KIONGOZI CHA TUSHIKAMANE
YALIYOMO
Majukumu na wajibu wa Mwezeshaji
wa Tushikamane
Maarifa ya Mwezeshaji wa Tushikamane juu ya Afya ya Mama
na Mtoto
Mchanga
Kuwa Mwezeshaji
Stadi za kufanya kazi na vikundi
Mzunguko wa Mikutano ya Tushikamane
Kuandaa ripoti za Tushikamane
Awamu ya 1: Kubainisha matatizo
pamoja
Mkutano wa 1: Kitongoji kukaa pamoja kuunda kikundi
Mkutano wa 2: Wanawake
katika umri wa uzazi kubainisha matatizo ya
afya
ya wanawake.
Mkutano wa 3: Wanawake katika umri wa uzazi kubainisha
matatizo ya
watoto wachanga
Mkutano wa 4: Kuainisha matatizo yatakayopewa kipaumbele
Mkutano wa 5: Kubainisha mambo ya msingi ambayo
yanachangia
matatizo hayo – mizizi ya matatizo
Awamu ya 2: Kupanga ufumbuzi
pamoja
Mkutano wa 6: Kubainisha shughuli za uzuiaji na usimamizi
wa matatizo hayo.
Mkutano wa 7: Kuandaa mpango kazi
Mkutano 8: Kuwasilisha taarifa juu ya maendeleo ya kikundi kwa wanajamii
Awamu ya 3: Kutekeleza njia za
ufumbuzi pamoja
Mkutano wa 9: Kupanga njia za ufumbuzi
Mkutano wa 10: Kukusanya rasilimali
Mkutano wa 11: Kuandaa mfumo wa ufuatiliaji
Awamu ya 4: Kutathmini pamoja
Mkutano wa 12: Maendeleo
ya mchakato wa tathmini
Mkutano wa 13: Kutathmini
mafanikio ya miradi na Vikundi vyenyewe
vya Tushikamane
Mkutano wa 14: Kupanga kwa ajili ya siku zijazo
SHUKRANI
Taasisi ya Afya Ulimwenguni ya Chuo Kikuu cha London
(The Institute for Global Health at University College, London), ina dhamira
kubwa ya kupunguza vifo vya akinamama na watoto wachanga katika nchi
zinazoendelea. Nchi nyingi zimekuwa
hazipati mafanikio yanayotarajiwa, na Prof Anthony Costello na timu yake katika
taasisi hiyo walikuwa na dira ya kuziona jamii zikihamasishwa kushiriki kwa
bidii katika mipango yao ya maendeleo.
Kilichofuata ni utafiti wenye kiwango cha hali ya juu,uliowezesha kugundua utaratibu wenye ufanisi mkubwa: Njia ya uhamasishaji
jamii yenye uhakika wa kusaidia kupunguza vifoo na kuleta maboresho katika afya
ya watoto wachanga, watoto wadogo na mama zao kwa kiwango kikubwa na kwa
gharama nafuu.
Kutokana na ugunduzi huo lilianzishwa Shirika la
hiyari la kuwahudumia wanawake na watoto liitwalo Women & Children First, au ‘Wanawake na
Watoto Kwanza’ likikusudia kutangaza manufaa ya njia hiyo kwa jamii zenye mahitaji makubwa sana duniani.
Mikey Rosato ni Meneja Mwandamizi wa
Programu katika shirika hilo, na anaongoza majaribio zaidi kwa niaba ya Shirika
la Afya Duniani juu ya Utaratibu wa Kujifunza na Utendaji Shirikishi kwa lengo la kupunguza
vifo vya akinamama(PRA).
Kazi za shirika la
Wanawake na Watoto Kwanza - Women & Children First, zinajenga kwenye mafanikio ya juhudi za
Shirika la Afya Duniani, Idara ya Afya ya Mama, Watoto na Uzazi, na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani UNICEF. Kwa pamoja, wameanzisha
uandaaji wa zana kwa ajili ya uhamasishaji
jamii juu ya Afya ya Akinamama na Watoto, kama nyongeza kwa zana zingine ambazo
tayari zinatumika kwa ajili ya matunzo ya watoto wachanga na watoto wadogo
kwenye jamii (2012), na Huduma
ya Kumtembelea Mtoto Mchanga Nyumbani: mkakati wa kuboresha uhai (2009).
Mafanikio ya
uhamasishaji jamii, mizunguko ya kujifunza, na utendaji shirikishi
yameimarishwa na kazi za Mradi wa MaiMwana
nchini Malawi. Florida Banda na timu
yake wameisaidia sana na kuipa moyo Tushikamane.
Mwaka 2015, Mikey
Rosato na timu yake waliweka pamoja zana hizi kwenye Kiongozi chao cha Shirika
la Afya Duniani, mahali
ambapo Kiongozi hiki kimetoka, na kuzifanya zana kuwa rafiki zaidi kwa wawezeshaji wa msitari wa mbele wa Mradi wa Tushikamane(tunaomba radhi kwa makosa yoyote yatakayojitokeza!).
Tunawashukuru mno mno. Asante sana sana!
REJEA
http://www.maimwana.org/
http://www.biomedcentral.com/1471-2393/14/243/abstract
http://apps.who.int/iris/bitstream/10665/127939/1/9789241507271_eng.pdf?ua=1
http://www.who.int/pmnch/countries/tanzaniamapstrategic.pdf
KIONGOZI CHA TUSHIKAMANE
Jinsi
ya kuendesha Vikundi vya Tushikamane kupitia
mzunguko wa mikutano 14
Vikundi vya Tushikamane
Tushikamane
ni neno la Kiswahili ambalo linatumika kumaanisha vikundi ambavyo vimeanzishwa chini ya miradi inayofanana
, hasa Mradi wa Malawi, unaoitwa ‘MaiMwana’.
