoti  za  Tushikamane

Awamu ya  1: Kubainisha matatizo pamoja
Mkutano wa  1: Kitongoji kukaa pamoja kuunda kikundi
Mkutano wa 2: Wanawake katika umri wa uzazi kubainisha matatizo ya
           afya ya wanawake.
Mkutano wa  3: Wanawake katika umri wa uzazi kubainisha matatizo ya
           watoto wachanga
Mkutano wa  4: Kuainisha matatizo yatakayopewa kipaumbele
Mkutano wa 5: Kubainisha mambo ya msingi ambayo yanachangia
           matatizo hayo – mizizi ya matatizo

Awamu ya  2: Kupanga ufumbuzi pamoja  
Mkutano wa  6: Kubainisha shughuli za uzuiaji na usimamizi wa matatizo hayo.
Mkutano wa  7: Kuandaa mpango kazi
Mkutano  8: Kuwasilisha taarifa  juu ya  maendeleo ya kikundi  kwa wanajamii

Awamu ya  3: Kutekeleza njia za ufumbuzi pamoja
Mkutano wa  9: Kupanga njia za ufumbuzi
Mkutano wa  10: Kukusanya rasilimali
Mkutano wa  11: Kuandaa mfumo wa ufuatiliaji

Awamu ya  4: Kutathmini pamoja
Mkutano wa   12: Maendeleo ya mchakato wa  tathmini
Mkutano wa 13: Kutathmini mafanikio ya miradi na Vikundi vyenyewe
           vya  Tushikamane
Mkutano wa  14: Kupanga kwa ajili ya siku zijazo


























SHUKRANI

Taasisi ya Afya Ulimwenguni ya Chuo Kikuu cha London (The Institute for Global Health at University College, London), ina dhamira kubwa ya kupunguza vifo vya akinamama na watoto wachanga katika nchi zinazoendelea. Nchi nyingi zimekuwa  hazipati mafanikio yanayotarajiwa, na  Prof Anthony Costello na timu yake katika taasisi hiyo walikuwa na dira ya kuziona jamii zikihamasishwa kushiriki kwa bidii katika mipango yao ya maendeleo.

Kilichofuata ni utafiti wenye kiwango cha  hali ya juu,uliowezesha kugundua  utaratibu wenye ufanisi mkubwa: Njia ya uhamasishaji jamii yenye uhakika wa kusaidia kupunguza vifoo na kuleta maboresho katika afya ya watoto wachanga, watoto wadogo na mama zao kwa kiwango kikubwa na kwa gharama nafuu. 

Kutokana na ugunduzi huo lilianzishwa Shirika la hiyari la kuwahudumia wanawake na watoto liitwalo  Women & Children First, au ‘Wanawake na Watoto Kwanza’ likikusudia kutangaza manufaa ya njia hiyo  kwa jamii zenye mahitaji makubwa sana duniani.  Mikey Rosato ni Meneja Mwandamizi wa Programu katika shirika hilo, na anaongoza majaribio zaidi kwa niaba ya Shirika la Afya Duniani  juu ya  Utaratibu wa Kujifunza  na Utendaji Shirikishi kwa lengo la kupunguza vifo vya akinamama(PRA).

Kazi za shirika la Wanawake na Watoto Kwanza - Women & Children First,  zinajenga kwenye mafanikio ya juhudi za Shirika la Afya Duniani, Idara ya Afya ya Mama, Watoto na Uzazi, na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani UNICEF. Kwa pamoja, wameanzisha uandaaji wa zana kwa ajili ya  uhamasishaji jamii juu ya Afya ya Akinamama na Watoto, kama nyongeza kwa zana zingine ambazo  tayari zinatumika kwa ajili  ya matunzo ya watoto wachanga na watoto wadogo kwenye jamii (2012), na  Huduma ya Kumtembelea Mtoto Mchanga Nyumbani: mkakati wa kuboresha uhai (2009).

Mafanikio ya uhamasishaji jamii, mizunguko ya kujifunza, na utendaji shirikishi yameimarishwa na kazi za Mradi wa  MaiMwana nchini  Malawi. Florida Banda na timu yake wameisaidia sana na kuipa moyo  Tushikamane.

Mwaka 2015, Mikey Rosato na timu yake waliweka pamoja zana hizi kwenye Kiongozi chao cha Shirika la Afya Duniani, mahali ambapo Kiongozi hiki kimetoka, na kuzifanya zana kuwa  rafiki zaidi kwa  wawezeshaji wa msitari wa mbele wa Mradi wa  Tushikamane(tunaomba radhi kwa makosa yoyote yatakayojitokeza!). Tunawashukuru mno mno. Asante sana sana!

REJEA

http://www.maimwana.org/
http://www.biomedcentral.com/1471-2393/14/243/abstract
http://apps.who.int/iris/bitstream/10665/127939/1/9789241507271_eng.pdf?ua=1
http://www.who.int/pmnch/countries/tanzaniamapstrategic.pdf









































KIONGOZI CHA TUSHIKAMANE

Jinsi ya kuendesha Vikundi vya  Tushikamane kupitia mzunguko wa mikutano 14

Vikundi vya Tushikamane
Tushikamane ni neno  la  Kiswahili ambalo linatumika  kumaanisha vikundi  ambavyo vimeanzishwa chini ya miradi inayofanana , hasa Mradi wa  Malawi, unaoitwa ‘MaiMwana’. Katika mradi huo, vilijulikana kama Vikundi vya Kujifunza na Utendaji Shirikishi kwa ajili ya Afya ya Mama na Mtoto Mchanga(‘Participatory Learning and Action Groups for Maternal and Newborn Health’).  Kichwa hiki kinaeleza vizuri  namna vinavyofanya kazi na kusudi lake: kwamba jamii hushiriki na kujihusisha kwa undani katika kutafuta njia za kuzuia vifo vya kusikitisha  vya akinamama na watoto wao.

Vikundi vya Tushikamane pia hulenga kuleta maboresho katika afya ya mama na watoto wachanga na kupunguza vifo kwa kutoa fursa za majadiliano, mahali ambapo  wanajamii hususan wanawake, huweza kubainisha vipaumbele vyao kuhusiana na matatizo ya afya ya mama na mtoto mchanga na kubuni, kutekeleza na kutathmini njia za ufumbuzi zinazotokana na jamii yenyewe.

Kikundi kimoja cha Tushikamane kitaanzishwa katika kila kitongoji, kwa kuanzia katika vitongoji 6. Nchini Tanzania, mahali ambapo  unakuta nyumba zote katika viitongoji  wakati mwingine havitengenezi  kijiji kimoja, tutatumia tafsiri iliyotumika katika Sensa ya Taifa  ambayo inasema  kuwa kitongoji kinapaswa kuwa na takriban watu  700.   

Vikundi vya Tushikamane vitaanza kwa kuandikisha wanawake walio kwenye umri wa uzazi kama wanakikundi, ili kuwa na uhakika wa kuwapatia wanawake vijana sauti katika maamuzi juu ya jinsi ya kushughulikia matatizo yanayowakabili.  Wajawazito, wanawake ambao ndiyo wamejifungua mara ya kwanza, na wasichana balehe wahimizwe kushiriki.  Wanajamii wengine wote ambao wanahusika na masuala ya  afya ya mama na mtoto mchanga, wakiwemo wanaume, wanawake wenye umri mkubwa na viongozi wa jamii pia wanastahili kuhudhuria na wataeleweshwa juu ya shabaha ya  vikundi hivi  ambayo ni  wanawake.  Vikundi vitaongonzwa na mwezeshaji wa kike  kupitia  mzunguko wenye awamu 4 za  mikutano. Mwezeshaji huyu  (Esther  Rehema), atasaidiwa na Msimamizi, (Alex Gongwe), Kiongozi wa Mradi, (Wilbard Mrase), na Mwenyekiti wa Mradi, (Isaac Mgego).


MUUNDO  WA  KIONGOZI  HIKI

Kiongozi hiki ni kwa ajili ya watumishi wote wa Mradi wa  Tushikamane ili waweze kuelewa mambo ambayo yanahitaji kufanyika, na namna gani. Lakini kimewalenga zaidi Wawezeshaji – kuwaongoza hatua kwa hatua kuunda na kuendesha vikundi. 

Kwa  sababu hii, Kiongozi hiki kimeandaliwa maksudi kwa ajili yako, Esther na Rehema, na ni kama vile kinaongea na ninyi !





VIFUPISHO



VHW            Village Health Worker (Mfanyakazi wa Afya Vijijini)
MNH             Maternal and Newborn Health (Afya ya Mama na Mtoto Mchanga)
TBA              Traditional Birth Attendant (Wakunga wa Jadi)
NGO             Non-Governmental Organisation – eg charities (Shirika lisilo la
                        Kiserikali- mfano  Shirika  la Misaada)


MAJUKUMU  NA  WAJIBU  WAKO

Katika  Mradi wa  Tushikamane, wewe mwezeshaji utakuwa na majukumu kwenye maeneo yafuatayo:
1.    Uundaji wa  vikundi
2.    Utekelezaji wa mzunguko wa mikutano  14, kuainisha matatizo yanayohusiana na vifo vya mama na watoto wachanga na kuweka vipaumbele.
3.    Rufaa kwa ajili ya mama au mtoto yeyote kwenye kituo cha afya kama itaonekana inahitajika
4.    Kujenga mtandao na viongozi wa jamii, wafanyakazi wa afya vijijini, wakunga wa jadi, viongozi wa serikali za vijiji na mitaa na wadau wengine
5.    Kutoa ripoti kwa Msimamizi na kwa Kiongozi wa Mradi – mathalan juu ya idadi ya mikutano; mahudhurio; shughuli ambazo zimekamilika; mafanikio; changamoto; nk.
6.    Kuhudhuria mikutano ya kila mwezi ya timu nzima kwa ajili ya kupokea ripoti hizi, kujadili mafanikio, na kubadilishana mawazo nk.


UELEWA  JUU  YA  AFYA  YA  MAMA  NA  MTOTO  MCHANGA

Ili kuviwezesha vikundi vya  Tushikamane kwa ufanisi na kuwasaidia wanavikundi ipasavyo, utahitaji uelewa wa msingi juu ya masuala ya afya ya mama na mtoto mchanga. Ingawa siyo wajibu wako kuwaelimisha wanakikundi, unahitaji taarifa za kutosha ili uweze kusaidia kujaza mianya katika uelewa wa pamoja, kubainisha vitendo hatarishi na kujibu maswali mahsusi ambayo unaweza kuulizwa. 

Hivyo, unapaswa kuwa na uelewa wa kutosha juu ya masuala yafuatayo ili uweze kuyazungumzia vizuri na kwa kujiamini ndani ya kikundi:
·         Huduma maalum kwa mama na mtoto kabla ya kuzaliwa – ziara ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne
·         Huduma kwa wajawazito nyumbani  – lishe, mapumziko na uzuiaji wa malaria
·         Kujiandaa kujifungua – kituo/hospitali atakapojifungulia, na uwepo wa mtaalam mwenye uzoefu, usafiri, fedha, kufanya maamuzi, vifaa vitakavyohitajika kwa ajili ya uzazi safi na salama, dalili za uchungu wa uzazi
·         Dalili za hatari wakati wa ujauzito
·         Dalili za hatari wakati wa kujifungua
·         Dalili za hatari kwa akinamama baada ya kujifungua
·         Dalili za hatari kwa mtoto mchanga baada ya kuzaliwa
·         Huduma kwa mama na mtoto mchanga nyumbani  – huduma ya nyumbani kwa mama mara baada ya kujifungua, utunzaji wa rulela (kitovu), kuzuia maambukizi, kumuogesha mtoto mchanga, unyonyeshaji maziwa ya mama, chanjo, ulinzi na usalama, huduma ya kangaroo.
·         VVU na UKIMWI  na umuhimu wa wenzi wote wawili kupimwa
·         Uzuiaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
·         Uzazi wa mpango
·         Haki na wajibu wa akinamama na wafanyakazi wa afya

Uelewa  wako juu ya  afya ya mama na mtoto unapaswa kupimwa  na Msimamizi na /au Kiongozi wa Mradi/Mkufunzi. 



UNAPOKUWA  MWEZESHAJI



Kwa nini kutumia neno ‘Mwezeshaji’?

Unaitwa Mwezeshaji siyo kiongozi au mwalimu, kwa sababu kazi yako siyo kuwambia watu kipi cha kufanya, wala kuwafundisha kipi cha kufanya. Badala yake unapaswa kuwasaidia  wao wenyewe kugundua kipi cha kufanya, na wapange ajenda yao wao wenyewe.

Mwezeshaji ni muonesha njia ambaye:
·         huhakikisha kila mtu katika kikundi anamsikiliza mwenzake
·         huuliza maswali ili kukisaidia kikundi kuamua wafanye nini
·         hujenga juu ya uelewa wa wanakikundi ili kuwasaidia wenyewe kutafuta majibu kwa masuali yaliyoko mbele yao
·         ana wajibu wa  kukisaidia kikundi  kutekeleza majukumu yake
·         huruhusu kikundi kujitathmini na kupata picha ya kiwango cha mafanikio yao.

Hupaswi  kuwa:
·         usukani au mwendeshaji wa kikundi;
·         mtaalam wa kikundi;
·         mwenye kujua zaidi kuliko wengine;
·         anayefanya maamuzi yote
·         anayefanya tathmini jinsi kitongoji kinavyoendelea

Katika masuala yote haya, Vikundi vya  Tushikamane ndivyo vinapaswa kuwa usukani; kutafuta utalaam; kuamua kipi ni bora zaidi; kutathmini maendeleo yao; nk.

Unapokuwa  unafanya kazi kama Mwezeshaji, hali hii itatoa fursa kwa kila mtu katika kikundi kueleza mawazo yake na kujisikia kuwa sehemu ya timu. Kwa kuwa kikundi kinafikia maamuzi pamoja, inakuwa rahisi kwa wanakikundi, mmoja mmoja, kusaidia kufanikisha malengo ya kikundi.

Kuliko kuwapa wanakikundi majibu, elimu inapaswa kuwaongezea uelewa ili waweze kubaini matatizo na visababishi vyake, na kuyatafutia ufumbuzi. Jukumu la Mwezeshaji ni  kukisaidia Kikundi kupitia mchakato huu kwa kuuliza maswali ambayo yanachochea njia mpya za kufikiri na kufanya uchambuzi wa  hali zao. Mwezeshaji hana majibu yote. Jukumu lake ni kukisaidia kikundi  kufikiria kwa makini juu ya mahitaji na maslahi ya kikundi, na kufanya maamuzi wenyewe.

Jukumu la Mwezeshaji ni kumtia moyo kila mwanakikundi kuchangia kadri ya uwezo wake. Kila mtu ana maarifa muhimu  na anaweza kutoa mchango muhimu. Lakini watu wengi kawaida hawana utayari wa kuwashirikisha wengine juu ya ujuzi au maarifa yao. Wanaweza kuwa wanakosa ujasiri au kufikiria kuwa yale wanayoyajua siyo muhimu. Wakati mwingine hawataki  kuwamegea wengine  maarifa au taarifa zao kwa sababu  kuyahodhi  huwapa nguvu na fursa zaidi juu ya wengine.

Hata hivyo, tunaposhirikishana maarifa yetu, kila mtu hufaidika. Mtu ambaye anawashirikisha wengine hapotezi maarifa hayo, na mtu anayepokea atakuwa amepokea  nyenzo mpya ambayo pia anaweza kuwashirikisha  wengine. Jukumu la Mwezeshaji ni kujenga hali ya kuaminiana  na kuheshimiana miongoni mwa  wanakikundi na kuchochea majadiliano na kujifunza, ambavyo hunufaisha kikundi kizima.





MBINU   ZA  KUFANYA KAZI NA VIKUNDI



Kutafuta watu wa kijiunga na vikundi
Unapokua unatafuta watu wa kuhudhuria mikutano na kuwatia moyo kuendelea kuhudhuria, unapaswa kujaribu njia mabalimbali zikiwemo:
·         Kwenda na kuandikisha wanakikundi nyumba kwa nyumba,  au kupitia  kamati na mwanakikundi mmoja mmoja
·         Barua kwa watu wanaostahili kuhudhuria
·         Matangazo kwenye mikutano ya vijiji, shughuli na matukio mengine  kijijini
·         Nyimbo na ngoma  kabla ya kuanza mikutano
·         Kueleza kusudi na manufaa ya kuhudhuria mikutano
·         Kueleza kwa nini afya ya mama na mtoto ni muhimu kwa wanawake na jamii nzima
·         Usiwafanye watu kutarajia mambo yaliyo  juu ya uwezo wako au wa programu  – kuwa mkweli juu ya jukumu lako
·         Mikutano  kufanyika  muda na sehemu mwafaka
·         Kusherekhea mafanikio na ushindi, hata ukiwa mdogo

Muhimu: ni jukumu lako  kuwakumbusha washiriki lini mkutano mwingine utafanyika na mada itakayojadiliwa.

Kuweka kanuni ili vikundi viweze kufanya kazi vizuri
Unahitaji kuhakikisha kuwa  wanakikundi  wote wanashiriki kwa usawa, na wanaume na wanawake wenye umri mkubwa wasitawale mijadala. Tunapokua tunahamasisha watu kushiriki kwa bidii kwenye mikutano, kumbuka kwamba watu hawalazimiki kushiriki , lakini wanapaswa kupewa fursa kushiriki iwapo wanataka.

Kuhakikisha kuwa watu wanapata fursa hii, himiza kikundi kujadili na kukubaliana juu ya kanuni  za kuongoza mikutano. Miongoni mwa kanuni  hizi iwe kanuni kwamba kila  mtu ana haki ya kushiriki na kushikilizwa. Himiza wanakikundi kuzingatia kanuni ambazo wamejiwekea  na kuweka mazingira salama kwa ajili ya mikutano. 

Kanuni za msingi zinaweza kujumwisha, kwa mfano:
·         Kuheshimu mawazo ya  kila mshiriki .
·         Washiriki  kuwashirikisha wanakikundi wengine  taarifa  zinazostahili walizonazo.
·         Mikutano itaanza na kumalizika kwa muda uliopangwa na itaanza kwa muda baada ya mapumziko.
·         Kutakuwa na mjadala mmoja kwa wakati mmoja (isipokuwa kama kuna kazi ambazo zinafanyika katika vikundi vidogo).
·         Kikundi chenyewe,(siyo Mradi wa  Tushikamane),ndiyo kinawajibika  kutoa matunda -kuonesha matokeo.
·         Mijadala na ukosoaji ilenge  masilahi ya kikundi  na siyo watu.

Usijilimbikizie  madaraka makubwa  na kukitawala kikundi !
Miongoni mwa matatizo magumu sana ambayo yanaweza kukukabili kama Mwezeshaji  ni  kusawishika kutawala mijadala au kuubadili mchakato wa kikundi.  Mara nyingi jambo hili hutokana na nia nzuri ya kutaka kukisaidia kikundi kusonga mbele. Kama umezoea mtindo wa ufundishaji wa kutoka juu kwenda chini, na hujawahi kupata fursa ya kuwangalia wawezeshaji wazuri wakifanya kazi, inaweza kuwa vigumu kubadili mtazamo wako juu ya  ubadilishanaji  mawazo.

Njia mojawapo ya kukitia moyo kikundi kuchukua usukani wa juhudi zao za kujifunza na maendeleo ni kukiomba kikundi kutayarisha kanuni za msingi za  ushiriki wao ili kila mtu ajisikie huru kutoa mawazo yake. Kanuni kama hizo zinaweza kujumuisha kutoingilia kati   mtu anapokua anachangia, kuheshimu mawazo tofauti, na kukubaliana  idadi ya juu ya pointi ambazo mtu anaweza kuchangia  katika   mjadala mmoja.  Kama  kikundi  kitaandika kanuni hizi, wanakikundi wote kwa pamoja watajisikia kuzimiliki na hivyo  kuhakikisha zinaheshimiwa.   

Njia zingine za kuepuka kutawala kikundi  ni pamoja na:
·         Kuwa na subira
·         Kuwasikiliza wengine na kuonesha  maoni yao yanathaminiwa.
·         Kuwa muwazi katika kujifunza  kutoka kwa wanakikundi wengine  ili ubadilishanaji wa taarifa  utoke  pande zote na kwenda pande zote.
·         Kutia moyo kikundi kuibua njia za ufumbuzi wao wenyewe




Kukabiliana na maswali magumu
Kuweza kuyajibu maswali yote kutoka kwa washiriki  inaweza kuwa kazi ngumu.  Mara nyingi unaweza kujisikia kuwa unapaswa kuwa na majibu yote. Unaweza kuwa huamini uwezo wako katika kujibu maswali juu ya mada fulani. Ni wajibu wa Msimamizi na Kiongozi wa Mradi kukusaidia juu ya jambo hili, na kukusaidia kupata taarifa zaidi, mathalan kutoka machapisho mbalimbali, serikalini au kutoka ofisi za Mashirika yasiyo ya Kiserikali nk.   Wanaweza pia kukusaidia kujifunza kutoka kwa watu  wenye hekima na maarifa katika jamii husika, nje ya kundi lako,ambao wanaweza kuwa na utaalam juu ya mada inayojadiliwa.

Njia zingine za kushughulikia maswali magumu ni pamoja na:
·         Kujiandaa  vizuri kwa ajili ya mijadala ya vikundi  kwa kusoma  kiongozi  hiki na  nyenzo zingine zinazofaa.
·         Hasa, unatakiwa kuwa na uelewa mpana wa  mambo yanayochangia vifo na magonjwa kwa wajawazito  na watoto wachanga.
·         Kutarajia maswali kutoka kwa wanakikundi na kila inapowezekana kufikiria mapema jinsi ya kuitikia.
·         Kama huna jibu kwa swali, usiogope  kusema hujui ! Kwa swali kama hilo, sema utatafuta taarifa zaidi na kuwashirikisha wanakikundi pale jibu litakapopatikana.

Kusimamia migogoro
Wakati mwingine watu wanaweza kuwa  na tofauti kubwa  juu ya jambo. Mivutano ndani ya kikundi inaweza  kuathiri  utendaji  na umoja wa kikundi kwa ujumla.  Unatakiwa kuwa makini katika kutambua mivutano ambayo inaweza kutokea na kuwatia moyo wanakikundi kwa pamoja kuangalia zaidi ya  mivutano hii, wakiweka malengo na maslahi ya watu wote kwanza. Kama tofauti haihusu mada ambayo inajadiliwa, utahitaji kuwasihi  kuweka tofauti hiyo pembeni.

Kanuni za msingi katika usimamizi wa migogoro ni pamoja na:
·         Kutambua na kukubali  uwepo wa mgogoro huo.
·         Jaribu kubaini chanzo cha mgogoro huo.
·         Kama unahusiana na mada inayojadiliwa, wasaidie washiriki kufikia makubaliano, ukiwatia moyo kuheshimiana.
·         Kama mgogoro hauhusu mada inayojadiliwa, na unahusisha tu baadhi ya wanakikundi, watie moyo kusuluhisha tofauti hii baadaye, nje ya mazingira ya kikundi.



Kukabiliana na washiriki wanaopenda kutawala mijadala
Wakati mwingine, mtu mmoja anaweza kuanza kuutawala mjadala, akionekana kujiamini  kuwa anayo majibu  sahihi kwa mswali yote.  Kama hali  hii itajitokeza, unahitaji kuhakikisha kuwa watu wengine pia wanapata fursa ya kuchangia . Njia ya kuliwezesha hili ni pamoja na:
·         Kuwaita wengine kwa majina yao ili nao watoe maoni
·         Gawa kikundi katika vikundi  vidogo kadhaa.
·         Anzisha mfumo wa mgao, ambapo kila mtu atapewa vijiwe 3 au vipande vya karatasi 3, na wanatakiwa kusalimisha kimoja kila mara watakapoongea. Watakapoishiwa, hawataweza kuongea tena!
·         Anzisha mfumo wa kuweka muda  ambao mtu hatakiwi kuuvuka anapochangia. Kila mtu anaweza kuongea kwa muda usiozidi dakika moja kwa wakati. Muda huo unapofika anatakiwa kutoa nafasi kwa  mwanakikundi mwingine kuongea.
·         Tumia ‘fimbo inayoongea’. Yeyote atakapokuwa ameshika fimbo hiyo ndiyo yeye peke anayeruhusiwa kuongea. Atakapomaliza kutoa mawazo yake, atakabidhi fimbo kwa mtu mwingine  ambaye anataka kuchangia. Watakapomaliza  kutoa mawazo yao, watakabidhi  fimbo kwa mwingine  ambaye angependa kuongea.
·         Kaa karibu na mtu ambaye anaongea sana, siyo kwa kuangaliana! Ukikaa kwa kuangaliana na mtu mwingine, hasa mtu ambaye anapenda sana kutawala mijadala, unajikuta unamuangalia sana, na yeye huhisi kuwa unaongea naye mahsusi.

Kufanya kazi na watu wenye aibu
Wakati mwingine watu wanaweza kuona aibu au kuogopa kutoa maoni yao mbele ya kikundi. Hii, hasa, inaweza kuwa ngumu zaidi mnapokua mnajadili masuala ya afya ya akinamama na watoto wachanga kwa sababu baadhi ya wanawake na wasichana balehe hupata tabu kujieleza mbele ya watu wengine, hususan kama ni wanafamilia wenzao. Njia moja wapo y ya kuwatia moyo watu wenye aibu au waoga ni kurejea na kutumia mawazo yao waliyoyatoa huko nyuma, ili wajue kuwa ni muhimu na yanathaminiwa. 

Pia, unaweza :
·         Kuomba watu kuyajadili maswali kwanza wakiwa wawili wawili.
·         Tumia njia  za vitendo kama vile  watu kuchora ramani au picha za mawazo yao na kuzihusianisha na picha za mawazo ya watu wengine,  kupanga  vitu au masuala husika na kuyapa namba kwa kutanguliza yaliyo muhimu zaidi, na  kuandaa ratiba inayruhusu washiriki  kutoa maoni yao.
·         Kuongea na watu wenye aibu peke yao pembeni baada ya mkutano ili kupata mawazo na mchango wao.
·         Kuwatia moyo mmoja mmoja, ndani na nje ya kikundi
·         Kuongea nao nje ya kikundi, na kutafuta sababu za ukimya wao.
·         Kutoa taarifa juu ya mada itakayojadiliwa mapema ili wapate muda wa kujiandaa.
·         Mpe mtu mwenye aibu mwenye uwezo  wajibu wa kutunza kumbukumbu na kutoa mrejesho.
·         Wape muda- wanaweza kuzoea na aibu kupungua.
·         Tumia igizo dhima kuwajengea moyo wa kujiamini na stadi mbalimbali zikiwemo za mawasiliano.

Hasa katika hali ngumu, inaweza kuhitaji kuunda vikundi tofauti vya kujifunza na utendaji shirikishi(PLA groups)kwa ajili ya makundi tofauti yaliyopo ndani ya jamii. Kwa mfano, kikundi mahsusi kwa ajili ya wanawake walio katika umri wa uzazi na  kingine kwa ajili ya wasichana balehe. Uamuzi huo utasababisha ongezeko la kazi kwako.Hivyo, uamuzi huo unatakiwa kuchukuliwa tu baada ya kutafakari kwa makini na baada ya njia zingine zilizopendekezwa kujaribiwa na kushindwa.



MZUNGUKO WA MIKUTANO YA VIKUNDI VYA  TUSHIKAMANE


Awamu na Mikutano
Mzunguko wa vikundi vya  Tushikamane una awamu 4 na jumla ya mikutano 14 :

Awamu ya  1:
Mkutano wa  1: Kuunda kikundi – Kitongoji kizima kikutane kuanzisha mchakato
(Kutoka hatua hii, kwa Awamu ya  1 na  ya 2, Kikundi cha  Tushikamane kitakuwa na wanawake tu!)
Mkutano wa  2: Wanawake kubainisha matatizo ya afya ya wanawake.
Mkutano wa  3: Wanawake kubainisha matatizo ya afya ya watoto wachanga
Mkutano wa 4: Wanawake kuainisha matatizo yatakayopewa kipaumbele
Mkutano wa 5: Wanawake kubainisha mambo yanayochangia matatizo ya afya ya wanawake na watoto wachanga

Awamu ya  2:
Mkutano wa  6: Wanawake kubainisha shughuli za uzuiaji na usimamizi wa matatizo ya afya ya wanawake na watoto wachanga
Mkutano wa  7: Wanawake kujadili mipango  ya kutatua matatizo yaliyoainishwa.
Mkutano wa  8: Wanawake kuwasilisha taarifa za maendeleo  kwa jamii nzima

Awamu ya  3:
Mkutano wa  9: Kupanga ufumbuzi – katika hatua hii wanaume na wahusika wengine muhimu wanaweza kujiunga na kikundi
Mkutano wa  10: Kutafuta rasilimali, halafu  kuzikusanya
Mkutano wa 11: Kuandaa zana za ufuatiliaji

Katika hatua hii, jamii itaanza utekelezaji wa njia za ufumbuzi walizozichagua,
(kwa msaada wowote watakaoweza kupata ili  kuongeza uwezekano wa mafanikio).

Awamu ya  4:
Mkutano wa  12: Kuandaa zoezi la kutathmini matokeo ya mchakato wa vikundi vya  Tushikamane
Mkutano wa  13: Kukusanya taarifa kwa ajili ya tathmini, halafu kujadili matokeo ya Mradi juu ya afya ya wanawake na watoto wachanga
Mkutano wa  14: Kupanga kwa ajili ya siku zijazo – kwa mfano, jamii inaweza kutaka  kuurudia tena mchakato huo!


RIPOTI

Ripoti ya mkutano
Unapaswa kuandaa ripoti ya mkutano kila baada ya mkutano kufanyika.  Hii itachangia ripoti yako ya kila mwezi. Katika maelezo yafuatayo ya kila mkutano, kuna vipengele ambavyo ripoti yako inapaswa kuzingatia.

Ripoti ya mwezi
Ripoti yako ya kila mwezi inapaswa kuwasilishwa kwa Msimamizi kila mwisho wa mwezi. Taarifa zinapaswa kukusanywa kutoka kwenye  kumbukumbu zako za mwezeshaji, sajala ya kikundi na ripoti za mikutano.

Unapaswa kuandaa ripoti yako ya mwezi kwa kila kitongoji unapofanyia kazi. Masuala muhimu ambayo unatakiwa kuelezea  ni pamoja na:
·         Idadi ya mikutano iliyofanyika
·         Mahudhurio katika  mikutano (idadi inapaswa kuwa kati ya  10 na  30).
·         Kuna wajawazito wangapi kwenye kikundi ? Je mmeweza kuwafikia wanawake walio kwenye umri wa uzazi, hasa wajawazito na wanawake ambao ndio wamejifungua mara ya kwanza, pamoja na wanawake ambao wameolewa hivi karibuni na wasichana balehe. Je, wanawake wenye hadi duni na walio pembezoni au ambao wametengwa kwa vigezo mbalimbali wamehimizwa kujiunga na kikundi ?
·         Ni wanajamii gani wengine wameweza kuhudhuria ?
·         Je kuna wajumbe wa kamati ya kikundi ambao wamejitoa  na hivyo kuwepo haja ya kuchagua wengine na kutoa mafunzo wa wanakikundi wapya ?
·         Je kikundi kinaendelea vuzuri kulingana na ratiba katika kukamilisha mzunguko mzima wa mikutano katika kipindi cha miezi 12 hadi  24 ?
·         Zana na njia ambazo zinatumika kuviwezesha vikundi zinakubalika na zinawafaa wanakikundii?
·         Muda na sehemu mikutano ya vikundi inapofanyikia zinafikika kwa urahisi na wanakikundi wanaotaka kuhudhuria?
·         Rasilimali zilizopo kwa  vikundi zinatosheleza kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zao kwa mafanikio?
·         Je masuala yanayojadiliwa kwenye mikutano yanalingana na matarajio?  Kwa mfano, wanabainisha matatizo yanayotarajiwa?  Je, wanapanga kutekeleza shughuli za ufumbuzi unaotarajiwa?


Kusambaza taarifa
Kati ya mikutano, unapaswa kuitembelea jamii, kwa lengo la  kukutana na watu ambao hawajashiriki, na pia kuwahimiza wanakikundi  kuwashirikisha wenzao ambao wanashindwa kuhudhuria   juu ya masuala yanayojadiliwa kwenye mikutano.





AWAMU YA  1: KUBAINISHA  MATATIZO PAMOJA

Dhumuni la Awamu ya  1
Shabaha ya awamu ya kwanza ya mzunguko wa mikutano ni vikundi kubainisha matatizo ya akinamama na watoto wachanga na  vipaumbele.
Awamu ya kwanza ina mikutano 5,ambayo hufanyika kwa utaratibu ufuatao:
·         Mkutano wa  1: Kuunda kikundi
·         Mkutano wa  2: Kubainisha matatizo ya afya ya akinamama
·         Mkutano wa  3: Kubainisha matatizo ya afya ya watoto wachanga
·         Mkutano wa  4: Kuainisha matatizo gani ya afya ya akinamama na watoto wachanga yatakayopewa kipaumbele.
·         Mkutano wa  5: Kubainisha mambo yanayochangia matatizo hayo




MKUTANO WA 1: KITONGOJI  KUKUTANA  KUUNDA  KIKUNDI

Nani anapaswa kuhudhuria mkutano wa  1?
Kabla mchakato wa  Tushikamane haujafikia hatua ya kuunda vikundi ndani ya kitongoji, kunahitajika kuwepo mkutano  wa wadau wote  ambao wanastahili kushiriki katika mchakato huo katika kitongoji husika.

Wadau hao ni pamoja na:
          Wanawake vijana na akinamama na wajawazito– hususan wale ambao wanatoka kwenye familia ambazo zimewahi kumpoteza mama kutokana na matatizo ya uzazi, au  kumpoteza mtoto mchanga
          Wanawake wenye ‘sauti’ ya nguvu ndani ya kitongoji – mathalan waalimu, wanawake katika  nafasi za uongozi, na pia wanawake wenye vipaji vya kuzaliwa vya uongozi.
          Viongozi wa kiutamaduni na viongozi wa kuchaguliwa katika kitongoji
          Viongozi wa dini
          Wafanyakazi wa afya vijijini
          Wataalam wa tiba za jadi
Mitandao ya vikundi vya kijamii, au mashirika yasiyo ya kiserikali  au asasi zingine  ambazo zinafanya kazi katika kitongoji husika nk.

Ufafanuzi juu ya mkutano wa kwanza wa kitongoji
Mkutano huu wa kwanza wa  kitongoji unaweza kuchukua saa 2. Mkutano unapaswa kufanyika sehemu iliyo kati na yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya watu wote.