Katika mradi huo, vilijulikana kama Vikundi vya Kujifunza na Utendaji
Shirikishi kwa ajili ya Afya ya Mama na Mtoto Mchanga(‘Participatory Learning
and Action Groups for Maternal and Newborn Health’). Kichwa hiki kinaeleza vizuri namna vinavyofanya kazi na kusudi lake: kwamba
jamii hushiriki na kujihusisha kwa undani katika kutafuta njia za kuzuia vifo
vya kusikitisha vya akinamama na watoto
wao.
Vikundi
vya Tushikamane pia hulenga kuleta maboresho
katika afya ya mama na watoto wachanga na kupunguza vifo kwa kutoa fursa za
majadiliano, mahali ambapo wanajamii
hususan wanawake, huweza kubainisha vipaumbele vyao kuhusiana na matatizo ya
afya ya mama na mtoto mchanga na kubuni, kutekeleza na kutathmini njia za
ufumbuzi zinazotokana na jamii yenyewe.
Kikundi kimoja cha Tushikamane kitaanzishwa katika kila kitongoji, kwa kuanzia
katika vitongoji 6. Nchini Tanzania, mahali ambapo unakuta nyumba zote katika viitongoji wakati mwingine havitengenezi kijiji kimoja, tutatumia tafsiri iliyotumika
katika Sensa ya Taifa ambayo
inasema kuwa kitongoji kinapaswa kuwa na
takriban watu 700.
Vikundi vya Tushikamane vitaanza kwa kuandikisha
wanawake walio kwenye umri wa uzazi kama wanakikundi, ili kuwa na uhakika wa
kuwapatia wanawake vijana sauti katika maamuzi juu ya jinsi ya kushughulikia
matatizo yanayowakabili. Wajawazito, wanawake
ambao ndiyo wamejifungua mara ya kwanza, na wasichana balehe wahimizwe
kushiriki. Wanajamii wengine wote ambao
wanahusika na masuala ya afya ya mama na
mtoto mchanga, wakiwemo wanaume, wanawake wenye umri mkubwa na viongozi wa
jamii pia wanastahili kuhudhuria na wataeleweshwa juu ya shabaha ya vikundi hivi ambayo ni wanawake.
Vikundi vitaongonzwa na mwezeshaji wa kike kupitia
mzunguko wenye awamu 4 za
mikutano. Mwezeshaji huyu (Esther
Rehema), atasaidiwa na Msimamizi, (Alex Gongwe), Kiongozi wa Mradi,
(Wilbard Mrase), na Mwenyekiti wa Mradi, (Isaac Mgego).
MUUNDO WA KIONGOZI HIKI
Kiongozi hiki ni kwa ajili ya
watumishi wote wa Mradi wa Tushikamane ili
waweze kuelewa mambo ambayo yanahitaji kufanyika, na namna gani. Lakini
kimewalenga zaidi Wawezeshaji – kuwaongoza hatua kwa hatua kuunda na kuendesha
vikundi.
Kwa sababu hii, Kiongozi hiki kimeandaliwa
maksudi kwa ajili yako, Esther na Rehema, na ni kama vile kinaongea na ninyi !
VIFUPISHO
VHW Village Health Worker (Mfanyakazi wa
Afya Vijijini)
MNH Maternal and Newborn Health (Afya
ya Mama na Mtoto Mchanga)
TBA Traditional Birth Attendant
(Wakunga wa Jadi)
NGO Non-Governmental Organisation –
eg charities (Shirika lisilo la
Kiserikali- mfano Shirika
la Misaada)
MAJUKUMU
NA WAJIBU WAKO
Katika Mradi wa Tushikamane, wewe mwezeshaji utakuwa na majukumu
kwenye maeneo yafuatayo:
1. Uundaji
wa vikundi
2. Utekelezaji
wa mzunguko wa mikutano 14, kuainisha matatizo
yanayohusiana na vifo vya mama na watoto wachanga na kuweka vipaumbele.
3. Rufaa
kwa ajili ya mama au mtoto yeyote kwenye kituo cha afya kama itaonekana
inahitajika
4. Kujenga
mtandao na viongozi wa jamii, wafanyakazi wa afya vijijini, wakunga wa jadi,
viongozi wa serikali za vijiji na mitaa na wadau wengine
5. Kutoa
ripoti kwa Msimamizi na kwa Kiongozi wa Mradi – mathalan juu ya idadi ya
mikutano; mahudhurio; shughuli ambazo zimekamilika; mafanikio; changamoto; nk.
6. Kuhudhuria
mikutano ya kila mwezi ya timu nzima kwa ajili ya kupokea ripoti hizi, kujadili
mafanikio, na kubadilishana mawazo nk.
UELEWA JUU YA AFYA YA
MAMA NA MTOTO MCHANGA
Ili kuviwezesha
vikundi vya Tushikamane kwa ufanisi na
kuwasaidia wanavikundi ipasavyo, utahitaji uelewa wa msingi juu ya masuala ya
afya ya mama na mtoto mchanga. Ingawa siyo wajibu wako kuwaelimisha wanakikundi,
unahitaji taarifa za kutosha ili uweze kusaidia kujaza mianya katika uelewa wa
pamoja, kubainisha vitendo hatarishi na kujibu maswali mahsusi ambayo unaweza
kuulizwa.
Hivyo,
unapaswa kuwa na uelewa wa kutosha juu ya masuala yafuatayo ili uweze
kuyazungumzia vizuri na kwa kujiamini ndani ya kikundi:
·
Huduma maalum kwa mama na mtoto kabla ya kuzaliwa – ziara ya kwanza,
ya pili, ya tatu na ya nne
·
Huduma kwa wajawazito nyumbani – lishe, mapumziko na uzuiaji wa malaria
·
Kujiandaa kujifungua – kituo/hospitali atakapojifungulia, na uwepo wa
mtaalam mwenye uzoefu, usafiri, fedha, kufanya maamuzi, vifaa vitakavyohitajika
kwa ajili ya uzazi safi na salama, dalili za uchungu wa uzazi
·
Dalili
za hatari wakati wa ujauzito
·
Dalili
za hatari wakati wa kujifungua
·
Dalili za hatari kwa akinamama baada ya kujifungua
·
Dalili za hatari kwa mtoto mchanga baada ya kuzaliwa
·
Huduma kwa mama na mtoto mchanga
nyumbani – huduma ya nyumbani kwa mama
mara baada ya kujifungua, utunzaji wa rulela (kitovu), kuzuia maambukizi, kumuogesha
mtoto mchanga, unyonyeshaji maziwa ya mama, chanjo, ulinzi na usalama, huduma
ya kangaroo.