Dhumuni la mkutano ni kupata azmai na ushirikiano wa  watu watakaohudhuria  juu ya mchakato wa Tushikamane.

Hii itahitaji kuanza kwa kueleza  Tushikamane inahusu nini: kuwapa wanawake – hususan wanawake walio kwenye umri wa uzazi, sauti katika kujadili jinsi ya kupunguza vifo vya akinamama na watoto wao wachanga. Hii itapelekea, hatimaye, kupanga pamoja na kitongoji kizima mambo  ambayo yanapaswa kushughulikiwa,  na namna gani.

Matarajio   ni kwamba  yataibuliwa  mawazo mazuri, pamoja na vipaumbele vya kufanyia kazi ambavyo vitaivuta jamii nzima kufanya kazi pamoja ili kupunguza vifo hivyo vya kusikitisha. Wanapaswa kutambua kuwa kwa kufanya hivyo, manufaa mengi zaidi yataanza kuonekana ndani ya jamii.

Hii ni njia bora zaidi ya kufanya kazi kuliko wageni kuja na kufanya mambo ambayo huenda hayaafikiwi  na watu wote; ambayo yanaweza kusababisha mgawanyiko, kukosa kuungwa mkono na jamii au kuwa endelevu, au ambayo hayakabiliani ipasavyo  na mizizi halisi ya vifo hivyo vya kusikitisha.

Mambo ambayo yanaweza   kujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na:
·         Madhara na athari kwa  jamii kutokana na kifo cha  mama.  
·         Watu waliohudhuria wana  raslimali, lakini wanahitaji kufanya kazi pamoja ili waweze kuvutia misaada kutoka nje inayolenga matatizo yao halisi.
·         Watu waliohudhuria hawapaswi kuogopa   kutenga muda wao  ili kujishughulisha na kikundi.
·         Mchango  wao kwa ujumla na uongozi bora  vitakuwa vigezo muhimu katika  kuleta mafanikio. 
·         Mchango wao na ushirikiano wao wakati  wa kukazia au kuzamisha  ufumbuzi  ndani ya jamii vitakuwa vigezo muhimu, siyo tu kuhakikisha mafanikio bali pia  uendelevu.  Mafanikio endelevu yatakapobainika kwa wakala wa  nje, kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kutoa misaada zaidi siku zijazo kwa jamii ambayo imejiwekea ajenda yake ya maendeleo, na inafanya bidii  kukamilisha utekelezaji wa shughuli  za kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Hawahitaji kuahidi chochote katika hatua hii, lakini wanapaswa kuelewa kwamba kuna wakati  wanaweza kutafutwa kuombwa  kuunga mkono mradi kwa hali na mali.

Ajenda ya mkutano wa kwanza wa kitongoji
Ajenda iliyopendekezwa kwa ajili ya mkutano huo ni kama ifuatayo:
1.    Makaribisho-kufanywa na Mwenyekiti wa Mradi, Mchungaji  Mgego
2.    Utambulisho-kufanywa na Kiongozi wa Mradi, Wilbard Mrase
3.    Malengo ya mkutano-kuelezwa  na Msimamizi wa Mradi, Alex Gongwe

4.    Mada ya dakika 20 juu ya programu ya  Tushikamane -kuwasilishwa na Mwezeshaji wa Mradi – Esther Paul au Rehema Semwali

(Wakati wa zoezi hili, unapaswa kueleza kuwa wakati wa mzunguko wa mikutano, kila mtu atashiriki kwa usawa, na wanaume na wanawake wenye umri mkubwa zaidi wasitawale majadiliano. Ili kuruhusu wanawake washiriki kikamilifu, wawezeshaji wanaweza kuwaomba  wanaume kuchangia  mwishoni baada ya kikundi kukamilisha mijadala ya mkutano. Pia  eleza kuwa wafanyakazi wa afya kwenye jamii  na  maafisa wengine wa afya na serikali za mitaa na vijiji wataalikwa kwenye mikutano na  kupewa muda na nafasi ya kuongea na wanakikundi.)

 5. Maswali, maoni na mawazo kutoka kwa wasikilizaji;
(Baada ya mada kuwasilishwa, washiriki wanapaswa kupewa muda mzuri kwa ajili ya maswali na majibu juu ya masuala mbalimbali yaliyowasilishwa. Mkutano pia ujadili jinsi gani washiriki   watakavyoweza kuusaida mradi kama wataombwa kufanya hivyo – mathalan ,kutoa ushauri jinsi  ya kuboresha hali ya usafi wa mwili na mazingira kijijini, ushauri juu ya ya kuinua kilimo cha mashamba madogo madogo au jinsi ya kukabiliana na  mahitaji mbalimbali kutoka kwa jamii .) 

  6. Njia za ufumbuzi ambazo vikundi vya  Tushikamane vingependa kutekeleza;
(Kutokana na uzoefu, njia za kawaida  za ufumbuzi ambazo zimebainishwa na kutekelezwa na makundi ni pamoja na : kutoa elimu ya afya; huduma ya usafiri; kuanzisha mfuko wa kikundi; kuhimiza vifaa safi kwa ajili ya kujifungua; kuhimiza shughuli za uzalishaji pato; kushughulikia mahitaji ya wakunga wa jadi yakiwemo  mafunzo; kuimarisha ushirikiano na ushawishi wa vituo vya afya; kuhimiza kilimo cha bustani za mbogamboga; kuhimiza matumizi ya viandarua vya kuzuia mbu na usambazaji wake.)

7.Majadiliano  jinsi gani washiriki wanaweza kuusaidia mradi
8. Kuongoza  uundaji  wa kikundi
(Kamati ndogo ya uongozi inapaswa kuundwa kutokana na washiriki kwenye mkutano. Jukumu la kamati hii ni kumsaidia  Mwezeshaji na kumpatia  ushauri  atakapokuwa anatekeleza programu ya   Tushikamane.  Mwezeshaji atakutana na kamati ya uongozi mara kwa mara ili kutoa mrejesho na kupata msaada na ushauri. Wakati mwingine Msimamizi, Alex Gongwe, atahudhuria mikutano ya Kamati Ndogo ya Uongozi. Kunatakiwa kuwepo Kamati Ndogo ya Uongozi moja tu katika kila kitongoji – kamati moja kwa kila kikundi cha Tushikamane.)
9. Majumlisho—kufanywa na  Wilbard Mrase
10. Ufungaji  wa mkutano -kutolewa na Mchungaji  Mgego
11. Kufunga.



Kubainisha huduma ambazo  programu ya Tushikamane itatoa  - na ambazo haitatoa
Kabla mkutano haujaisha, na mchakato wa Tushikamane kuanza rasmi, kunahitajika kuwepo uelewa bayana kwenye jamii juu ya huduma ambazo programu ya Tushikamane itatoa na  ambazo haitatoa :

Huduma ambazo zitatolewa kwa kila kitongoji:
·         Mwezeshaji aliyepitia mafunzo atawezesha uanzishaji wa kikundi cha  Tushikamane na kuongoza  mikutano ya Kikundi.
·         Msimamizi ambaye atamsaidia Mwezeshaji kufanikisha shughuli za Kikundi.

·         Mara mchakato utakapofikia kiwango cha kitongoji kuwa kimefanya uchambuzi wa matatizo ya msingi ambayo yanasababisha vifo vya mama na watoto wachanga, na kimeweka vipaumbele ambavyo vinapaswa kufanyiwa kazi ili kupunguza matatizo hayo, programu ya  Tushikamane itajaribu kusaidia kukiunganisha kitongoji na wadau wengine ambao wanaweza kusaidia. Mathalan, vitongoji vingine ambavyo vinapambana na matatizo kama hayo; juhudi au programu zingine  zinazostahili, au na mashirika mengine ya  misaada  yenye dhamira ya kusaidia juhudi  kama hizo ambazo zimepangwa  na Kikundi cha Tushikamane.

Mifano
Kwa mfano, kitongoji kinaweza kuweka kipaumbele juu ya ufumbuzi wa tatizo la usafiri ili kusaidia kuwafikisha  wajawazito   hospitalini haraka. Huenda vitongoji vingine pia vimeweka kipaumbele juu ya suala la usafiri. Programu ya Tushikamane inaweza kusaidia kuziunganisha jamii hizo na shirika la  misaada lenye uwezo wa kutoa pikipiki maalum ya kubeba wagonjwa, mara  shirika hilo litakapojihakikishia kuwepo huduma za matunzo ya kifaa hicho na hata mtu wa kukiedesha kitongojini hapo.


Mifano mingine ni pamoja na:
·         Kuwaongezea stadi za utendaji  – mfano kuanzisha programu endelevu  ya mafunzo kwa wakunga wa jadi.
·         Huduma za afya – mfano kuanzisha huduma za chanjo  zinazopatikana kwa urahisi, huduma ya kupima msukumo wa damu(presha), kutibu  anemia, nk; au  kuisaidia jamii kukubali uzazi wa mpango, na kutoa huduma husika.
·         Kilimo na chakula  – mathalan kuanzisha na  kupanua huduma za ziada za lishe kwa ajili ya  watoto wanaolikizwa.
·         Elimu  – mathalan  kuboresha elimu kwa akinamama juu ya afya wakati wa ujauzito.
·         Afya ya mazingira na usafi wa mazingira hususan huduma ya vyoo – mathalan kufanya kazi pamoja katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama.


Programu ya TUSHIKAMANE haitatoa huduma zifuatazo:
·         Misaada ya kifedha au posho za aina yote kutoka kwa timu ya  Tushikamane yenyewe.
·          Bakshishi
·         Kuwafanyia wanajamii kazi  mbalimbali bila wao wenyewe kushiriki. Msaada wowote utakaotolewa  utategemea   juhudi za jamii yenyewe kujitegemea, na ushiriki wake. Misaada haitategemea fikra za wageni juu ya mahitaji ya jamii. Misaada ‘haitabwagwa’ tu kwenye  kitongoji.


Kuunda kamati ya uongozi
Kamati ya uongozi itasaidia kuifanya kazi yako kuwa rahisi zaidi, na kuimarisha uwezo wa jamii kujiamulia. Unapaswa kusaidia kikundi kuunda kamati ya uongozi mwishoni wa  mkutano wa kwanza. Kamati hiyo, kwa msaada wako, itasaidia kuendesha shughuli za kikundi.

Kamati inapaswa angalau kuwa na mwenyekiti na katibu. Baada ya hapo, wanaweza kuhitaji mweka hazina. Kadri muda unavyokwenda, kamati itaendelea kuongezewa wajumbe hadi kufikia wajumbe 5 hadi  10 watakaoendesha kikundi na kufanikisha shughuli zake. Kwenye kamati, wawepo wanaume, lakini wasizidi  2 katika kamati ndogo, au  3 katika kamati kubwa.

Jukumu la mwenyekiti ni kuongoza kikundi, na huyu anapaswa kuwa  mwanamke.  Jukumu la mwenyekiti linajumuisha kutoa mwongozo na dira, kusimamia wajumbe wa kamati na wanakikundi, na kukiwakilisha kikundi katika majukwaa ya kijamii, kiwilaya na kitaifa.

Jukumu la katibu ni kutunza kumbukumbu za shughuli zote za kikundi. Jukumu hili linajumuisha kujaza rejesta ya kikundi  baada ya kila mkutano.

Jukumu la mweka hazina ni kufuatilia fedha za kikundi na rasilimali zingine za kikundi.

Jukumu la wajumbe wote wa kamati ni kushawishi wanajamii kujiunga na kikundi na kushiriki katika mikutano.Wahimize wanakikundi kujadili na kuchagua wajumbe wa kamati kwa kupendekeza na kuunga mkono pale  mjumbe aliyependekezwa anaoonekana anafaa.   

Kimsingi, wajumbe wa kamati wanapaswa kuwa na uzoefu na /au stadi za uongozi. Watabeba wajibu wa  kuhakikisha shughuli za kikundi zinatekelezwa, kutatua migogoro au tofauti na kukipa dira  kikundi. Wataweza  mkazo katika kutekeleza shughuli mbalimbali kwa maslahi ya kikundi, siyo kwa maslahi binafsi.

Watakusaidia kutimiza majukumu yako.  Kadri kikundi kitakavyoendelea na shughuli zake, wajumbe wa kamati wanaweza pia kusaidia uwezeshaji wa  baadhi ya mikutano kama unakuwa hupo.


Masuala ya muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 1
·         Rejesta inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wajumbe wangapi walihudhuria,wanawake walikua wangapi, wangapi walikua na ujauzito?
·         Mkutano uliendeleaje – mafanikio yoyote au matatizo?
·         Wajumbe wa kamati ya uongozi ni nani ?
·         Ni kanuni gani ambazo zimewekwa kwa ajili ya uendeshaji wa mikutano?


Nini kifanyike baada ya mkutano wa kwanza
Unapaswa kuwaorodhesha wote waliohudhuria  katika rejesta ya kikundi.  Yote yakienda vizuri, kuanzia mkutano unaofuata hii itakuwa kazi ya katibu ambaye atachuguliwa wakati wa mkutano huu.


MKUTANO WA  2 – WANAWAKE VIJANA  (WENYE UMRI MDOGO) KUBAINI MATATIZO YA AFYA  YA  AKINAMAMA

Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa  2?
Mchakato wa Tushikamane unahusu kuzuia vifo vya kusikitisha vya wanawake na watoto wachanga, hasusan vinavyohusiana na uzazi. Hivyo, wanawake walio katika umri wa uzazi wanapaswa kuwa ndiyo washiriki  wakuu wa mkutano huu wa  2, ili waweze kuanza kubainisha matatizo ya msingi yanayosababisha vifo hivyo.

Uanachama katika kikundi utaamuliwa na wanawake hao wenyewe. Hata hivyo,wanapaswa kuhimizwa kuwapa kipaumbele wajawazito na akinamama ambao ndiyo wameanza uzazi, pamoja na wanawake ambao wameolewa hivi karibuni na wasichana balehe.  Wanapaswa pia kukumbushwa kuhakikisha kuwa wanawake wenye hali duni na ambao wametengwa kwa vigezo mbalimbali wanaalikwa  kuhudhuria.

Wakunga wa Jadi, kwa umuhimu wa pekee, wanapaswa kualikwa kuwa sehemu ya mchakato huu kuanzia mwanzoni.

Kama Mfanyakazi wa Afya Kiijijini ni mwanamke na anajiona sehemu ya jamii, basi   naye anapaswa kuhudhuria. Kama mfanyakazi huyu, mathalan, ni mwanaume mwenye umri mkubwa ambaye haishi kwenye kitongoji husika, basi wanawake wanaweza kupenda kumshirikisha kwenye mchakato baadaye.

Hata hivyo, ni muhimu kulegeza masharti  ya uanachama kwenye kikundi, mathalan, kuwaruhusu wanawake maarufu wenye umri mkubwa,  na viongozi wa dini  ambao wanaweza  kushawishi jamii kuviunga   mkono  vikundi vya Tushikamane na shughuli zake.


Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa  2
Tembelea watu maarufu  kwenye kitongoji  waliohudhuria mkutano wa  1. Wafanye wajisikie ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Kadri mkutano utakapokaribia, wakumbushe watu tarehe na muda wa mkutano, na mahali utakapofanyika, na kuwahimiza kuhudhuria. Kwa kuwa ni vigumu kutunza muda, chagua muda mwafaka, ili kuwarahisishia  wanawake kuhudhuria.


Ajenda ya Mkutano wa  2
1.    Makaribisho; utambulisho; na kupitia mhutasari wa kikao kilichopita.

2.    Kukubaliana ni katika hatua gani wanawake wangehitaji wanaume na watu wengine maarufu kwenye kitongoji kujiunga na mchakato huo. Muda utakaopendekezwa kuwashirikisha watu hao uwe baada ya Mkutano wa 8. Kabla ya hapo, wanawake watakuwa wanajadili masuala ya ndani ya kike, na pia wakijaribu kutafuta ufumbuzi unaowezekana miongoni mwao, pasipo mijadala hiyo  kugubikwa na  wingu wa wanaume.

Mkutano wa  8 ndiyo mkutano mahali ambapo  mrejesho juu ya maendeleo wa mchakato hutolewa kwa jamii. Baada ya hapo, ni jambo zuri kupanua wigo wa kikundi na kuwaingiza watu wengine ambao wanaweza kuchangia kupunguza matukio ya vifo vya mama wakati wa kujifungua, na kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Baada ya hapo, kikundi kitahitaji kuzingatia  mila na desturi; lakini  mikutano inaweza kuwahusisha pia wafanyakazi wa afya vijijini au aina yoyote ile ya wafanyakazi wa afya; viongozi wa jamii; waalimu; wenzi wa wanawake au wasichana balehe kwenye kikundi; wafanyakazi wa serikali au mashirika ya misaada; na yeyote ambaye angependa kuchangia kuboresha afya ya mama na watoto.
3.    Kuwasilisha malengo ya mkutano:
·         Kujadili hali halisi ya  matunzo  ya mama  nyumbani kuhusiana na uzazi na akinamama huwa wanafanya nini wanapohitaji huduma zingine za afya.
·         Kubainisha matatizo ya afya yanayowakabili wanawake wakati wa ujauzito, wanapojifungua, na baada ya kujifungua.

4.    Kujadili namna  akinamama hujipanga kwa ajili ya ujauzito wao na kujifungua - ni wakati gani na katika mazingira gani  huamua  kutafuta huduma na misaada ya kiafya. Pia mkutano utajadili ni  katika mazingira gani wanapojifungulia nyumbani.

5.    Kujadili umuhimu wa kubainisha matatizo – Wakumbushe wanawake kwamba ni muhimu kubainisha matatizo yanayowakumba akinamama kuhusiana na uzazi  na watoto wachanga kwa sababu:
·         Wanawake wengi huugua na kufariki kila mwaka kuhusiana na uzazi, na baadhi ya vifo hivi vinaweza kuzuiwa na jamii zao.
·         Matatizo ya afya yanapaswa kubainishwa kabla ufumbuzi haujatafutwa
·         Wanajamii, hususan wanawake, na wana haki na wapo katika nafasi  nzuri zaidi  kubainisha matatizo ya afya yanayowaathiri  (ingawa wanaume pia wana wajibu muhimu na wanapaswa kusikilizwa na hata kushirikishwa katika mipango hiyo).

6.    Kuongeza uelewa juu ya matatizo muhimu ya afya ya mama na watoto wachanga ambayo huwakabili akinamama wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua, na baada ya kujifungua na njia muhimu za kupunguza matatizo hayo. Tumia kadi za picha za matatizo kusaidia(Matatizo makuu ni kutokwa damu nyingi; mtoto kushindwa kupita kwenye mfupa wa pango la nyonga wakati wakuzaliwa; kondo la nyuma kuchelewa kutoka baada ya mtoto kuzaliwa; malaria; anemia ambayo huzidisha matatizo mengine; na mkao mbaya wa mtoto katika tumbo la uzazi wakati wa uchungu wa uzazi.)

7.   Shughuli kuu za mkutano: Wezesha wanawake katika kikundi hicho kubainisha matatizo ambayo yanawaathiri wanawake katika jamii hiyo wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua, na baada ya kujifungua.  Mara hii tena, tumia kadi za picha za matatizo.

8.    Toa majumlisho ya mkutano na chunguza iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini katika mkutano ujao?

9.    Karibisha maswali.

10. Panga tarehe ya mkutano ujao.


Jinsi ya kuwezesha mjadala juu ya matatizo ya afya ya akinamama
Taarifa kuhusiana na  matatizo ya afya ya akinamama zinaweza kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali  vikiwemo: uzoefu binafsi na shuhuda; vifaa vya kampeni za afya kwa umma; vituo vya kutolea huduma za afya;na kutoka watu tofauti mathalan wanume na wanawake kitongojini, wakunga wa jadi, wafanyakazi wa afya vijijini, na watalaam wa afya wengine.


Eleza kwamba matatizo ya afya yanayolengwa ni yale yanayowaathiri wanawake na watoto wachanga na kusababisha kuugua au hata vifo. Inaweza kuwa rahisi kuyajadili matatizo hayo kwa kufikiria zile hatua  4 ambapo matatizo hayo kujitokeza: wakati wa ujauzito, mara baada ya kujifungua na hadi mwezi 1 baada ya mtoto kuzaliwa.

Hivyo unaweza kuanza kwa kukiuliza kikundi  juu ya matatizo ambayo hujitokeza kabla ya kujifungua. Tumia kadi za picha za matatizo kuibua mawazo. Tunza kumbukumbu ya mambo muhimu kutokana na mjadala.

Kumbuka, hakuna majibu yasiyo sahihi. Kikundi kinapaswa kuhimizwa kuorodhesha matatizo yote ya afya watakayofikiria. Baadhi ya matatizo yamejificha, yakiwemo ukatili wa kingono(ubakaji) na virusi vya UKIMWI(VVU). Wahimize wanawake binafsi kuomba  msaada kama matatizo ambayo wanataka kueleza yanahitaji faragha.

Baada ya mkutano, kikundi kinaweza kuendelea kuongeza kwenye orodha matatizo mengine zaidi kadri yatapokuwa yakibainishwa.

Kwa kila tatizo, hakikisha linafafanuliwa kwa ukamilifu hadi kikundi kiweze kukubali kuwa  ni tatizo au la.


Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa  2
·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·         Mkutano uliendaje – je kulikuwa na mafanikio au changamoto zozote?
·         Matatizo gani ya afya ya akinamama yalibainishwa?

Nini cha kufanya baada ya Mkutano wa  2
Makatibu wanapaswa kuorodhesha washiriki  wote kwenye rejesta ya kikundi.
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano, ikiwa na  kumbukumbu ya matatizo yote yaliyoibuliwa. Pia wahimize wanakikundi  kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano.

MKUTANO WA  3 – WANAWAKE VIJANA ( WENYE UMRI MDOGO) KUBAINISHA MATATIZO YA AFYA KABLA MTOTO HAJAZALIWA


Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya mkutano wa  3
Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu muhimu kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  2. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga namna ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Wakumbushe wanawake kuwa mkutano unaokuja unakusudia kujadili  matatizo yanayohusiana na vifo vya watoto.

Mkutano utapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha wale walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.

Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa 3 ?
Wanawake wote waliohudhuria mkutano wa  2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Pia, kwa vile sasa wana uelewa zaidi juu ya mchakato huu, unaweza kushawishi wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria  – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na  wana uwezo  wa kuwashawishi wengine.

Ajenda ya  Mkutano wa  3
1.    Makaribisho, utambulisho na mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita.

2.    Wasilisha malengo ya mkutano:
·         Kujadili hali halisi ya matunzo ya watoto wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, ikijumuisha wakati wanapojifungulia nyumbani; na mazingira ambamo akinamama hutafuta misaada ya kiafya kwa ajili ya watoto wao wachanga.
·         Kubainisha matatizo ya kiafya yanayowakumba  watoto wachanga wakati wa ujauzito, wanapokuwa wanazaliwa na baada ya kuzaliwa.

3.    Kujadili hali halisi ya matunzo ya watoto wachanga wakati na baada ya kuzaliwa.

4.    Kujadili umuhimu wa kubainisha matatizo-kumbuka ni muhimu kubainisha matatizo yanayowaathiri mama na watoto wachanga kwa sababu:
·         Watoto wengi wanaotoka kuzaliwa huugua na kufariki kila mwaka na baadhi ya vifo hivyo vinaweza kuzuiwa na jamii zao.
·         Matatizo ya afya yanahitaji kubainishwa kabla ufumbuzi haujatafutwa.
·         Wanajamii, hususan, wanawake, wako katika nafasi nzuri zaidi  na wana haki ya kubainisha matatizo yanayowaathiri watoto wao wachanga, (ingawa wanaume nao wana jukumu na wanapaswa   kushirikishwa).

5.    Kuongeza uelewa juu ya matatizo makuu ambayo yanawaathiri watoto wachanga wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, na njia za ufumbuzi. Tumia  kadi za picha za matatizo. Matatizo makuu ni pamoja na: baridi -watoto wachanga  kukosa joto la kutosha; utapiamlo; sepsisi-maambukizi kutokana na  sumu  kwenye damu; kifafa cha mimba; matatizo ya kupumua kwa mtoto mara baada ya kuzaliwa; kuhara; malaria; maambukizi katika mfumo wa kupumua ; -homa ya manjano; na  kuzaliwa kabla ya kutimiza muda wake.

6.   Shughuli kuu za mkutano: Wawezeshe wanawake kubainisha matatizo yanayowaathiri watoto wachanga kwenye jamii wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa, na  baada ya kuzaliwa. Tumia kadi za picha za matatizo.

7.    Fanya majumlisho ya mkutano na kuhakiki iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini katika mkutano ujao?

8.    Himiza washiriki kuuliza maswali.

9.    Panga tarehe ya mkutano ujao.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 3
 • Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
• Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
• Matatizo gani ya afya ya watoto ambao hawajazaliwa  yalibainishwa?


Nini kifanyike baada ya Mkutano wa  3

·         Makatibu wanapaswa kuorodhesha waliohudhuria wote kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano.



MKUTANO WA  4 –  KUAINISHA MATATIZO YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa  4

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu muhimu kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  3. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Wakumbushe wanawake kuwa mkutano unaokuja unakusudia  kujadili  jinsi ya kuyapa kipaumbele matatizo ya vifo vya mama na watoto wachanga, na kuandaa orodha ya mambo muhimu yakufanya ili kukabiliana na matatizo hayo.

Mkutano utakapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa ili kuwezesha wale walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.



Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa  4 ?

Wanawake wote waliohudhuria mkutano wa  3 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Pia, kwa vile sasa wana uelewa zaidi juu ya mchakato, unaweza kushawishi wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria  – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao  wana uwezo  wa kuwashawishi wengine.


Angalia iwapo Wakunga wa Jadi wote wameshirikishwa na vuzuri zaidi wanapanga  kuhudhuria kila mkutano.


Ajenda kwa ajili ya Mkutano wa  4

1.    Makaribisho, utambulisho na mapitio ya mhutasari ya mkutano uliopita.

2.    Wasilisha lengo ya mkutano: Kuainisha matatizo makuu 4 ya afya ya mama na watoto wachanga ambayo yatashughulikiwa katika mzunguko huu.

3.    Kujadili umuhimu wa kuanisha matatizo yatakayopewa kipaumbele. Ni muhimu kuanisha matatizo yatakayopewa kipaumbele kwa sababu:
·         Kuliko kujaribu kushughulikia matatizo yote ya afya kwa mpigo, ni bora kuanza na matatizo muhimu machache.
·         Ni bora zaidi kuanza na matatizo ambayo jamii inahisi kuwa ndiyo muhimu zaidi.
·         Siku za usoni, baada ya  matatizo haya ya kwanza kushughulikiwa, kikundi kinaweza kurudi nyuma na kushughulikia  matatizo mengine yaliyobainishwa.




4. Shughuli kuu za mkutano:  Wezesha wanawake ndani ya kikundi kuainisha matatizo makuu 4 yanayohusiana na vifo vya mama na /au watoto wachanga ambayo yatashughulikiwa katika mzunguko huu. Tumia kadi za picha za matatizo.
Angalia MAELEZO chini jinsi ya kuuendesha mkutano.

5. Fanya majumlisho ya mkutano: Fanya uchambuzi iwapo malengo ya mkutano yamefanikiwa vya kutosha. Kama hayajafanikiwa, unaweza kurudi nyuma na kurudia vipengele vyote au  baadhi ya vipengele vya  mkutano. Angalia iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?
6. Himiza washiriki kuuliza maswali.
7. Panga tarehe ya mkutano ujao.





MAELEZO JUU YA NAMNA YA KUKIWEZESHA KIKUNDI KUAINISHA MATATIZO YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE

1.    Panga kwenye misitari 2 kadi za picha au michoro ya matatizo yote yaliobainishwa: msitari wa kadi za picha zikionesha matatizo ya akinamama, na msitari mwingine wa kadi za picha zikionesha  matatizo ya watoto wachanga.

2.    Wezesha kikundi kujadili sababu tofauti kwa nini tatizola afya linaweza  kuchukuliwa kuwa muhimu. (Tatizo linaweza kuchukuliwa kuwa muhimu kwa sababu: ni tatizo kubwa; au siyo kubwa  lakini limeenea; au kwa sababu lina athari zenye wigo mpana – huathiri nyanja zingine za maisha  zaidi ya afya. Hata kama tatizo siyo kubwa au halijaenea sana, linaweza kuchukuliwa kuwa muhimu kwa sababu, mathalan, linakera kwa kuonekana haliwezi kutatuliwa.)

3.    Omba kila mwanakikundi kuja mbele kwenye misitari ya picha, mmoja mmoja, na kuweka jiwe karibu na tatizo linalowaathiri akinamama  ambalo anadhani ndiyo muhimu zaidi, na lingine linaoathiri watoto wachanga ambalo anadhani ndiyo muhimu zaidi.

Wambie kuwa hakuna jibu lisilo sahihi-majibu yote ni sahihi ! Vyovyote anavyofikiri ndiyo muhimu zaidi kwetu kujua.

4.    Hesabu idadi ya mawe pembeni ya kila tatizo na kuyapanga kwa kuzingatia umuhimu (idadi kubwa ya mawe inamaanisha muhimu zaidi).

5.    Wezesha kubainisha matatizo 2 muhimu zaidi ya akinamama, na matatizo 2 muhimu zaidi ya watoto wachanga.  

6.    Wezesha kikundi kujadili kama wanadhani kuwa matatizo  makuu 4 yaliyotambuliwa yanaaksi ukweli wa hali katika jamii. Angalia kama kikundi kinaafiki  matatizo yaliyobainishwa na wanawake   ni  matatizo  ambayo wanawake kwenye kikundi wanaamini kuwa ndiyo  muhimu zaidi.

Mfano:
Wanawake ishirini katika kikundi cha  Tushikamane, baada ya kubungua bongo, waliibua matatizo 10 yafuatayo ambayo  yanasababisha vifo vya akinamama kuhusiana na uzazi. Baada ya hapo, walipiga kura 1 kila mtu kwa tatizo ambalo walifikiri ndiyo baya zaidi. Kura zilienda kama ifuatavyo:
1.    Kupoteza damu nyingi sana baada ya kujifungua ……… kura 6
2.    Mtoto kushindwa kupita kwenye pango la nyonga………..kura 4
3.    Malaria………………………………………………………… kura 3
4.    Kifafa cha mimba…………………………………………….. kura 2
5.    Anemia…………………………………………………………kura 2
6.    Matatizo yanayohusiana na kondo la nyuma
      kuchelewa kutoka baada ya mtoto kuzaliwa………………  kura 1
7.    Maambukizi baada ya mimba kuharibika ……………….    kura1
8.    Mkao mbaya wa mtoto katika tumbo la uzazi……………   kura 1



Kikundi kilifikiria kuwa matatizo makuu muhimu zaidi ni: kupoteza damu nyingi baada ya kujifungua, na  mtoto kushindwa kupita kwenye  pango la nyonga.

Kura kwa matatizo ya watoto zilikuwa kama ifuatavyo:

1.    Matatizo ya kupumua  mara baada ya kuzaliwa …………kura 7 
2.    Malaria………………………………………..                      kura 4
3.    Maambukizi kwenye mfumo wa kupumua….                    kura 4
4.    Kuhara………………………………………….                      kura 3
5.    Sepsisi(maambukizi kwenye damu kutokanana  sumu )   kura 1
6.    Kuzaliwa kabla ya kutimiza siku……………                         kura1
7.    Utapiamlo………………………………………..                   kura 0
8.    Baridi-halijoto ya mwili kuwa chini ya kiwango
Cha kawaida                           …………………………        kura 0
9.    Tetanasi( pepopunda)…………………                      kura  0
10. Homa ya manjano………………….                                      kura 0


Kama mtaalam, unaweza kutokubaliana na vipaumbele vyao – unaweza mathalan kutaka kuweka  sepsisi(maambukizi  ya sumu kwenye damu) na baridi-halijoto ya mwili  kuwa  chini sana ya kiwango cha kawaida  kwenye nafasi za juu katika orodha. Inawezekana una taarifa au takwimu za vifo vya  watoto  kutokana na matatizo hayo.

Hata hivyo, dhamira ya mchakato wa  Tushikamane ni kuishirikisha jamii na kuihamasisha  kukabiliana na matatizo ambayo wanaamini ndiyo muhimu zaidi. Kwa njia hii, tunatarajia kutakuwepo na shughuli nyingi zaidi, ushirikiano, shughuli hazitakwama, azma ya kufanikiwa na undelevu wa matokeo ya mradi.

Hivyo, kikundi kimebainisha  matatizo yafuatayo kupewa kipaumbele:
Kwa mama:
·         kupoteza damu nyingi  baada ya kujifungua, na
·         mtoto kushindwa kupita kwenye pango la nyonga;
Kwa watoto wachanga:
·         Matatizo ya kupumua  mara baada ya kuzaliwa; na
·         Malaria.


Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya mkutano wa 4


·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wajawazito walikua wajawazito?
·          Mkutano uliendaje – kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·          Orodha ya matatizo yalioainishwa kupewa kipaumbele ikoje ?


Nini kifanyike baada ya Mkutano wa  4

·         Makatibu wanapaswa kuorodhesha wote waliohudhuria kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wenzao  ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano.





MKUTANO WA  5 – KUBAINISHA MAMBO YANAYOCHANGIA  MATATIZO  HAYO – MIZIZI  YA  MATATIZO

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa  5

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu maarufu  kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  4. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Wakumbushe wanawake kuwa mkutano unaokuja utajaribu kubainisha mambo ambayo yanachangia sana  vifo vya mama na watoto wachanga.

Mkutano unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha wale walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.



Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa 5?

Wanawake wote waliohudhuria mkutano wa  4 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Endelea kuwahimiza  wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria  – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao   wana  ushawishi.



Ajenda ya Mkutano wa  5
1. Makaribisho, utambulisho na mapitio ya mhutasari ya mkutano uliopita.

2. Wasilisha lengo ya mkutano: kubainisha mambo ya msingi yanayosababisha matatizo makuu yaliyotambuliwa  ambayo  yanahusiana na vifo vya mama na watoto wachanga. Ni vigezo gani vinachangia matatizo hayo kuongezeka na /au  kuwa na athari mbaya zaidi?
3.Wezesha kikundi kujadili umuhimu wa kubainisha mambo yanayochangia matatizo yaliyotambuliwa. Kumbuka ni muhimu kubainisha mambo ya msingi  yanayochangia kwa sababu:
·         Inawezekana kuzuia matatizo ya afya kuongezeka kwa kudhibiti mambo hayo  ambayo yanachangia.
·         Baadhi, siyo yote, ya matatizo ya afya yana mambo ambayo yanayachochea, ambayo yanaweza kubainishwa.
·         Tatizo moja la afya linaweza kuwa linachangiwa na mambo kadhaa.