·
VVU na UKIMWI na umuhimu wa wenzi wote wawili kupimwa
·
Uzuiaji wa maambukizi ya virusi
vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
·
Uzazi wa mpango
·
Haki na wajibu wa akinamama na
wafanyakazi wa afya
Uelewa wako juu ya afya ya mama na mtoto unapaswa kupimwa na Msimamizi na /au Kiongozi wa Mradi/Mkufunzi.
UNAPOKUWA MWEZESHAJI
Kwa nini kutumia neno ‘Mwezeshaji’?
Unaitwa
Mwezeshaji siyo kiongozi au mwalimu, kwa sababu kazi yako siyo kuwambia watu
kipi cha kufanya, wala kuwafundisha kipi cha kufanya. Badala yake unapaswa
kuwasaidia wao wenyewe kugundua kipi cha
kufanya, na wapange ajenda yao wao wenyewe.
Mwezeshaji ni muonesha njia ambaye:
·
huhakikisha kila mtu katika kikundi
anamsikiliza mwenzake
·
huuliza maswali ili kukisaidia kikundi
kuamua wafanye nini
·
hujenga juu ya uelewa wa wanakikundi ili
kuwasaidia wenyewe kutafuta majibu kwa masuali yaliyoko mbele yao
·
ana wajibu wa kukisaidia kikundi kutekeleza majukumu yake
·
huruhusu
kikundi kujitathmini na kupata picha ya kiwango cha mafanikio yao.
Hupaswi
kuwa:
·
usukani
au mwendeshaji wa kikundi;
·
mtaalam
wa kikundi;
·
mwenye
kujua zaidi kuliko wengine;
·
anayefanya
maamuzi yote
·
anayefanya
tathmini jinsi kitongoji kinavyoendelea
Katika
masuala yote haya, Vikundi vya Tushikamane ndivyo vinapaswa kuwa usukani; kutafuta
utalaam; kuamua kipi ni bora zaidi; kutathmini maendeleo yao; nk.
Unapokuwa unafanya kazi kama Mwezeshaji, hali hii
itatoa fursa kwa kila mtu katika kikundi kueleza mawazo yake na kujisikia kuwa
sehemu ya timu. Kwa kuwa kikundi kinafikia maamuzi pamoja, inakuwa rahisi kwa
wanakikundi, mmoja mmoja, kusaidia kufanikisha malengo ya kikundi.
Kuliko kuwapa wanakikundi majibu,
elimu inapaswa kuwaongezea uelewa ili waweze kubaini matatizo na visababishi
vyake, na kuyatafutia ufumbuzi. Jukumu la Mwezeshaji ni kukisaidia Kikundi kupitia mchakato huu kwa
kuuliza maswali ambayo yanachochea njia mpya za kufikiri na kufanya uchambuzi
wa hali zao. Mwezeshaji hana majibu
yote. Jukumu lake ni kukisaidia kikundi kufikiria
kwa makini juu ya mahitaji na maslahi ya kikundi, na kufanya maamuzi wenyewe.
Jukumu la Mwezeshaji ni kumtia
moyo kila mwanakikundi kuchangia kadri ya uwezo wake. Kila mtu ana maarifa
muhimu na anaweza kutoa mchango muhimu. Lakini
watu wengi kawaida hawana utayari wa kuwashirikisha wengine juu ya ujuzi au
maarifa yao. Wanaweza kuwa wanakosa ujasiri au kufikiria kuwa yale wanayoyajua
siyo muhimu. Wakati mwingine hawataki
kuwamegea wengine maarifa au
taarifa zao kwa sababu kuyahodhi huwapa nguvu na fursa zaidi juu ya wengine.
Hata hivyo, tunaposhirikishana
maarifa yetu, kila mtu hufaidika. Mtu ambaye anawashirikisha wengine hapotezi
maarifa hayo, na mtu anayepokea atakuwa amepokea nyenzo mpya ambayo pia anaweza kuwashirikisha wengine. Jukumu la Mwezeshaji ni kujenga hali
ya kuaminiana na kuheshimiana miongoni
mwa wanakikundi na kuchochea majadiliano
na kujifunza, ambavyo hunufaisha kikundi kizima.
MBINU ZA KUFANYA KAZI NA VIKUNDI
Kutafuta
watu wa kijiunga na vikundi
Unapokua unatafuta watu wa kuhudhuria mikutano na kuwatia moyo kuendelea
kuhudhuria, unapaswa kujaribu njia mabalimbali zikiwemo:
·
Kwenda na kuandikisha wanakikundi nyumba kwa nyumba, au kupitia
kamati na mwanakikundi mmoja mmoja
·
Barua kwa watu wanaostahili kuhudhuria
·
Matangazo kwenye mikutano ya vijiji, shughuli na matukio mengine kijijini
·
Nyimbo na ngoma kabla ya kuanza mikutano
·
Kueleza kusudi na manufaa
ya kuhudhuria mikutano
·
Kueleza kwa nini afya ya mama na mtoto ni muhimu kwa wanawake na jamii
nzima
·
Usiwafanye watu kutarajia mambo yaliyo
juu ya uwezo wako au wa programu – kuwa mkweli juu ya jukumu lako
·
Mikutano kufanyika muda na sehemu mwafaka
·
Kusherekhea mafanikio na ushindi, hata ukiwa mdogo
Muhimu: ni jukumu lako
kuwakumbusha washiriki lini mkutano mwingine utafanyika
na mada itakayojadiliwa.
Kuweka kanuni
ili vikundi viweze kufanya kazi vizuri
Unahitaji
kuhakikisha kuwa wanakikundi wote wanashiriki kwa usawa, na wanaume na
wanawake wenye umri mkubwa wasitawale mijadala. Tunapokua tunahamasisha watu
kushiriki kwa bidii kwenye mikutano, kumbuka kwamba watu hawalazimiki kushiriki
, lakini wanapaswa kupewa fursa kushiriki iwapo wanataka.