4. Shughuli kuu za mkutano:  Wezesha wanawake ndani ya kikundi kubainisha  mambo ya msingi ambayo yanachangia yale matatizo makuu 4 yanayohusiana na vifo vya mama na /au watoto wachanga yaliyotambuliwa.  Tumia kadi za picha za matatizo na kadi za picha za mambo yayochangia matatizo hayo.
 Angalia MAELEZO yanayofuata namna ya kuendesha mkutano huo.

5. Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?

6. Fanya uchambuzi iwapo malengo ya mkutano yamefanikiwa vya kutosha. Kama hayajafanikiwa, unaweza kurudi nyuma na kurudia vipengele vyote au  baadhi ya vipengele vya  mkutano.

7.Himiza washiriki kuuliza maswali
8. Panga tarehe ya mkutano ujao.



MAELEZO JUU YA NAMNA YA KUKIWEZESHA KIKUNDI KUBAINISHA MAMBO YA MSINGI AMBAYO YANACHANGIA MATATIZO YALIYOTAMBULIWA
1.    Elezea kwamba mambo ya msingi  yanayochangia ni  vile vigezo vya kitabibu au kitiba, kijamii, na kiuchumi ambavyo husababisha matatizo ya afya kutokea.

2.    Chora  kwenye kipande kikubwa cha karatasi picha ya mti ikionesha mizizi, shina na matawi.Shina la mti huwakilisha tatizo. Mizizi huwakilisha matatizo yanayochangia-vile vigezo ambavyo husababisha tatizo kukua. Matawi ya mti huwakilisha madhara na athari zitokanazo na tatizo.





  
3. Weka kadi ya picha ya tatizo kuu lililotambuliwa(mfano malaria) kwenye shina la mti.

4. Wambie wanakikundi kutazama mizizi ya tatizo, (au mambo yanayochangia tatizo hilo), na kuorodhesha mambo ambayo wanafikiri yanachangia tatizo la malaria kuongezeka. 

5. Kadri kila jambo au kigezo ambacho kinachangia kinapobainishwa, weka kadi ya picha ya kigezo hicho kwenye mizizi ya mti. ( Kama hakuna kadi yenye picha hiyo unaweza kuchora jambo hilo  au kuandika kigezo hicho kwenye karatasi na kukiweka kwenye mizizi ya mti.)

Mathalan, kikundi kinaweza kubainisha mambo yanayochangia kuongezeka kwa tatizo la malaria kuwa ni pamoja na:  mbu wengi !; ukosefu wa maarifa  kuzuia malaria; mazalia mengi ya mbu yanayozunguka nyumba zenye maji yaliyotuama; kutolala chini ya kiandarua kila siku; kutotibu vyandarua  mara kwa mara na dawa ya kufukuza mbu; kukosa fedha za kununua dawa unapogundua dalili za ugonjwa huo; kutowahi kwenye kituo cha afya mara baada ya kuhisi dalili za kwanza za ugonjwa huo.

Kama unafikiri  bado hujaifikia mizizi ya tatizo, basi endelea huhoji kwa  kuuliza swali  “kwa nini”. (mathalan  “kwa nini unashindwa kwenda kwenye kituo cha afya?” “Hatuna usafiri”, “kwa nini huna usafiri?” nk.

Jaribu kuhakikisha kuwa unapata mchanganyiko mzuri wa mawazo juu ya mizizi ya tatizo, ambayo inajumuisha, kwa mfano, masuala ya afya; miundombinu; umasikini; mila na desturi; hali ya kijamii; familia; na elimu.

Hakuna majibu yasiyo sahihi na kikundi kinapaswa kuhimizwa kuorodhesha mambo yote ambayo yanachangia, na madhara au athari zake ambazo wanaweza kufikiria.

6. Rudia hatua  3 hadi 5 kwa ajili ya matatizo mengine 3 makuu yaliyotambuliwa.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 5

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto gani ?
·          Mambo gani ambayo yanayochangia matatizo  yameibuliwa kwa   kila tatizo ambalo limetambuliwa ?



Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 5

·         Makatibu wanapaswa kuorodhesha watu wotewaliohudhuria  kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wenzao ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.





AWAMU YA  2: KUPANGA NJIA ZA UFUMBUZI PAMOJA

Shabaha ya Awamu  ya  2 ya mzunguko wa mikutano ya Tushikamane ni kwa ajili ya vikundi vya  Tushikamane kupanga njia za ufumbuzi au utatuzi wa matatizo ambayo husababisha vifo vya mama na watoto wachanga. 

Awamu hii ina mikutano 3 ambayo itafuatana hivi:
·         Mkutano wa  6: Kubainisha shughuli za kuzuia na kusimamia matatizo hayo
·         Mkutano wa  7: Kubainisha njia za ufumbuzi au utatuzi wa matatizo yaliyotambuliwa
·         Mkutano wa  8: Kuwasilisha maendeleo ya mchakato huu  kwa wanajamii


MKUTANO WA  6 – KUBAINISHA SHUGHULI ZA KUZUIA NA KUSIMAMIA MATATIZO HAYO

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa  6

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu maarufu  kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  5. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Wakumbushe wanawake kuwa mkutano unaokuja utajaribu kubainisha shughuli za kuzuia   vifo vya mama na watoto wachanga.

Mkutano unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha wale walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.

Hakikisha kuwa unazo kadi za picha za matatizo makuu yote 4; na kadi za picha za mambo yanayochangia kila tatizo.




Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa 6 ?

Wanawake wote waliohudhuria mkutano wa  5 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Endelea kuwahimiza  wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria  – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao   wana uwezo  wa kuwashawishi wengine.

Ajenda ya  6
1.    Makaribisho, mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita na utambulisho

2.    Kuwasilisha malengo: Kikundi kimechagua matatizo makuu 4 ya kushughulikia – 2 ya akinamama, na  2 ya watoto wachanga. Katika mkutano huu, lengo ni kuibua shughuli ambazo zinaweza:
·         Kuzuia matatizo hayo yasitokee.
·         Kusimamia (kukabiliana) na matatizo hayo iwapo yatajitokeza.


Mifano ya uzuiaji na usimamizi kama tatizo ni  malaria:
Shughuli za uzuiaji
·         Kuongeza uelewa juu ya uzuiaji wa  malaria.
·         Kuondoa mazalia ya mbu yanayozunguka nyumba.
·         Kuwashawishi wafanyakazi wa afya kutoa vyandarua kwenye kliniki za mama wajawazito.
·         Kuwashawishi viongozi na wasimamizi wa idara husika kuhakikisha kuwepo  akiba ya vyandarua vya kutosha na kupunguza rushwa.
·         Kulala chini ya chandarua kila siku.
·         Kutibu vyandarua na dawa ya kuua mbu kila baada ya muda kama itakavyoshauriwa.
·         Wajawazito kujifungulia kwenye kituo cha afya chini ya chandarua.
·         Kuboresha lishe ya mama ili kuimarisha kinga yake dhidi ya magonjwa.


Shughuli za usimamizi   malaria
·         Kutumia vidonge vya malaria, (kama vinapatikana) kama itakavyoelekezwa na mfanyakazi wa afya.
·         Kumwahisha mgonjwa kwenye kituo cha afya cha karibu kama ana dalili  za malaria. kama vile homa, kuhisi baridi kali, maumivu ya kichwa, au maumivu ya viungo.


3.    Kujadili umuhimu wa kuibua  shughuli za uzuiaji na usimamizi wa matatizo hayo:
·         Kama mambo yanayochangia matatizo makuu yaliyotambuliwa  yapo ndani ya jamii husika, basi shughuli za uzuiaji zinaweza kuyasimamisha ili yasiendelee kusababisha matatizo ya afya.
·         Hata kama matatizo haya makuu ya afya yaliyotambuliwa yatajitokeza kwenye jamii, basi shughuli za usimamizi zinaweza kusaidia kuyadhibiti  ili yasilete madhara au athari mbalimbali.
Jaribu kukifanya kikundi kutambua   kuwa mara nyingi  tunaamua kuishi na matatizo bila kujitahidi kukabiliana nayo vizuri mara yanapojitokeza, wala kushughulikia mizizi yake  iliyojichimbia kwenye jamii zetu.

4.   Shughuli kuu za mkutano: Kamata orodha ya matatizo makuu 4 yaliyotambuliwana kikundi.  Wambie wanawake kwenye kikundi kufikiria shughuli mbalimbali za uzuiaji na usimamizi wa matatizo hayo. Angalia MAELEZO chini, na kutumia seti 4 za kadi za picha:
·         ‘Kadi za picha za matatizo’;
·         ‘Kadi za picha za mambo yanayochangia matatizo hayo;
·         ‘Kadi za picha za shughuli za uzuiaji; na
·         ‘Kadi za picha za shughuli za usimamizi wa matatizo hayo’.

5.    Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?

6. Fanya uchambuzi iwapo malengo ya mkutano yamefanikiwa vya kutosha. Kama hayajafanikiwa, unaweza  kurudia vipengele vyote au  baadhi ya vipengele vya  mkutano.
7. Himiza washiriki kuuliza maswali.
8. Panga tarehe ya mkutano ujao.




MAELEZO JUU YA KUBAINISHA SHUGHULI MBALIMBALI KWA AJILI YA  KUZUIA NA KUSIMAMIA MATATIZO MAKUU  YANAPOJITOKEZA

1.    Eleza kwamba shughuli za uzuiaji ni zile shughuli ambazo zinaweza kuzuia mambo yanayochangia matatizo ya afya kutokea na hivyo kusimamisha au kuzuia matatizo hayo ya afya yasiibuke.   

2.    Eleza kwamba shughuli za usimamizi ni zile shughuli ambazo zinaweza kuzuia matatizo ya afya yasisababishe madhara au athari.

3.    Weka chini kadi ya picha ya tatizo kuu la afya lililotambuliwa. 

4.    Katika mkutano wa  5, kikundi kilibainisha mambo ambayo yanachangia tatizo hili kuibuka. Kama mlivyofanya kwenye mkutano wa kwanza, chora chini picha ya mti, na kuweka tatizo katikati ya mti. Halafu weka kadi za picha ya mambo yanayochangia kwenye mizizi.


5.    Himiza wanakikundi kuweka shabaha kwenye shughuli za uzuiaji ambazo husaidia kuzuia mambo yanayochangia yasiibuke. Tumia kadi za picha za uzuiaji, (au tengeneza za kwako kama kikundi hakitapata mbadala).

Usisahau  zile shughuli za uzuiaji kama vile mabadiliko ya mila na desturi hatarishi ili watu waweze kutafuta msaada wa kiafya mapema; au kuwaweka wanajamii pamoja kushinikiza maboresho huduma za afya; au kufanya mambo ambayo husaidia kuhakikisha kuwa mabadiliko yaliyoahidiwa yatapatikana.  

Kusanya pamoja kadi zote za picha ambazo wanawake wamechagua kuwa zinaelekeza jinsi ya kutatua mizizi ya matatizo ili kuyazuia kutokea.

6.    Halafu badilisha shabaha ya kikundi ielekee kwenye shughuli za usimamizi wa matatizo yaliyobainishwa. Himiza kikundi kulenga  shughuli ambazo husaidia kusimamisha tatizo lililobainishwa kutosabisha vifo au uharibifu mwingine. Tumia kadi za picha za shughuli za usimamizi (au tengeneza za kwako kama kikundi hakiwezi kutoa mbadala wa kadi  ya picha ambayo umekosa).

Majibu yote ni sahihi ! Usifadhaike iwapo utaona mjadala unapanuka sana na kutoka kwenye shabaha. Lakini kumbuka kuwarudisha  kwenye kipengele husika- kuchagua kadi za picha  ambazo zinawakilisha njia mbalimbali za kutatua tatizo husika,au  angalau zitalizuia tatizo kutosababisha vifo.

Kusanya pamoja kadi zote zenye picha ambazo wanawake wamechagua kuwa zinaonesha jinsi ya kusimamia tatizo ili kuzuia lisisababishe vifo.

Rudia hatua  1 hadi  6 kwa yale matataizo mengine makuu 3. Mwisho wa  mchakato huu, utakuwa na seti ya kadi za picha za uzuiaji, na seti za kadi za picha za usimamizi,ambazo zinaelezea njia zote zinazoweza kuchukuliwa na kikundi kusimamisha vifo kutokea.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 6

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·         Ni shughuli gani za uzuiaji na usimamizi ziliibuliwa kwa ajili ya   kila tatizo ambalo limepewa kipaumbele ?


Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 6

·         Makatibu wanapaswa kuorodhesha wahudhuriaji wote kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.




MKUTANO WA  7 – KUANDAA MIPANGO

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa  7

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu maarufu kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  5. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Wakumbushe wanawake kuwa mkutano unaokuja utajaribu kutafakari mipango inayostahili na kubainisha njia za ufumbuzi. Hii itakuwa  fursa maalum kwa wanawake kutoa maoni yao na mawazo yao kusikika.

Mkutano utakapokaribia, wakumbushe wanakitongoji  tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha wale walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.

Kusanya pamoja kadi zote za picha kutokana na mkutano uliopita:


·         Kadi za picha za matatizo yote 4
·         Kadi za picha zenye mizizi ya kila tatizo- mambo yanayochangia tatizo hilo;
·         Kadi za picha walizochagua  wanawake ambazo zinaonesha  shughuli za kuzuia tatizo husika; na
·         Kadi za picha  walizochagua  wanawake ambazo zinaonesha shughuli zitakazofanyika  kuzuia vifo, iwapo tatizo husika litajitokeza.

Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa 7 ?

Wanawake wote waliohudhuria mkutano wa  6 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Endelea kuwahimiza  wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria  – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao  huwa wana uwezo  wa kuwashawishi .


Ajenda kwa ajili ya  Mkutano wa  7
1.    Makaribisho, mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita na utambulisho
2.    Kuwasilisha lengo la mkutano: mkutano huu unalenga kuweka pamoja mawazo kutokana na mikutano kadhaa ambayo imefanyika, na kuyageuza kuwa mipango na ufumbuzi wa kukabiliana na matatizo makuu 4 yaliyotambuliwa, au vizuri zaidi,  kuweza kupambana na mizizi ya matatizo hayo. Baada ya hapo, unaweza kuendelea kujadili jinsi gani njia hizi za ufumbuzi zinaweza kufanikishwa. 

Siku ya mkutano huo  ni siku ya kugeuza mijadala iliyofanyika huko nyuma kuwa mapendekezo kamili kwa kitongoji kizima.

 3. Shughuli kuu za mkutano: Chagua tatizo kuu mojawapo – vizuri zaidi lile ambalo kila mtu anataka ndiyo litatuliwe haraka. Katika mikutano 3 iliopita, wanawake watakua walikwisha  kutafakari mizizi ya tatizo, na kuibua mawazo mbalimbali  namna  ya kukabiliana na  tatizo hilo ili lisisababishe vifo, na pia namna ya kushughulikia  mizizi yake.
Tandaza chini kadi ya picha ya tatizo; kadi za picha ya mambo  yanayochangia; kadi za picha za shughuli za uzuiaji; na kadi za picha za shughuli za usimamizi wa tatizo. Unaweza kutaka kuendelea na zana  ya mti na mizizi yake, na kuuweka mti kama tatizo, mambo yanayochangia kama  mizizi, na kuweka  kadi za picha za shughuli za uzuiaji na usimamizi wa tatizo kuzunguka mti- zikiwa ndiyo shughuli zitakazofanyika kukabiliana na tatizo hilo.

Sasa unaweza kuyageuza haya yote kuwa mipango ya awali. Mipango halisi itakamilishwa wakati kikundi kitakapopanuliwa na kujumuisha wanaume na wale wote ambao watahitaji kujiunga na kikundi. Lakini mkutano huu unahusu  kuwawezesha wanawake kutoa mawazo yao kwanza.

Waulize wanawake mambo gani  hasa wangependa wayaone yakitekelezwa, kwani sasa wamekwisha kutafakari kwa kina juu ya  tatizo. Katika hatua hii, usijisumbue sana na  masuala ya fedha na vipengele vyote vidogo vidogo  ndani ya  mipango hii. Tunachotaka ni orodha ya mambo ambayo wanawake hasa wangependa kuona yakifanyika, na baada ya hapo tunaweza kuangalia  uwezekano wa kutekeleza na  kufanikisha njia mbalimbali za ufumbuzi  ambazo zimechaguliwa.

Kama matatizo yote 4 ambayo yamechaguliwa ni, mfano: kwa akinamama, kupoteza damu nyingi baada ya kujifungua na mtoto kushindwa kupita kwenye pango la nyonga; kwa watoto wachanga, maambukizi (yakiwemo  malaria), na kuhara. Kikundi kitakuwa kinafikiria siyo tu wafanye nini  wakati tayari mama au mtoto ana tatizo hilo, lakini pia jinsi ya kuzuia tatizo hilo kutokea.

Unataka kutumia  yote hayo kutengeneza orodha ya njia za ufumbuzi wa tatizo ambazo zinawezekana. Wanaweza kuibua orodha kama ifuatayo:

·         Mafunzo kwa  wakunga wa jadi ili waweze kukabiliana na matatizo,   kuzuia yasitokee, na  kuwafikisha wajawazito  haraka hospitalini kupata msaada zaidi.
·         Shughuli mbalimbali za uzalishaji pato ili kupunguza umasikini na utapimalo.
·         Kuboresha huduma ya maji safi na salama kupitia juhudi za jamii yenyewe.
·         Kuanzisha bustani za kikundi za mbogamboga  ambazo zitatoa  chakula cha ziada  kwa wajawazito wenye mahitaji.
·         Kuanzisha kampeni ndani ya kitongoji kwa ajili ya kusafisha mazalia ya mbu. Kuazisha juhudi za kuwapatia  akinamama wote na watoto vyandarua.
·         Kuanzisha juhudi za kutibu vyandarua vyote na dawa ya kuua au kufukuza mbu  kadri  itakavyoelekezwa na wataalam.
·         Kuhakikisha wajawazito wanahudhuria kliniki, hasa kuanzia mwezi 6 – 7, wakati afya zao zinatakiwa kupimwa, (mathalan kwa ajili ya  anemia), na hatari ya kupata matatizo wakati wa kujifungua inaweza kujadiliwa. Mathalan msichana  wa miaka 15 mwenye umbo dogo yuko katika hatari zaidi  ya kushindwa kumpitisha mtoto kwenye pango la nyonga kuliko yule ambaye tayari amezaa watoto kadhaa.
·         Kutafuta baisikeli au pikipiki maalum ya wagonjwa  kwa ajili ya kuwawahisha wanawake na watoto wachanga kwenye kituo cha afya kilichoko karibu.
·         Programu ya elimu ya afya kwa akinamama juu ya kulinda  watoto wachanga wasipatwe na maambukizi makali, na namna ya kuwahudumia ili wasipoteze maisha kama watapata maambukizi.
·         Kuanzisha mfuko wa kikundi wa dharura kwa ajili ya usafiri.
·         Kuanzisha utaratibu  wa kuwaita wanaume kutoa msaada kwa ajili ya kuwapeleka wanawake kwenye kituo cha afya au hospitalini wakati wa dharura.

Katika hatua hii ya mchakato wa Tushikamane,huhitaji kutafuta vipaumbele- kuchagua hili au lile. Hii itakuja baada ya mikutano kadhaa inayofuata.
4.Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?
5. Pima kama umepata orodha nzuri ya mipango na njia za ufumbuzi za kuanzia. Kama hili halijafikiwa, unaweza kurudi nyuma na kurudia baadhi ya  vipengele   vya mkutano au vipengele vyote.

6. Himiza washiriki kuuliza maswali
7. Panga tarehe ya mkutano ujao.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 7

·         Rejesta ya mahudhurioinapaswakukamilishwa kwa muhtasari:wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wajawazito walikuwa wangapi ?
·          Mkutano uliendaje – je, kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·         Ulitoka na orodha gani ya mwisho ya mipango na njia za ufumbuzi?

Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 7

·         Makatibu wanapaswa kuwaorodhesha washiriki  wote kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·         Jaribu kujenga hamasa ndani ya kitongoji kizima juu ya mkutano ujao, ambao unatarajiwa  kupeleka mchakato mbele kwenye hatua nyingine.








MKUTANO WA  8 – KUWASILISHA MAENDELEO YA  MCHAKATO KWA JAMII

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 8

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Hasa, wewe na kikundi, kwa msaada wa Alex, Wilbard na Mchungaji Isaac, mnatakiwa kufanya mazoezi  ya kazi  itakayowasilishwa kwenye mkutano.


Tembelea watu maarufu  kwenye  kitongoji  waliohudhuria mkutano wa  5. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Wakumbushe wanawake kuwa mkutano unaokuja utajaribu kutafakari mipango na kubainisha njia za ufumbuzi, na hiyo itakuwa  fursa ya pekee kwa wanawake kutoa maoni yao na mawazo yao kusikika.

Mkutano unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu wote maarufu kwenye kitongoji  kuhudhuria.




Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa  8?
Mkutano wa 8 ni mkutano mahali ambapo  ripoti juu ya maendeleo ya mchakato wa Tushikamane itawasilishwa kwa jamii. Kuanzia hatua hii, itakuwa bora kupanua uanachama kujumuisha wale wote ambao wanaweza kuchangia, kwa namna moja au nyingine, kupunguza vifo vya akinamama wakati wa kujifungua, na  vifo vya watoto wachanga.

Uanachama katika kikundi utahitaji kuzingatia mila na desturi, lakini vikundi vinaweza kujumuisha wafanyakazi wa afya  vijijini au wafanyakazi  wengine wa afya; viongozi wa jamii; walimu; wenzi wa wanawake na wasichana balehe walioko kwenye kikundi; wafanyakazi wa ugani au wa mashirika ya misaada ambao wanashughulikia matatizo haya; na yeyote ambaye anaguswa na afya ya wanawake na watoto wao kwa ujumla.


Endelea kuwashawishi wanawake wote waliohudhuria mkutano wa  7  kuhudhuria kama wanaweza. Endelea pia kuwahimiza  wanawake wengine katika umri wa uzazi  kuhudhuria  – hususan wale wenye sauti  wanaosikilizwa sana kwenye kitongoji, na  wana  ushawishi.

Kupanga uwasilishaji wa ripoti kwa jamii katika  mkutano wa  8
Unahitaji kufanya mkutano rasmi na Msimamizi wako Alex, na Kiongozi wa Mradi, Wilbard Mrase, kupanga jinsi gani Kikundi cha Tushikamane kutakaivyowasilisha ripoti ya maendeleo kwa wanakitongoji. Mnaweza kuamua pamoja kuwa na mkutano mwingine kutoa mawazo yenu kwa Mwenyekiti wa Mradi, Mchungaji  Isaac Mgego, ili kupitia  mipango yenu  na kuiboresha  zaidi.

Wewe  Alex na  Wilbard, kwa ushauriano na Kikundi cha  Tushikamane, mnahitaji kutoka na mwafaka  jinsi gani mkutano utakavyoendeshwa. Mnahitaji kuamua mtasema nini juu ya mambo yafuatayo, na jinsi ya kuyasema. Mnaweza kuamua kugawana majukumu – kwa mfano Kiongozi wa Mradi kutoa utambulisho  na malengo ya mkutano; Msimamizi kueleza jinsi programu inavyofanya kazi; na wewe kueleza mafanikio gani yamepatikana.

Ili kufanya shughuli kuwa changamfu  na kuvuta umakini na matumaini ya watu wengi, unaweza  kuingiza kwenye ripoti yako ya maendeleo, baadhi ya michango ya wanawake kutoka kikundi hicho – mathalan   igizo dhima dogo au  mziki au wimbo.

Usisahau kutumia kadi za picha kukusaidia kuwasilisha ujumbe.

Baada ya kufanya mkutano na Kiongozi wa Mradi, Msimamizi, na ikiwezekana Mwenyekiti, unapaswa kuwa na picha kamili jinsi kila kipengele cha mkutano kitakavyoshughulikiwa:
·         Ajenda na malengo ya mkutano – mathalan kuwasilishwa na Kiongozi wa Mradi  Wilbard Mrase.
·         Taarifa za msingi juu  ya programu ya  Tushikamane  na jinsi inavyofanya kazi – mathalan kuwasilishwa na Alex Gongwe.
·         Taarifa ya maendeleo ya Kikundi  kuwasilishwa na wewe, pamoja na wanawake kutoka Tushikamane watakaoteuliwa. Pamoja, mnaweza kueleza kwa nini na namna gani mmechagua matatizo hayo makuu 4; kueleza mizizi yake; kueleza mambo ambayo yanaweza kuwa yanachangia matatizo hayo au mizizi yake; na kutoka na orodha ya mipango na njia za ufumbuzi.
·         Zoezi la maswali, maoni na mawazo kutoka kwa washiriki  linaweza kuongozwa na  Alex au  Wilbard.


Kuandaa  mwaliko kwa jamii kuhudhuria  Mkutano wa  8
Katika mkutano wako wa kuandaa mpango wa mwaliko na  Alex na Wilbard, unahitaji pia kuamua nani wataalikwa na kwa njia gani. Watu ambao mnaweza kualika wameorodheshwa juu.

Wataalikwaje ? Kwa mfano, kwenda nyumba  mmoja hadi nyingine; kupitia matangazo kanisani; kwa njia ya barua; kuwaomba wanawake kwenye kikundi kuja na  watu nk.

Kuendesha wa Mkutano 8 – kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya kikundi cha  Tushikamane  

1.    Makaribisho na utambulisho.

2.    Kuwasilisha malengo ya mkutano:Kutoa mrejesho juu ya mijadala, yakiwemo matatizo makuu yaliyobainishwa na njia za ufumbuzi, kwa wanajamii wote ili kupata maoni yao; mawazo yao; na  kupata misaada ya hali na mali kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli  za ufumbuzi.

3.    Mambo  ya  msingi juu ya Mradi wa  Tushikamane na jinsi unavyofanya kazi.

4.    Shughuli kuu za mkutano: Kutumia njia zilizopangwa mapema, kuwasilisha kwa jamii taarifa ya maendeleo ya kikundi hadi sasa. Shirikisha wanawake kutoka kwenye kikundi kukusaidia katika zoezi hili.Tumia njia zingine shirikishi –mathalan nyimbo, kucheza ngoma, kuigiza, kadi za picha nk.

Malizia kwa kuwasilisha kwa washiriki orodha ya mipango na njia za ufumbuzi ambazo wanawake walipendekeza. Hadi hatua hii, kitongoji kizima kinapaswa kuwa na uelewa kwamba ili kukabiliana na vifo vya akinamama na watoto wachanga, wanapaswa kukabiliana na mizizi ya matatizo yanayosababisha vifo hivyo.

5.    Fungua mjadala kwa wanajamii kubadilishana mawazo. Majadiliano yanaweza kuchukua mkondo wowote ule lakini katikati warudishe washiriki kwenye msitari ili wakubaliane kwa pamoja kuchagua wafanye nini, na namna gani.

6.    Fanya majumlisho ya mkutano, na tafuta mwafaka  kutoka kwa washiriki kuwa ndivyo mkutano ulivyokuwa. Nani atafanya nini kabla ya mkutano unaofuata?

7.    Panga tarehe ya mkutano ujao.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 8

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·         Taarifa gani, maswali na mawazo gani yaliibuliwa na wanajamii ?


Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 8

·         Makatibu wanapaswa kuorodhesha wote waliohudhuria kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·         Jaribu kupata maoni ya viongozi na watu wengine ambayo yanaweza kusaidia kupima umuhimu wa juhudi inayoendelea kwenye kitongoji, na kushiriki   angalau   katika mkutano 1 au 2, ili waweze kuona kama wangependa kushiriki katika programu ya Tushikamane.







AWAMU YA  3: KUTEKELEZA NJIA ZA UFUMBUZI PAMOJA



Shabaha ya Awamu ya  3 ya mzunguko wa mikutano ni kwa vikundi vya  Tushikamane kutekeleza njia za ufumbuzi zilizobainishwa katika kukabiliana na matatizo ambayo yanasababisha vifo vya mama na watoto wao wachanga.

Awamu ya 3 ina mikutano 3:
·         Mkutano wa  9: Kupanga ufumbuzi: ambapo jamii itaunda kamati mbalimbali  – kamati 1 kwa ajili ya kila njia ya ufumbuzi ambayo wanapanga kutekeleza.
·         Mkutano wa  10: Kukusanya rasilimali: kila kamati kufanya kazi na mbia au asasi ambayo Tushikamane itasaidia kutafuta, kukusanya rasilimali ambazo watahitaji kutekeleza ufumbuzi uliopangwa.
·         Mkutano wa  11: Kubuni zana za ufuatiliaji: ili tuweze kujua iwapo njia za ufumbuzi ambazo  zinatekelezwa zinazaa matunda.

Baada ya hapo, kutakuwa na muda  kabla ya Awamu ya  4 – mikutano 3 ya mwisho – ili njia za ufumbuzi ziweze kutekelezwa, na  shughuli zilizopangwa kufuatiliwa vizuri. Muda  huu unaweza kuwa takriban kati ya miezi 3 na  6.


MKUTANO WA 9 – KUPANGA NJIA ZA UFUMBUZI

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 9

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Hasa, wewe na kikundi, kwa msaada wa Alex, Wilbard na Mchungaji Isaac, mnatakiwa kufanya mazoezi  ya kazi  itakayowasilishwa kwenye mkutano.


Tembelea watu muhimu kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  8. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kutekeleza mipango ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.

Eleza bayana kwamba programu ya Tushikamane haitagharamia  ufumbuzi, lakini itasaidia kuunganisha kitongoji na wadau au asasi zingine ambazo zinaweza kuwaunga mkono kufanikisha njia za ufumbuzi walizopanga. Ni rahisi zaidi kupata msaada-kwa mfano kutoka idara za serikali au mashirika ya misaada-pale ambapo kuna mipango ambayo imetokana mchakato makini shirikishi,  ambao umewashirikisha kwa ukamilifu wanawake walio katika umri wa uzazi.

Mkutano unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu wote maarufu  kwenye kitongoji  kushiriki.

Watu wanaostahili kwenye jamii sasa wanaweza kujiunga na kikundi cha  Tushikamane. Hivyo,  kutakuwa fursa nzuri zaidi za kutafuta msaada na kuunganisha nguvu na juhudi za jamii. Hii italeta mabadiliko makubwa katika juhudi za kuzuia vifo.

Wakumbushe watu maarufu katika kitongoji kwamba mkutano ujao utajaribu kubainisha njia za ufumbuzi ambazo zinatarajiwa  kuendelezwa, na mkutano huo utakuwa  wakati maalum kwa mawazo yao kusikika, yakiongzea   yale ambayo  wanawake watakuwa tayari wamejadili.

Mkutano utapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu wote maarufu  kwenye kitongoji  kushiriki.

Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa 9 ?

Wanawake wote waliohudhuria Awamu ya 1 na 2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza.
Pia, kikundi kitakuwa kimebaini watu maarufu kupitia mikutano iliyopita, ambao ushiriki wao utasaidia kikundi kufanya kazi vizuri na kuongeza uwezekano wa kufanikiwa.
Watu kama hao ni pamoja na Wenyeviti wa Vijiji, Wafanyakazi wa Afya Vijijini, wafanyakazi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, nk.

Endelea kuwahimiza  wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria  – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao  huwa wana uwezo  wa kuwashawishi wengine.


Ajenda ya Mkutano wa  9
1.    Makaribisho, utambulisho, na taarifa fupi ya mchakato wa Tushikamane hadi ulipofikia sasa, na wapi unaelekea.

2.    Hasa wakaribishe wanakikundi wapya, hususan wanaume. Sisitiza kwamba wana wajibu muhimu ambao wanapaswa kutimiza. Wana wajibu wa kutoa ushauri na msaada pale unapohitajika, ili kufanikisha lengo la kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.  Lakini kutokana na jinsi kikundi kinavyofanya kazi, wanatarajiwa kusikiliza na kuheshimu mawazo na maoni ya wanawake.

3.    Wasilisha malengo ya mkutano:
·         Baada ya mkutano, kutoka na orodha ya njia za ufumbuzi zilizopendekezwa ambazo jamii itakuwa ikitekeleza.
·         Kuunda  kamati ya kufanikisha  kila ufumbuzi uliopendekezwa.
·         Halafu kila kamati  kukubaliana juu ya mpango kazi wake kwa ajili ya utekelezaji wa ufumbuzi waliopewa.

Eleza kwa nini mchakato huu makini wa kupanga  husaidia siyo tu kuchagua matatizo sahihi ya kukabiliana nayo, na njia sahihi za kukabiliana nayo, lakini pia huwaleta  watu wote kufanya kazi pamoja, kigezo ambacho huchangia uwezekano mkubwa wa kufanikiwa.

4. Shughuli kuu za mkutano: Angalia kwenye orodha ya njia za ufumbuzi ambayo imewasilishwa kwa jamii kwenye mkutano wa  8. Sasa unahitaji kupunguza orodha hii hadi shughuli 3 au 4  ambazo kikundi kitakabiliana nazo.

Andika shughuli zilizochaguliwa (mfano shughuli 4) kwenye vipande vya karatasi, na kuweka shughuli moja kwenye kila kona ya chumba, au kama ni mduara  weka nje ya mduara vipande 4 vya karatasi vyenye majina ya shughuli hizo 4, kuzunguka mdwara ukiacha  nafasi sawa katikati.

Wambie wanakikundi kuinuka na kuelekea kwenye shughuli iliopangwa ambayo wangependa kushiriki. (Kama wanataka kushiriki katika zaidi ya shughuli moja, basi wawezeshe katika hatua hii kuchagua moja ambayo wanahisi ndiyo muhimu zaidi.)

Mchakato huu unapaswa kuishia  katika kukigawa kikundi katika vikundi vidogo 3 au 4. Kila kikundi kidogo kinakuwa kamati ya kusaidia utekelezaji wa shughuli iliopangwa ambayo wamechagua kushiriki.Kamati zote zinapaswa kufanya kazi pamoja kwa takriban saa 1, na kutoka na mpango kazi kwa ajili ya shughuli yao iliyopangwa kusaidia kutatua tatizo au matatizo yaliyobainishwa.