Kuhakikisha kuwa watu wanapata fursa hii, himiza kikundi kujadili na
kukubaliana juu ya kanuni za kuongoza
mikutano. Miongoni mwa kanuni hizi iwe
kanuni kwamba kila mtu ana haki ya
kushiriki na kushikilizwa. Himiza wanakikundi kuzingatia kanuni ambazo wamejiwekea na kuweka mazingira salama kwa ajili ya
mikutano.
Kanuni
za msingi zinaweza kujumwisha, kwa mfano:
·
Kuheshimu mawazo ya kila mshiriki .
·
Washiriki
kuwashirikisha wanakikundi wengine
taarifa zinazostahili walizonazo.
·
Mikutano itaanza na kumalizika kwa muda
uliopangwa na itaanza kwa muda baada ya mapumziko.
·
Kutakuwa na mjadala mmoja kwa wakati mmoja (isipokuwa
kama kuna kazi ambazo zinafanyika katika vikundi vidogo).
·
Kikundi chenyewe,(siyo Mradi wa Tushikamane),ndiyo kinawajibika kutoa matunda -kuonesha matokeo.
·
Mijadala na ukosoaji ilenge masilahi ya kikundi na siyo watu.
Usijilimbikizie madaraka makubwa na kukitawala kikundi !
Miongoni
mwa matatizo magumu sana ambayo yanaweza kukukabili kama Mwezeshaji ni kusawishika
kutawala mijadala au kuubadili mchakato wa kikundi. Mara nyingi jambo hili hutokana na nia nzuri
ya kutaka kukisaidia kikundi kusonga mbele. Kama umezoea mtindo wa ufundishaji wa
kutoka juu kwenda chini, na hujawahi kupata fursa ya kuwangalia wawezeshaji
wazuri wakifanya kazi, inaweza kuwa vigumu kubadili mtazamo wako juu ya ubadilishanaji
mawazo.
Njia
mojawapo ya kukitia moyo kikundi kuchukua usukani wa juhudi zao za kujifunza na
maendeleo ni kukiomba kikundi kutayarisha kanuni za msingi za ushiriki wao ili kila mtu ajisikie huru kutoa
mawazo yake. Kanuni kama hizo zinaweza kujumuisha kutoingilia kati mtu
anapokua anachangia, kuheshimu mawazo tofauti, na kukubaliana idadi ya juu ya pointi ambazo mtu anaweza kuchangia
katika mjadala mmoja. Kama kikundi kitaandika kanuni hizi, wanakikundi wote kwa
pamoja watajisikia kuzimiliki na hivyo
kuhakikisha zinaheshimiwa.
Njia
zingine za kuepuka kutawala kikundi ni
pamoja na:
·
Kuwa na subira
·
Kuwasikiliza wengine na
kuonesha maoni yao yanathaminiwa.
·
Kuwa muwazi katika kujifunza kutoka kwa wanakikundi wengine ili ubadilishanaji wa taarifa utoke pande zote na kwenda pande zote.
·
Kutia moyo kikundi kuibua njia za
ufumbuzi wao wenyewe
Kukabiliana na maswali magumu
Kuweza kuyajibu maswali yote
kutoka kwa washiriki inaweza kuwa kazi
ngumu. Mara nyingi unaweza kujisikia
kuwa unapaswa kuwa na majibu yote. Unaweza kuwa huamini uwezo wako katika
kujibu maswali juu ya mada fulani. Ni wajibu wa Msimamizi na Kiongozi wa Mradi
kukusaidia juu ya jambo hili, na kukusaidia kupata taarifa zaidi, mathalan
kutoka machapisho mbalimbali, serikalini au kutoka ofisi za Mashirika yasiyo ya
Kiserikali nk. Wanaweza pia kukusaidia
kujifunza kutoka kwa watu wenye hekima
na maarifa katika jamii husika, nje ya kundi lako,ambao wanaweza kuwa na
utaalam juu ya mada inayojadiliwa.
Njia zingine za kushughulikia
maswali magumu ni pamoja na:
·
Kujiandaa vizuri kwa ajili ya mijadala ya vikundi kwa kusoma kiongozi hiki na
nyenzo zingine zinazofaa.
·
Hasa, unatakiwa kuwa na uelewa mpana
wa mambo yanayochangia vifo na magonjwa
kwa wajawazito na watoto wachanga.
·
Kutarajia maswali kutoka kwa
wanakikundi na kila inapowezekana kufikiria mapema jinsi ya kuitikia.
·
Kama huna jibu kwa swali, usiogope
kusema hujui ! Kwa swali kama hilo, sema
utatafuta taarifa zaidi na kuwashirikisha wanakikundi pale jibu
litakapopatikana.
Kusimamia migogoro
Wakati mwingine watu wanaweza
kuwa na tofauti kubwa juu ya jambo. Mivutano ndani ya kikundi inaweza
kuathiri utendaji
na umoja wa kikundi kwa ujumla. Unatakiwa
kuwa makini katika kutambua mivutano ambayo inaweza kutokea na kuwatia moyo
wanakikundi kwa pamoja kuangalia zaidi ya
mivutano hii, wakiweka malengo na maslahi ya watu wote kwanza. Kama
tofauti haihusu mada ambayo inajadiliwa, utahitaji kuwasihi kuweka tofauti hiyo pembeni.
Kanuni za msingi katika usimamizi
wa migogoro ni pamoja na:
·
Kutambua na kukubali uwepo wa mgogoro huo.
·
Jaribu
kubaini chanzo cha mgogoro huo.
·
Kama unahusiana na mada
inayojadiliwa, wasaidie washiriki kufikia makubaliano, ukiwatia moyo
kuheshimiana.
·
Kama mgogoro hauhusu mada
inayojadiliwa, na unahusisha tu baadhi ya wanakikundi, watie moyo kusuluhisha
tofauti hii baadaye, nje ya mazingira ya kikundi.
Kukabiliana na washiriki wanaopenda
kutawala mijadala
Wakati mwingine, mtu mmoja
anaweza kuanza kuutawala mjadala, akionekana kujiamini kuwa anayo majibu sahihi kwa mswali yote. Kama hali hii itajitokeza, unahitaji kuhakikisha kuwa
watu wengine pia wanapata fursa ya kuchangia . Njia ya kuliwezesha hili ni
pamoja na:
·
Kuwaita wengine kwa majina yao
ili nao watoe maoni
·
Gawa kikundi katika vikundi vidogo kadhaa.
·
Anzisha mfumo wa mgao, ambapo
kila mtu atapewa vijiwe 3 au vipande vya karatasi 3, na wanatakiwa kusalimisha
kimoja kila mara watakapoongea. Watakapoishiwa, hawataweza kuongea tena!
·
Anzisha mfumo wa kuweka muda ambao mtu hatakiwi kuuvuka anapochangia. Kila
mtu anaweza kuongea kwa muda usiozidi dakika moja kwa wakati. Muda huo
unapofika anatakiwa kutoa nafasi kwa
mwanakikundi mwingine kuongea.
·
Tumia ‘fimbo inayoongea’. Yeyote
atakapokuwa ameshika fimbo hiyo ndiyo yeye peke anayeruhusiwa kuongea.
Atakapomaliza kutoa mawazo yake, atakabidhi fimbo kwa mtu mwingine ambaye anataka kuchangia. Watakapomaliza kutoa mawazo yao, watakabidhi fimbo kwa mwingine ambaye angependa kuongea.
·
Kaa karibu na mtu ambaye anaongea
sana, siyo kwa kuangaliana! Ukikaa kwa kuangaliana na mtu mwingine, hasa mtu
ambaye anapenda sana kutawala mijadala, unajikuta unamuangalia sana, na yeye
huhisi kuwa unaongea naye mahsusi.
Kufanya kazi na watu wenye aibu
Wakati mwingine watu wanaweza
kuona aibu au kuogopa kutoa maoni yao mbele ya kikundi. Hii, hasa, inaweza kuwa
ngumu zaidi mnapokua mnajadili masuala ya afya ya akinamama na watoto wachanga
kwa sababu baadhi ya wanawake na wasichana balehe hupata tabu kujieleza mbele
ya watu wengine, hususan kama ni wanafamilia wenzao. Njia moja wapo y ya
kuwatia moyo watu wenye aibu au waoga ni kurejea na kutumia mawazo yao
waliyoyatoa huko nyuma, ili wajue kuwa ni muhimu na yanathaminiwa.
Pia, unaweza :
·
Kuomba watu kuyajadili maswali
kwanza wakiwa wawili wawili.
·
Tumia njia za vitendo kama vile watu kuchora ramani au picha za mawazo yao na kuzihusianisha
na picha za mawazo ya watu wengine, kupanga vitu au masuala husika na kuyapa namba kwa
kutanguliza yaliyo muhimu zaidi, na kuandaa ratiba inayruhusu washiriki kutoa maoni yao.
·
Kuongea na watu wenye aibu peke
yao pembeni baada ya mkutano ili kupata mawazo na mchango wao.
·
Kuwatia moyo mmoja mmoja, ndani
na nje ya kikundi
·
Kuongea nao nje ya kikundi, na
kutafuta sababu za ukimya wao.
·
Kutoa taarifa juu ya mada
itakayojadiliwa mapema ili wapate muda wa kujiandaa.
·
Mpe mtu mwenye aibu mwenye uwezo wajibu wa kutunza kumbukumbu na kutoa mrejesho.
·
Wape muda- wanaweza kuzoea na
aibu kupungua.
·
Tumia igizo dhima kuwajengea moyo
wa kujiamini na stadi mbalimbali zikiwemo za mawasiliano.
Hasa katika hali ngumu, inaweza
kuhitaji kuunda vikundi tofauti vya kujifunza na utendaji shirikishi(PLA groups)kwa
ajili ya makundi tofauti yaliyopo ndani ya jamii. Kwa mfano, kikundi mahsusi kwa
ajili ya wanawake walio katika umri wa uzazi na kingine kwa ajili ya wasichana balehe. Uamuzi
huo utasababisha ongezeko la kazi kwako.Hivyo, uamuzi huo unatakiwa kuchukuliwa
tu baada ya kutafakari kwa makini na baada ya njia zingine zilizopendekezwa
kujaribiwa na kushindwa.
MZUNGUKO WA MIKUTANO YA VIKUNDI VYA TUSHIKAMANE
Awamu na
Mikutano
Mzunguko wa vikundi vya Tushikamane una awamu 4 na jumla ya mikutano
14 :
Awamu ya 1:
Mkutano wa 1: Kuunda kikundi – Kitongoji kizima kikutane
kuanzisha mchakato
(Kutoka hatua hii, kwa
Awamu ya 1 na ya 2, Kikundi cha Tushikamane kitakuwa na wanawake tu!)
Mkutano wa 2: Wanawake kubainisha matatizo ya afya ya wanawake.
Mkutano wa 3: Wanawake kubainisha matatizo ya afya ya
watoto wachanga
Mkutano wa 4: Wanawake kuainisha
matatizo yatakayopewa kipaumbele
Mkutano wa 5: Wanawake kubainisha
mambo yanayochangia matatizo ya afya ya wanawake na watoto wachanga
Awamu ya 2:
Mkutano wa 6: Wanawake kubainisha shughuli za uzuiaji na
usimamizi wa matatizo ya afya ya wanawake na watoto wachanga
Mkutano wa 7: Wanawake kujadili mipango ya kutatua matatizo yaliyoainishwa.
Mkutano wa 8: Wanawake kuwasilisha taarifa za
maendeleo kwa jamii nzima
Awamu ya 3:
Mkutano wa 9: Kupanga ufumbuzi – katika hatua hii wanaume
na wahusika wengine muhimu wanaweza kujiunga na kikundi
Mkutano
wa 10: Kutafuta rasilimali, halafu kuzikusanya
Mkutano
wa 11: Kuandaa zana za ufuatiliaji
Katika hatua hii, jamii
itaanza utekelezaji wa njia za ufumbuzi walizozichagua,
(kwa msaada wowote
watakaoweza kupata ili kuongeza
uwezekano wa mafanikio).