Mwisho   wa mchakato huu, kikundi kizima kitaungana tena, na kila kamati kutoa mrejesho kwa kikundi kikubwa inayojumuisha mambo yafuatayo:

·         Jina la shughuli iliopangwa ambayo wamechagua kushiriki ili kusaidia kuzuia vifo vya mama na watoto wadogo.
·         Jina la mwenyekiti wa kamati, ambaye atatunza kumbukumbu za kila kinachoendelea na kutoa taarifa katika mkutano ujao.
·         Hatua zinofuata  – watafanya nini; na ifikapo lini?
·         Nani hasa atafanya nini ?


7. Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?
8. Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa vya kutosha. Kama hapana, unaweza kurudi nyuma na kurudia  baadhi au vipengele vyote  vya mkutano.

9. Himiza washiriki kuuliza maswali
10. Panga tarehe ya mkutano ujao.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 9

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wajawazito walikua wangapi ?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·         Kwa kila njia ya ufumbuzi iliyobainishwa, wamekubaliana nini juu ya kamati, kanuni na mpango kazi ?



Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 9

·         Makatibu wanapaswa kuorodhesha waliohudhuria wote kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·         Jaribu kupata maoni ya viongozi na watu wengine ambayo yanaweza kusaidia kupima umuhimu wa juhudi inayoendelea kwenye kitongoji, na kushiriki   angalau   katika mkutano 1 au 2, ili waweze kuona kama wangependa kushiriki katika programu ya Tushikamane.
·         Tembelea kila mwenyekiti wa kamati, pamoja na watu wengine maarufu ambao ungependa washiriki. Washawishi kuchukua hatua, na kuwauliza wangehitaji msaada gani ili waweze kufanikisha  shughuli zao.
·         Jadiliana mambo haya na msimamizi wako, na kuyaleta kwenye mkutano wa kila mwezi na Kiongozi wa Mradi na Mwenyekiti wa Mradi. Katika hatua hii ya mchakato wa  Tushikamane, huu ndiyo wakati wa  kuanza kuvisaidia vikundi kuwasiliana na wadau  wengine ambao wanaweza kutoa misaada ya hali na mali kufanikisha shughuli za kikundi.

Ili kuweza kuwaunganisha na wadau husika, watahitaji picha halisi ya kinachoendelea, na nini hasa kila kamati inatafuta.









MKUTANO WA 10 – KUKUSANYA RASILIMALI

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 10

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Hasa, wewe na kikundi, kwa msaada wa Alex, Wilbard na Mchungaji Isaac, mnatakiwa kuifanya mazoezi   kazi  itakayowasilishwa kwenye mkutano.


Tembelea watu muhimu kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  9. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kupanga kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga. Hii hatimaye itavutia misaada ya hali na mali kutoka nje ya kitongoji ambayo itaunganishwa na juhudi za jamii, na kuleta msukumo mkubwa katika kuzuia vifo hivyo vya kusikitisha.

Wakumbushe watu maarufu kwenye kitongoji  kwamba mkutano unaokuja utajaribu kubainisha rasilimali zinazohitajika na wapi pa kuzipata, na wao wenyewe wanaweza kuwa na chochote cha kuchangia.

Mkutano unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu wote maarufu  kwenye kitongoji  kuwepo.



 Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa 10 ?

Wanawake wote waliohudhuria Awamu ya 1 na 2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza, na  wengine wapya waliohudhuria mkutano wa 9.
Pia, kikundi kitakuwa kimetambua  watu maarufu kupitia mikutano iliyopita ambao ushiriki wao utasaidia kikundi kufanya kazi vizuri na kuongeza uwezekano wa kufanikiwa.
Watu kama hao ni pamoja na wenyeviti wa vijiji, wafanyakazi wa afya vijijini, wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, nk.

Endelea kuwahimiza  wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria  – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao  huwa wana uwezo  wa kuwashawishi wengine.



Ajenda ya Mkutano wa  10
1.    Makaribisho, mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita na utambulisho.

2.    Kuwasilisha lengo la mkutano: kupanga jinsi ya kukusanya rasimali ambazo zinahitajika kwa ajili ya utekelezaji wa ufumbuzi kwa matatizo yaliyobainishwa.

3.   Shughuli kuu za mkutano: kupanga jinsi ya kukusanya rasilimali kwa ajili ya kufanikisha ufumbuzi. Ingawa kikundi sasa kina, kwa mfano kamati 4, kila moja ikijaribu kutekeleza ufumbuzi wake uliopangwa, bado ni bora kufanya zoezi la leo la kupanga kwa pamoja. Sababu ni kwamba inawezekana  wanakikundi wengine ndani ya  Tushikamane wamepata mawazo zaidi ambayo yanaweza kusaidia. Pia, kuna uwezekano kwamba  baadhi ya kamati    zinaweza kuwa zinashughulikia tatizo lenye mahitaji yanayofanana – mfano kuhusiana na usafiri au miundombinu.

Kila mwenyekiti wa kamati atawasilisha kwa kikundi kizima ufumbuzi au shughuli ambayo kikundi chake kidogo kinapanga.  Atawasilisha taarifa ya kazi iliyofanyika hadi sasa.

Kikundi kizima cha Tushikamane baada ya hapo kitajadili rasilimali ambazo zinaweza kuhitajika ili ufumbuzi huo uweze kutekelezwa vizuri. Baada ya mjadala wa dakika 10 au 15, watakuwa na orodha ya rasilimali ambazo watahitaji.

Kwa ajili ya kila rasilimali, watahitaji sasa kufikiria vyanzo vyake  – watazipata kutoka wapi au  kwa nani ?

Mfano
Mathalan, ufumbuzi unaweza kuwa mafunzo kwa wakunga wa jadi.
Rasilimali ambazo watahitaji ni:
·         mtu wa kutoa mafunzo kwa wakunga wa jadi;
·         kiongozi cha mafunzo kutoka kwa watu wenye uzoefu katika kufundisha wakunga wa jadi;
·         sehemu ya kufanyia mafunzo hayo;
·         pengine zana au vitendea kazi ambavyo  wakunga wa jadi watahitaji baada ya mafunzo hayo kama vile mashine ya kupima presha;
·         nyenzo au utaratibu wa kuwasafirisha akinamama   kwenda hospitalini pale itakapohitajika.


Baada ya hapo wataanza  kufikiria  vyanzo vya mahitaji hayo:

           Mtu wa kutoa  mafunzo kwa waganga wa jadi – watamuomba nani?

Je kuna mtu yeyote ambaye atawasaidia kutatua suala hili? Hii ndiyo aina ya rasilimali ambayo wewe, kama Mwezeshaji wa  Tushikamane, unaweza kuwasaidia.

Je vipi kuhusu vifaa vya mafunzo? Hapa tena  unaweza kusaidia.

Sehemu ya kufanyia mafunzo: watahitaji kufikiria nani wa kumuomba kuwasaidia kupata sehemu inayofaa. Nani ataongea naye?

Huenda kuna juhudi au huduma  za serikali   ambazo zinaweza kuwasaidia. Nani  atafuatilia?

Kwa vitu ambavyo hugharimu fedha, usikurupuke  kutoa ahadi ya kusaidia kuwatafutia shirika la misaada. Lakini kwa vyovyote vile, wasaidie  kuliandikia shirika la misaada ambalo linaweza kuwa linafanya kazi katika eneo hilo au wilaya hiyo, kuelezea yale yote ambayo tayari wamefanya hadi kufikia hatua hii ya kuhitaji fedha za kusaidia kuzuia vifo vya mama na watoto wachanga.

Mashirika mengi ya misaada yanaweza kuitikia vizuri maombi ya jamii ambazo zimeonesha azma na ushirikishaji wa kiwango hiki, na ambazo zimesikiliza sauti za wanawake. Nani ataongoza juhudi hii?

Mwisho wa mchakato huu, kamati itakuwa na orodha ya rasilimali zilizopendekezwa ambazo wanaweza kuhitaji kufanikisha mipango yao. Watakuwa na wazo pia kuhusu mahali wanaweza kwenda kutafuta rasilimali hizi, na pia  wazo juu ya nani atafanya nini kabla ya mkutano ujao.

4.   Rudia mchakato huu kwa kila kamati. Kila kamati  itawasilisha ufumbuzi wao au shughuli yao iliyopangwa, na kikundi kizima baada ya hapo kitachangia katika utambuzi wa  rasilimali zinazohitajika, na wapi rasilimali hizo zinaweza kupatikana.

     5. Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi.     Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?
     6. Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa vya kutosha. Kama hapana, unaweza kurudi nyuma na kurudia  baadhi au vipengele vyote  vya mkutano.
     7.Himiza washiriki kuuliza maswali.
     8. Panga tarehe ya mkutano ujao.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 10

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wajawazito  walikua wangapi ?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·         Kwa kila njia ya ufumbuzi iliyobainishwa, wamekubaliana nini juu ya kamati, kanuni na mpango kazi ?
·         Kila kamati itachukua hatua gani zinazofuata kutafuta mahitaji ya kufanikisha mipango yao? Unahitaji kuwa na kumbukumbu ya mambo waliyokubaliana, ili uweze kuwakumbusha walichokisema…na kusaidia kukifanikisha.

Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 10

·         Makatibu wanapaswa kuorodhesha wahudhuriaji wote kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·         Jaribu kupata maoni ya viongozi na watu wengine ambayo yanaweza kusaidia kupima umuhimu wa juhudi inayoendelea kwenye kitongoji, na kushiriki   angalau   katika mkutano 1 au 2, ili waweze kuona kama wangependa kushiriki katika programu ya Tushikamane.
·         Tembelea kila mwenyekiti wa kamati, pamoja na watu wengine maarufu ambao ungependa washiriki. Washawishi kuchukua hatua, na kuwauliza wangehitaji msaada gani ili   shughuli hizo ziweze kufanikiwa.
·         Jadili mambo haya na msimamizi wako, na kuyaleta kwenye mkutano wa kila mwezi na Kiongozi wa Mradi na Mwenyekiti wa Mradi. Katika hatua hii ya mchakato wa  Tushikamane, wanahitaji kuanza kuvisaidia vikundi kuwasiliana na wadau  wengine ambao wanaweza kutoa misaada ya hali na mali kufanikisha shughuli za kikundi.

Ili kuweza kusaidia, wadau watahitaji picha halisi ya kinachoendelea, na nini hasa kila kamati inatafuta.





MKUTANO WA  11 – KUTENGENEZA MIFUMO YA UFUATILIAJI


Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 11

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu muhimu kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  10. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha  programu inapoelekea: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika maandalizi ya  mipango ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga. Hii itasaidia kuvutia misaada ya hali na mali kutoka nje ya kitongoji ambayo itaunganishwa na juhudi za jamii, na kuleta msukumo mkubwa katika kuzuia vifo hivyo vya kusikitisha.

Wakumbushe watu maarufu kwenye kitongoji  kwamba mkutano ujao utajaribu kubuni njia za kusaidia kujua iwapo mchakato wa Tushikamane unafanya kazi, na wao wenyewe wanaweza kuwa na chochote cha kuchangia.

Waeleze bayana kwamba hili siyo jambo ambalo kitongoji kinataka kwa ajili tu ya kujipatia ari zaidi. Lakini zaidi ya ari, wadau wengine nje ya mchakato ambao wangependa kusaidia watataka kujua kama kweli mchakato huu unasaidia. Mashirika ya misaada kama vile Mission Morogoro, AMREF, na asasi nyingine zenye uwezo zinaweza  kusaidia  mchakato au programu  kama watajua  upo utaratibu  wa kufuatilia na kupima mafanikio yake.

Mkutano utapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu maarufu wote kwenye kitongoji  kuwepo.

Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa 11 ?

Wanawake wote waliohudhuria Awamu ya 1 na 2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza, na  wengine wapya waliohudhuria mkutano wa 10. Pia, kikundi kitakuwa kimebaini watu maarufu kupitia mikutano iliyopita ambao ushiriki wao utasaidia kikundi kufanya kazi vizuri na kuongeza uwezekano wa kufanikiwa.

Fikiria watu wengine mmoja mmoja  ambao ni muhimu kuhudhuria-kwa mfano mtu yeyote mwenye uzoefu katika ufuatiliaji. Watu kama hao ni pamoja na  wafanyakazi wa afya vijijini, lakini pia baadhi ya wenyeviti wa vijiji, waalimu, nk.



Ajenda ya Mkutano wa 11
1.    Makaribisho, mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita na utambulisho

2.    Kuwasilisha lengo la mkutano: kupanga jinsi ya kufuatilia utekelezaji wa njia za ufumbuzi.

Jadili  kwa nini ni muhimu kufuatilia utekelezaji  wa njia za ufumbuzi: kusherekhea mafanikio na kubainisha changamoto zozote, ili muweze kupanga jinsi ya kuzishughulikia.

3.   Shughuli kuu za  mkutano: Kupanga jinsi ya kufuatilia utekelezaji wa njia za ufumbuzi.

Kwa mfano, kuna  kamati  4, na kila kamati inawajibika kufanya ufuatiliaji ili kujua iwapo yale waliyopanga yanafanikiwa au la.

Anza na kamati mojawapo – mathalan kamati moja inataka kuanzisha mafunzo kwa wakunga wa jadi.

Ili kupata jibu kwa  jinsi gani mtafanya ufuatiliaji wa mpango huu, ongoza kikundi cha  Tushikamane kupitia mchakato ufuatao:

A.   Jadili na kukubaliana  manufaa gani yatatokana na ufumbuzi huo? Kwa mfano, mama atapona haraka baada ya kujifungua na hatapoteza maisha; wakunga wa jadi watakuwa na ufanisi zaidi katika utendaji wao; wanawake watajisikia salama zaidi na hisia kutengwa wanapokuwa wanajifungua kupungua; mahusiano imara zaidi yatajengwa baina ya programu na vituo vya kutolea huduma za afya; nk.

B.   Ulizia maoni yao juu ya nani atanufaika na matunda kutokana na ufumbuzi huo?  Kwa mfano, wanawake wote  wanaojifungua; pia hospitali kwa sababu kazi ya kushughulikia makosa ambayo yanatokana na utendaji wa wakunga wa jadi itapungua; wakunga wajadi wenyewe ambao uwezo wao utaongezeka; jamii kwa sababu mama atapona haraka zaidi baada ya kujifungua, nk.

C.   Jadili na kukubaliana  lini watu hao watanufaika na ufumbuzi huo.  Kwa mfano, mara nyingi; mara moja kwa mwezi; mara moja katika maisha; nk. Hakuna sababu ya kujaribu kufanya ufuatiliaji wa kitu ambacho hutokea ghafla au  kwa nadra.

D.   Jadili na kukubaliana  wapi watu watanufaika.  Kwa mfano, ni watu wa  kitongoji hiki, au pia watu kutoka vijiji vyote vya jirani ?.

E.   Maswali hayo yatakupa msingi wa kujadili na kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji ambao utakuambia iwapo njia ya ufumbuzi inayotekelezwa inafanikiwa.

Kwa mfano, haishi kujua kwamba mtu alikuja kutoa mafunzo kwa wakunga wa jadi. Tunaweza pia kutaka kujua, kwa mfano, ni wakunga wa jadi wangapi wameanza mafunzo?; wangapi wamemaliza?; wameyatumia mafunzo waliyoyapata namna gani ili kuleta mabadiliko?; Kituo cha Afya au Hospitali imeona tofauti yoyote? Je jamii imeona mabadiliko yoyote?

Kamati itapataje majibu kwa maswali haya? Watakapokuwa na majibu wanaweza kusherekhea mafanikio, na pia kukabiliana na changamoto ambazo zitagundulika kuzuia  shughuli au ufumbuzi kwenda vizuri.

Mchakato huu kwa kamati ya kwanza utakapokamilika, na ufumbuzi wake uliopangwa, kikundi cha Tushikamane baada ya hapo kitajadili mpango wa kufanya tathmini ya shughuli zingine zilizopangwa, au kurudia hatua A hadi E juu.

 4.Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi.    Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?
 5. Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa vya kutosha. Kama hapana, unaweza  kurudia  baadhi au vipengele vyote  vya mkutano.
6.Himiza washiriki kuuliza maswali
7.Panga tarehe ya mkutano ujao, mfano miezi 3 hadi 6 kutoka sasa, tarehe ambayo inaacha  muda wa  kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zilizopangwa.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 11

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·         Ni mpango gani wa ufuatiliaji ambao umeandaliwa kwa kila ufumbuzi uliopangwa ?

Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 11

·         Makatibu wanapaswa kuwaorodhesha wahudhuriaji wote kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.


Baada ya mkutano wa  11, sasa ni wakati wa kuanza utekelezaji.
Kila kamati inahitaji msaada wako na msaada wa timu nzima ya  Tushikamane, kadri itakavyokuwa ikitekeleza shughuli na ufumbuzi ambazo ilipanga.

·         Wamekwisha kutambua  rasilimali ambazo wanahitaji, na hatua zinapaswa kuwa zimechukuliwa katika kutafuta rasilimali hizi.

·         Wana mpango kazi na wanajua nani anahusika kwa kufanya nini, na lini.

·         Wamekubaliana juu ya mfumo wa ufuatiliaji wa maendeleo ya shughuli zao. 

·         Unapaswa kukutana na kamati mara kwa mara katika kipindi hiki, kupitia maendeleo ya utekelezaji, kusherehkea mafanikio na kubainisha na kushughulikia changamoto ambazo zitakuwa zimejitokeza. 

Ratiba ya  mikutano  itaamuliwa na wanakikundi wenyewe.