Awamu ya 4:
Mkutano
wa 12: Kuandaa zoezi la kutathmini
matokeo ya mchakato wa vikundi vya Tushikamane
Mkutano
wa 13: Kukusanya taarifa kwa ajili ya
tathmini, halafu kujadili matokeo ya Mradi juu ya afya ya wanawake na watoto
wachanga
Mkutano
wa 14: Kupanga kwa ajili ya siku zijazo
– kwa mfano, jamii inaweza kutaka
kuurudia tena mchakato huo!
RIPOTI
Ripoti ya mkutano
Unapaswa kuandaa ripoti ya
mkutano kila baada ya mkutano kufanyika. Hii itachangia ripoti yako ya kila mwezi. Katika
maelezo yafuatayo ya kila mkutano, kuna vipengele ambavyo ripoti yako inapaswa
kuzingatia.
Ripoti ya mwezi
Ripoti yako ya kila mwezi
inapaswa kuwasilishwa kwa Msimamizi kila mwisho wa mwezi. Taarifa zinapaswa
kukusanywa kutoka kwenye kumbukumbu zako
za mwezeshaji, sajala ya kikundi na ripoti za mikutano.
Unapaswa kuandaa ripoti yako ya
mwezi kwa kila kitongoji unapofanyia kazi. Masuala muhimu ambayo unatakiwa kuelezea
ni pamoja na:
·
Idadi ya mikutano iliyofanyika
·
Mahudhurio katika mikutano (idadi inapaswa kuwa kati ya 10 na 30).
·
Kuna wajawazito wangapi kwenye kikundi
? Je mmeweza kuwafikia wanawake walio kwenye umri wa uzazi, hasa wajawazito na
wanawake ambao ndio wamejifungua mara ya kwanza, pamoja na wanawake ambao
wameolewa hivi karibuni na wasichana balehe. Je, wanawake wenye hadi duni na
walio pembezoni au ambao wametengwa kwa vigezo mbalimbali wamehimizwa kujiunga
na kikundi ?
·
Ni wanajamii gani wengine
wameweza kuhudhuria ?
·
Je kuna wajumbe wa kamati ya
kikundi ambao wamejitoa na hivyo kuwepo
haja ya kuchagua wengine na kutoa mafunzo wa wanakikundi wapya ?
·
Je kikundi kinaendelea vuzuri
kulingana na ratiba katika kukamilisha mzunguko mzima wa mikutano katika
kipindi cha miezi 12 hadi 24 ?
·
Zana na njia ambazo
zinatumika kuviwezesha vikundi zinakubalika na zinawafaa wanakikundii?
·
Muda na sehemu
mikutano ya vikundi inapofanyikia zinafikika kwa urahisi na wanakikundi
wanaotaka kuhudhuria?
·
Rasilimali zilizopo
kwa vikundi zinatosheleza kwa ajili ya
utekelezaji wa shughuli zao kwa mafanikio?
·
Je masuala yanayojadiliwa kwenye mikutano yanalingana na matarajio? Kwa mfano, wanabainisha matatizo
yanayotarajiwa? Je, wanapanga kutekeleza
shughuli za ufumbuzi unaotarajiwa?
Kusambaza taarifa
Kati ya mikutano, unapaswa
kuitembelea jamii, kwa lengo la kukutana
na watu ambao hawajashiriki, na pia kuwahimiza wanakikundi kuwashirikisha wenzao ambao wanashindwa kuhudhuria
juu ya masuala yanayojadiliwa kwenye
mikutano.
AWAMU
YA 1: KUBAINISHA MATATIZO PAMOJA
Dhumuni la Awamu ya 1
Shabaha ya awamu ya kwanza ya mzunguko wa mikutano
ni vikundi kubainisha matatizo ya akinamama na watoto wachanga na vipaumbele.
Awamu ya kwanza ina mikutano 5,ambayo hufanyika kwa
utaratibu ufuatao:
·
Mkutano wa 1: Kuunda kikundi
·
Mkutano wa 2: Kubainisha matatizo ya afya ya akinamama
·
Mkutano wa 3: Kubainisha matatizo ya afya ya watoto
wachanga
·
Mkutano wa 4: Kuainisha matatizo gani ya afya ya
akinamama na watoto wachanga yatakayopewa kipaumbele.
·
Mkutano wa 5: Kubainisha mambo yanayochangia matatizo
hayo
MKUTANO WA 1: KITONGOJI KUKUTANA KUUNDA KIKUNDI
Nani
anapaswa kuhudhuria mkutano wa 1?
Kabla
mchakato wa Tushikamane haujafikia hatua
ya kuunda vikundi ndani ya kitongoji, kunahitajika kuwepo mkutano wa wadau wote ambao wanastahili kushiriki katika mchakato
huo katika kitongoji husika.
Wadau hao ni pamoja na:
•
Wanawake vijana na akinamama na wajawazito– hususan
wale ambao wanatoka kwenye familia ambazo zimewahi kumpoteza mama kutokana na
matatizo ya uzazi, au kumpoteza mtoto
mchanga
•
Wanawake wenye
‘sauti’ ya nguvu ndani ya kitongoji – mathalan waalimu, wanawake katika nafasi za uongozi, na pia wanawake wenye
vipaji vya kuzaliwa vya uongozi.
•
Viongozi wa
kiutamaduni na viongozi wa kuchaguliwa katika kitongoji
•
Viongozi wa dini
•
Wafanyakazi wa
afya vijijini
•
Wataalam wa tiba
za jadi
Mitandao ya
vikundi vya kijamii, au mashirika yasiyo ya kiserikali au asasi zingine ambazo zinafanya kazi katika kitongoji husika
nk.
Ufafanuzi
juu ya mkutano wa kwanza wa kitongoji
Mkutano
huu wa kwanza wa kitongoji unaweza
kuchukua saa 2. Mkutano unapaswa kufanyika sehemu iliyo kati na yenye nafasi ya
kutosha kwa ajili ya watu wote.
Dhumuni
la mkutano ni kupata azmai na ushirikiano wa
watu watakaohudhuria juu ya
mchakato wa Tushikamane.
Hii
itahitaji kuanza kwa kueleza Tushikamane inahusu nini: kuwapa wanawake – hususan
wanawake walio kwenye umri wa uzazi, sauti katika kujadili jinsi ya kupunguza
vifo vya akinamama na watoto wao wachanga. Hii itapelekea, hatimaye, kupanga
pamoja na kitongoji kizima mambo ambayo
yanapaswa kushughulikiwa, na namna gani.
Matarajio ni kwamba yataibuliwa mawazo mazuri, pamoja na vipaumbele vya
kufanyia kazi ambavyo vitaivuta jamii nzima kufanya kazi pamoja ili kupunguza
vifo hivyo vya kusikitisha. Wanapaswa kutambua kuwa kwa kufanya hivyo, manufaa
mengi zaidi yataanza kuonekana ndani ya jamii.
Hii ni njia bora zaidi ya kufanya kazi kuliko wageni
kuja na kufanya mambo ambayo huenda hayaafikiwi na watu wote; ambayo yanaweza kusababisha
mgawanyiko, kukosa kuungwa mkono na jamii au kuwa endelevu, au ambayo
hayakabiliani ipasavyo na mizizi halisi
ya vifo hivyo vya kusikitisha.
Mambo
ambayo yanaweza kujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na:
·
Madhara
na athari kwa jamii kutokana na kifo cha mama.
·
Watu waliohudhuria
wana raslimali, lakini wanahitaji
kufanya kazi pamoja ili waweze kuvutia misaada kutoka nje inayolenga matatizo
yao halisi.
·
Watu
waliohudhuria hawapaswi kuogopa kutenga muda wao ili kujishughulisha na kikundi.
·
Mchango
wao kwa ujumla na uongozi bora vitakuwa vigezo muhimu katika kuleta mafanikio.
·
Mchango
wao na ushirikiano wao wakati wa kukazia
au kuzamisha ufumbuzi ndani ya jamii vitakuwa vigezo muhimu, siyo
tu kuhakikisha mafanikio bali pia uendelevu.
Mafanikio endelevu yatakapobainika kwa
wakala wa nje, kutakuwa na uwezekano
mkubwa wa kutoa misaada zaidi siku zijazo kwa jamii ambayo imejiwekea ajenda
yake ya maendeleo, na inafanya bidii
kukamilisha utekelezaji wa shughuli za kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.
Hawahitaji
kuahidi chochote katika hatua hii, lakini wanapaswa kuelewa kwamba kuna wakati wanaweza kutafutwa kuombwa kuunga mkono mradi kwa hali na mali.
Ajenda ya mkutano wa kwanza wa kitongoji
Ajenda iliyopendekezwa kwa ajili ya mkutano huo ni
kama ifuatayo:
1.
Makaribisho-kufanywa na Mwenyekiti wa Mradi, Mchungaji
Mgego
2.
Utambulisho-kufanywa na Kiongozi wa Mradi,
Wilbard Mrase
3.
Malengo ya mkutano-kuelezwa na Msimamizi wa Mradi, Alex Gongwe
4.
Mada ya dakika 20 juu ya programu ya Tushikamane -kuwasilishwa na Mwezeshaji wa
Mradi – Esther Paul au Rehema Semwali
(Wakati
wa zoezi hili, unapaswa kueleza kuwa wakati wa mzunguko wa mikutano, kila mtu
atashiriki kwa usawa, na wanaume na wanawake wenye umri mkubwa zaidi wasitawale
majadiliano. Ili kuruhusu wanawake washiriki kikamilifu, wawezeshaji wanaweza
kuwaomba wanaume kuchangia mwishoni baada ya kikundi kukamilisha mijadala
ya mkutano. Pia eleza kuwa wafanyakazi
wa afya kwenye jamii na maafisa wengine wa afya na serikali za mitaa
na vijiji wataalikwa kwenye mikutano na kupewa
muda na nafasi ya kuongea na wanakikundi.)
5. Maswali,
maoni na mawazo kutoka kwa wasikilizaji;
(Baada
ya mada kuwasilishwa, washiriki wanapaswa kupewa muda mzuri kwa ajili ya
maswali na majibu juu ya masuala mbalimbali yaliyowasilishwa. Mkutano pia
ujadili jinsi gani washiriki
watakavyoweza kuusaida mradi kama wataombwa kufanya hivyo – mathalan ,kutoa
ushauri jinsi ya kuboresha hali ya usafi
wa mwili na mazingira kijijini, ushauri juu ya ya kuinua kilimo cha mashamba
madogo madogo au jinsi ya kukabiliana na mahitaji mbalimbali kutoka kwa jamii .)
6. Njia za ufumbuzi ambazo vikundi vya Tushikamane vingependa kutekeleza;
(Kutokana
na uzoefu, njia za kawaida za ufumbuzi
ambazo zimebainishwa na kutekelezwa na makundi ni pamoja na : kutoa elimu ya
afya; huduma ya usafiri; kuanzisha mfuko wa kikundi; kuhimiza vifaa safi kwa
ajili ya kujifungua; kuhimiza shughuli za uzalishaji pato; kushughulikia
mahitaji ya wakunga wa jadi yakiwemo mafunzo; kuimarisha ushirikiano na ushawishi
wa vituo vya afya; kuhimiza kilimo cha bustani za mbogamboga; kuhimiza matumizi
ya viandarua vya kuzuia mbu na usambazaji wake.)
7.Majadiliano jinsi gani washiriki wanaweza kuusaidia mradi
8. Kuongoza
uundaji wa kikundi
(Kamati
ndogo ya uongozi inapaswa kuundwa kutokana na washiriki kwenye mkutano. Jukumu
la kamati hii ni kumsaidia Mwezeshaji na
kumpatia ushauri atakapokuwa anatekeleza programu ya Tushikamane.