AWAMU YA  4 – KUFANYA TATHMINI PAMOJA


Shabaha ya Awamu ya  4 ya mzunguko wa mikutano ni kutathmini matokeo ya njia za  ufumbuzi ambazo zinatekelezwa juu ya matatizo makuu yaliyobainishwa.  Awamu hii ina mikutano 3:

Mkutano wa  12: Maendeleo ya mchakato wa tathmini. Baada ya mkutano, wanakikundi watahitaji kuwa na uhakika  kuwa wanaendelea  vizuri katika ukusanyaji wa taarifa wanazohitaji kwa ajili ya  kufanya tathmini ya matokeo ya shughuli zao  juu ya matatizo ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo.

Mkutano wa 13: Kufanya tathmini ya kazi za kamati, kikundi cha  Tushikamane na mchakato wa  Tushikamane.

Mkutano wa  14: Kupanga kwa ajili ya siku za usoni.



MKUTANO WA 12 – MAENDELEO YA MCHAKATO WA  TATHMINI

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 12

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu muhimu kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  11. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha wapi  programu inapoelekea: kuwapa  sauti wanawake walio katika umri wa uzazi katika mipango ya   kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga. Hii hatimaye itavutia misaada ya hali na mali kutoka nje ya kitongoji, ambayo itaunganishwa na juhudi za jamii, na kuleta msukumo mkubwa katika kuzuia vifo hivyo vya kusikitisha.

Wakumbushe watu maarufu kwenye kitongoji  kwamba mkutano ujao utajaribu kubuni njia mbalimbali za kusaidia kujua iwapo mchakato wa Tushikamane unafanya kazi, na wao wenyewe wanaweza kuwa na chochote cha kuchangia.

Endelea kuwaeleza  kwamba  wadau wengine nje ya mchakato ambao wangependa kusaidia watataka kujua kama kweli mchakato huu unafanya kazi vizuri. Mashirika yenye  rasilimali yanaweza  kusaidia  mchakato au programu  kama watajua programu hiyo ina utaratibu  wa kufuatilia na kupima mafanikio yake.

Mkutano unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu maarufu wote kwenye kitongoji  kuwepo.

Mkumbushe Mwenyekiti wa kila kamati kwamba ataombwa  kukitaarifu kikundi jinsi  mchakato wa tathmini yao unavyokwenda !


Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa 12 ?

Wanawake wote waliohudhuria Awamu ya 1 na 2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza, na  wengine wapya waliohudhuria mkutano wa 11. Pia, kikundi kitakuwa kimebaini watu maarufu kupitia mikutano iliyopita ambao ushiriki wao utasaidia kikundi kufanya kazi vizuri na kuongeza uwezekano wa kufanikiwa.

Fikiria watu wengine mmoja mmoja  ambao wana umuhimu kuhudhuria-kwa mfano mtu yeyote mwenye uzoefu katika ufuatiliaji. Watu kama hao ni pamoja na  wafanyakazi wa afya vijijini, lakini pia baadhi ya wenyeviti wa vijiji, waalimu, nk.



Ajenda ya Mkutano wa  12
1.    Makaribisho. Utambulisho kama kuna washiriki wapya.

2.    Mapitio ya Awamu ya  3 na kuwakumbusha watu kiasi gani tayari kimefanyika.

3.    Kuwasilisha malengo ya mkutano, ambayo ni kupata ari na utayari wa kufanya tathmini  ya mradi. Jadili kwa nini tathmini ni muhimu, na hasa sisitiza kuwa  uwezekano wa kuvutia misaada kutoka nje utakuwa mkubwa  zaidi kwa sababu jamii inaweza kuonesha kwamba siyo tu wanayashughulikia matatizo yao, lakini pia wana utaratibu wa kupima matokeo.

Hadithi ifuatayo inatoa njia moja wapo ya kukisaidia kikundi kuelewa kwa nini tathmini ya ukweli  inathaminiwa sana,  hasa kwa sababu husaidia:

·         Kutazama  nyuma na kuona maendeleo;
·         Kubainisha mambo ambayo yalikwenda vizuri,na ambayo wanapaswa kuendeleza ;
·         Kubainisha changamoto na kuona wapi hasa penye tatizo;
·         Kukabiliana na tatizo sahihi kwa njia sahihi;
·         Kusherekhea mafanikio!


Wasomee hadithi hii: "Bibi. [weka jina], kutoka [weka jina la kijiji] , aliamua kuwekeza katika biashara ya kutengeneza mikate. Aliajiri wafanyakazi 3 ambao walimsaidia katika ujenzi wa jiko la bekari hiyo, kuanzisha kiduka kidogo cha rejareja, na kutengeneza mikate yenyewe. 

Mzunguko wa kwanza wa uzalishaji wa mikate midogo ya skonzi  ulitoa mikate yenye kiwango cha chini. Hivyo  alipata shillingi  2,000 tu.  Bibi [weka jina] alisikitika na kufikiria kuwa kiwango kidogo cha bidhaa zake kilitokana na malighafi aliyoitumia. Hivyo, aliamua kununua malighafi tofauti na kuitumia kutengeneza mzunguko wa pili wa skonzi. 

Hata hivyo, skonzi zilizozalishwa katika mzunguko wa pili  zilikuwa mbaya hata kuliko za mzunguko wa kwanza!  Bibi. [weka  jina] alisikitika tena na kuomba ushauri kutoka kwa rafiki yake ambaye alikua akijishughulisha na ufugaji kuku. Ingawa jamaa huyu alikuwa hajui chochote juu ya  kutengeneza mikate, alimwambia kuwa huenda wafanyakazi walikua wakimwibia   malighafi na kuwauzia  wafanyabishara wengine wanaotengeneza mikate. Bibi   [weka jina] alikasirika sana na wafanyakazi wake na kuwaamuru wafanye kazi miezi 3 bila mshahara. 

Mzunguko wa 3 walitengeneza skonzi   za kiwango  kile kile cha chini!  Bibi [weka jina] alisikitika tena na kuamua kutafuta ushauri kutoka kwa mtengenezaji mikate mwenzake. Mwanamke huyu alijua mambo mengi juu ya biashara hiyo na kumwambia Bibi[weka jina] kwamba wafanyakazi wake hawakuwa na utaalam wa kutengeneza mikate.Kabla ya hapo, walikuwa wanafanya kazi kama walinzi kwenye bekari mmoja mjini. Hawakua na stadi zozote katika uokaji mikate.  Bibi [weka jina] aliamua kuajiri wafanyakazi wapya wenye stadi za utengenezaji mikate na mzunguko wa 4  ulizalisha skonzi zenye  ubora wa hali ya juu.

Wezesha mjadala mfupi, kwa mfano kwa kuuliza maswali yafuatayo:
Tumesikia nini kwenye hadithi hii?
Mambo kama hayo huwa yanatokea?
Kwa nini yanatokea?
Tumejifunza nini kutokana na hadithi hii?

·         Katika mzunguko wa kwanza wa kutengeneza skonzi, hakuajiri watu sahihi.
·         Katika mzunguko wa pili, alifanya mabadiliko bila kuchunguza  tatizo lilikuwa nini. 
·         Katika mzunguko wa 3, alipata ushauri kutoka kwa mtu asiye na utaalam katika utengenezaji wa mikate. 
·         Katika mkutano wa 4, alipata ushauri kutoka kwa mtaalam na kutathmini tatizo kwa usahihi.


4.   Shughuli kuu za mkutano: Kuangalia maendeleo ambayo yamefanyika katika kutathmini kila mojawapo wa  miradi 4( kila kamati inatekeleza mradi wake).

Kila moja wapo ya (mfano)  kamati 4 inapaswa kuwasilisha, moja baada ya nyingine, yaliyoamuliwa katika mkutano wa  11 juu ya ufuatiliaji wa mafanikio ya shughuli yao. Wamefika hatua gani katika utekelezaji wa mifumo ya ufuatiliaji? Je wameanza kupata mafanikio? Wamekumbana na matatizo yoyote katika utekelezaji wa ufuatiliaji, na kama ndivyo, unaweza wewe au kikundi kusaidia kuyatatua matatizo?

Rudia mchakato kwa kila kamati.


    5.Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi.     Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?
    6. Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa vya kutosha. Kama hapana, unaweza kurudi nyuma na kurudia  baadhi au vipengele vyote  vya mkutano.
    7.Himiza washiriki kuuliza maswali
    8.Panga tarehe ya mkutano ujao ambayo inatakiwa kuwapa watu nafasi ya kutosha  kutekeleza shughuli zilizopangwa-mfano miezi 3 hadi 6 kutoka sasa.


Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 12

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·         Zoezi la tathmini limeonesha matokeo gani kwa kila tatizo kuu ambalo  lilitambuliwa ?

Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 12

·         Makatibu wanapaswa kuorodhesha wahudhuriaji wote kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.

·         Tembelea kila mwenyekiti wa kamati, pamoja na watu wengine maarufu ambao ungependa washirikishwe, au waliokubali kusaidia juhudi hiyo. Wahimize kuuboresha mfumo wa  tathmini ya mradi wao, na kuwauliza msaada gani wangehitaji ili kufanikisha kazi hii.
·         Jadili mambo haya na msimamizi wako, na kuyaleta pia kwenye mkutano wa kila mwezi na Kiongozi wa Mradi na Mwenyekiti wa Mradi. Ili  kusaidia kulifanikisha hili, watahitaji kuwa na ufahamu bayana wa changamoto ambazo kamati zinakabiliana nazo, na nini hasa kila kamati inatafuta.



MKUTANO WA  13 – KUFANYA TATHMINI YA MATOKEO YA MIRADI YA  TUSHIKAMANE NA TUSHIKAMANE YENYEWE

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 13

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu maarufu  kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  11 na 12  .

Wakumbushe watu maarufu kwenye kitongoji  kwamba mkutano ujao utajaribu kufanya tathmini ya mwisho kupima iwapo mchakato wa  Tushikamane unafanya kazi. Wanaweza kuwa na chochote cha kuchangia, lakini  nao pia wangetaka kujua matokeo.

Endelea kuwaeleza  kwamba  wadau  au asasi zenye uwezo wanaweza  kusaidia  mchakato au programu yenye mafanikio, na ambayo inaweza kuthibitisha au kuonesha  mafanikio hayo.

Mkutano unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu  waliotoa mchango mzuri katika mkutano uliopita   kuwepo.

Mkumbushe Mwenyekiti wa kila kamati kwamba atatakiwa kutoa taarifa kwa  kikundi jinsi  zoezi lao  la tathmini linavyoendelea  !!


Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa  13?
Wanawake wote ambao wamekuwa wakishiriki kwa njia yeyote ile katika mchakato huu.

Wakumbushe viongozi na watu maarufu kwenye jamii kwamba ni muhimu sana kuhudhuria mkutano huu, ili waweze kujua iwapo mchakato wa Tushikamane ulifanikiwa au hapana.


Ajenda kwa ajili ya Mkutano wa  13
1.    Makaribisho. Utambulisho kama kuna washiriki wapya.

2.    Mapitio ya mkutano uliopita ambao ulikazia sana suala la tathmini.

3.    Kuwasilisha malengo ya mkutano:
·         Kufanya tathmini kupima jinsi matatizo makuu  yalivyoshughulikiwa.
·         Kufanya tathmini ya utendaji wa kikundi.
·         Kupanga kwa ajili ya siku za usoni.

4.   Shughuli kuu za mkutano: Kufanya tathmini ya mchakato mzima, mafanikio na changamoto kuhusiana na mchakato wa Tushikamane, na kazi za kamati katika kukabiliana na matatizo makuu yaliyobainishwa.

Muda wa mkutano wa  13 utapokaribia, timu ya Tushikamane itapanga  jinsi gani watakaa pamoja kama kikundi cha  Tushikamane kufanya tathmini hii.

Kinachotakiwa ni kutoka na picha iliyowazi ya kiwango cha mafanikio katika maeneo yafuatayo:

·         Ushiriki katika vikundi na kwenye mikutano;
·         Kubainisha matatizo na mizizi yake;
·         Ufanisi wa kamati katika kushughulikia  matatizo hayo na mizizi yake; kukiwa na  maelezo mafupi juu ya  mafanikio na changamoto muhimu.
·         Ubia au ufadhili na mahusiano muhimu na wadau wengine ambayo yalianzishwa.
·         Uwezeshaji na usimamizi wako;
·         Tathmini ya mchakato wa  Tushikamane  – mzunguko wa mikutano  14 kama njia ya kusonga mbele.

Lingekuwa jambo zuri kuweka  alama halisi (mfano kati ya 5) kwa kila eneo, pamoja na maelezo ya mafanikio na vikwazo.
5.   Jinsi ya kuboresha zaidi shughuli za programu: kwa eneo au suala lolote  katika tathmini ambalo lilipata alama chini ya wastani, ongoza mjadala kwa lengo la kufanya eneo au mtu husika kufanya kazi kwa  ufanisi zaidi katika shughuli zijazo.
6.    Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi.    Nani atafanya nini  kabla ya mkutano unaofuata?
7.    Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa vya kutosha. Kama hapana, unaweza kurudi nyuma na kurudia  baadhi au vipengele vyote  vya mkutano.
8.    Himiza washiriki kuuliza maswali.
9.    Panga tarehe ya mkutano ujao –mfano miezi 3 hadi 6 kutoka sasa, ili kuwapa watu muda wa kutosha  kutekeleza shughuli zilizopangwa.

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 13

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto gani?
·         Ni maendeleo, mafanikio, na changamoto gani ambazo kikundi kizima kimepata, na kamati moja moja  ?


Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 13

·         Makatibu wanapaswa kuwaorodhesha washiriki  wote kwenye rejesta ya kikundi.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Fanya mkutano wa nusu saa na   timu nzima ya Tushikamane  kujadili matokeo ya tathmini na kufanya mapendekezo.









MKUTANO WA  14 – KUPANGA  KWA  AJILI  YA  SIKU  ZIJAZO

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 14

Soma Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.

Tembelea watu maarufu  kwenye  kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa  13.

Wakumbushe watu maarufu kwenye kitongoji  kwamba mkutano ujao ni kuamua nini cha kufanya baada ya hapo walipofikia. Kwa hivyo, mawazo yao ni muhimu na yanahitaji kuzingatiwa. Wakumbushe wanawake ambao wametoa mchango mkubwa katika mchakato huu kuwa ni muhimu  kuhakikisha kuwa sauti za wanawake zinaendelea kusikilizwa. 

Mkutano utapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu  waliotoa mchango mzuri katika mkutano uliopita   kuwepo.



Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano wa  14?
Huu ni mkutano wa  kitongoji kizima. Wakumbushe viongozi na watu wengine maarufu  kwamba huu ni mkutano muhimu sana kuhudhuria, ili waweze kusaidia kupanga hatua zitakazofuata.

Timu nzima ya  Tushikamane inapaswa kuhudhuria – Mchungaji Mgego, Mwenyekiti; Wilbard Mrase, Kiongozi wa Mradi; na Alex Gongwe, Msimamizi wa Mradi.

Muhimu zaidi, wanawake ambao wamekuwa wakishiriki katika mikutano yote ya Tushikamane wanaweza kuja kusherekhea mafanikio – na kusaidia kuhakikisha kuwa wataendelea  kusikilizwa, na kuchangia  kuboresha afya ya baadaye ya dada zao na mabinti zao – na watoto wao.


Ajenda kwa ajili ya Mkutano wa  14
1.    Makaribisho, mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita, na utambulisho

2.    Kuwasilisha lengo la mkutano: Kuamua nini kifanyike na kikundi-hatima ya kikundi.

3.    Kujadili kazi gani ambayo bado haijafanywa na kikundi

4.    Kufanya majumlisho ya mkutano

5.    Kufanya mipango ya baadaye!
6.    Kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano unaofuata

Chagua tatizo moja kuu na kukiongoza  kikundi kupitia mchakato wa maamuzi ufuatao:
1.Tatizo kuu limeshughukiwa vya kutosha? Kama NDIYO: basi kikundi kinapaswa kurudi kwenye Awamu ya 1 kubainisha na kuainisha matatizo mapya ambayo  yatapewa kipaumbele.



    2. Kama HAPANA:

Tatizo sahihi ndiyo  lililoshughulikiwa ?  Kama hapana, rudi nyuma na kuchagua tatizo lingine.

Huenda lilikuwa tatizo sahihi, lakini ufumbuzi uliotekelezwa ndiyo haukuwa sahihi, kwa sababu haukuikabili  ipasavyo  mizizi ya tatizo , au  kuambatana na  shughuli za uzuaji na /au usimamizi wa tatizo hilo ?

Kama hilo ndilo tatizo, basi kikundi kinaweza kurudi kwenye Awamu ya  2, na kuangalia tena mizizi ya tatizo, na kupanga mikakati mbalimbali ya kutatua mizizi ya tatizo na kuzuia tatizo kutojitokeza.

Vinginevyo, huenda tatizo lilikuwa sahihi na mipango ya ufumbuzi ilikuwa nzuri, lakini haikufanikiwa. Kama sivyo , ni sababu gani zingine? Hii inaweza kurekebishwa?

Au ni kwamba unahitaji muda  zaidi ?

Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 14

·         Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi  walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·          Mkutano uliendaje – je kulikuwa na  mafanikio au changamoto zozote?
·         Ni hatua gani zitafuata ?


Nini kifanyike baada ya Mkutano wa 14

·         Makatibu wanapaswa kuwaorodhesha  kwenye rejesta ya kikundi washiriki  wote.
·         Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·         Fanya mkutano wa  timu nzima ya Tushikamane, kujadili matokeo ya tathmini na kufanya mapendekezo.