Mwezeshaji atakutana na kamati ya uongozi mara kwa mara ili kutoa
mrejesho na kupata msaada na ushauri. Wakati mwingine Msimamizi, Alex Gongwe, atahudhuria
mikutano ya Kamati Ndogo ya Uongozi. Kunatakiwa kuwepo Kamati Ndogo ya Uongozi
moja tu katika kila kitongoji – kamati moja kwa kila kikundi cha Tushikamane.)
9.
Majumlisho—kufanywa na Wilbard Mrase
10. Ufungaji
wa mkutano -kutolewa na Mchungaji Mgego
11.
Kufunga.
Kubainisha huduma ambazo programu
ya Tushikamane itatoa - na ambazo
haitatoa
Kabla mkutano haujaisha, na mchakato wa Tushikamane kuanza
rasmi, kunahitajika kuwepo uelewa bayana kwenye jamii juu ya huduma ambazo
programu ya Tushikamane itatoa na ambazo
haitatoa :
Huduma ambazo zitatolewa kwa kila kitongoji:
·
Mwezeshaji aliyepitia mafunzo atawezesha
uanzishaji wa kikundi cha Tushikamane na
kuongoza mikutano ya Kikundi.
·
Msimamizi ambaye atamsaidia Mwezeshaji
kufanikisha shughuli za Kikundi.
·
Mara
mchakato utakapofikia kiwango cha kitongoji kuwa kimefanya uchambuzi wa
matatizo ya msingi ambayo yanasababisha vifo vya mama na watoto wachanga, na
kimeweka vipaumbele ambavyo vinapaswa kufanyiwa kazi ili kupunguza matatizo
hayo, programu ya Tushikamane itajaribu
kusaidia kukiunganisha kitongoji na wadau wengine ambao wanaweza kusaidia. Mathalan,
vitongoji vingine ambavyo vinapambana na matatizo kama hayo; juhudi au programu
zingine zinazostahili, au na mashirika
mengine ya misaada yenye dhamira ya kusaidia juhudi kama hizo ambazo zimepangwa na Kikundi cha Tushikamane.
Mifano
Kwa
mfano, kitongoji kinaweza kuweka kipaumbele juu ya ufumbuzi wa tatizo la
usafiri ili kusaidia kuwafikisha
wajawazito hospitalini haraka. Huenda
vitongoji vingine pia vimeweka kipaumbele juu ya suala la usafiri. Programu ya Tushikamane
inaweza kusaidia kuziunganisha jamii hizo na shirika la misaada lenye uwezo wa kutoa pikipiki maalum
ya kubeba wagonjwa, mara shirika hilo
litakapojihakikishia kuwepo huduma za matunzo ya kifaa hicho na hata mtu wa kukiedesha
kitongojini hapo.
Mifano
mingine ni pamoja na:
·
Kuwaongezea
stadi za utendaji – mfano kuanzisha
programu endelevu ya mafunzo kwa wakunga
wa jadi.
·
Huduma
za afya – mfano kuanzisha huduma za chanjo zinazopatikana kwa urahisi, huduma ya kupima
msukumo wa damu(presha), kutibu anemia, nk;
au kuisaidia jamii kukubali uzazi wa
mpango, na kutoa huduma husika.
·
Kilimo
na chakula – mathalan kuanzisha na kupanua huduma za ziada za lishe kwa ajili ya watoto wanaolikizwa.
·
Elimu – mathalan
kuboresha elimu kwa akinamama juu ya afya wakati wa ujauzito.
·
Afya
ya mazingira na usafi wa mazingira hususan huduma ya vyoo – mathalan kufanya
kazi pamoja katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama.
Programu ya
TUSHIKAMANE haitatoa huduma zifuatazo:
·
Misaada
ya kifedha au posho za aina yote kutoka kwa timu ya Tushikamane yenyewe.
·
Bakshishi
·
Kuwafanyia
wanajamii kazi mbalimbali bila wao
wenyewe kushiriki. Msaada wowote utakaotolewa utategemea
juhudi za jamii yenyewe kujitegemea, na ushiriki wake. Misaada haitategemea fikra
za wageni juu ya mahitaji ya jamii. Misaada ‘haitabwagwa’ tu kwenye kitongoji.
Kuunda kamati ya uongozi
Kamati ya uongozi itasaidia kuifanya
kazi yako kuwa rahisi zaidi, na kuimarisha uwezo wa jamii kujiamulia. Unapaswa kusaidia
kikundi kuunda kamati ya uongozi mwishoni wa mkutano wa kwanza. Kamati hiyo, kwa msaada
wako, itasaidia kuendesha shughuli za kikundi.
Kamati
inapaswa angalau kuwa na mwenyekiti na katibu. Baada ya hapo, wanaweza kuhitaji
mweka hazina. Kadri muda unavyokwenda, kamati itaendelea kuongezewa wajumbe
hadi kufikia wajumbe 5 hadi 10 watakaoendesha
kikundi na kufanikisha shughuli zake. Kwenye kamati, wawepo wanaume, lakini
wasizidi 2 katika kamati ndogo, au 3 katika kamati kubwa.
Jukumu
la mwenyekiti ni kuongoza kikundi, na huyu anapaswa kuwa mwanamke.
Jukumu la mwenyekiti linajumuisha kutoa mwongozo na dira, kusimamia
wajumbe wa kamati na wanakikundi, na kukiwakilisha kikundi katika majukwaa ya
kijamii, kiwilaya na kitaifa.
Jukumu
la katibu ni kutunza kumbukumbu za shughuli zote za kikundi. Jukumu hili
linajumuisha kujaza rejesta ya kikundi
baada ya kila mkutano.
Jukumu
la mweka hazina ni kufuatilia fedha za kikundi na rasilimali zingine za
kikundi.
Jukumu
la wajumbe wote wa kamati ni kushawishi wanajamii kujiunga na kikundi na
kushiriki katika mikutano.Wahimize wanakikundi kujadili na kuchagua wajumbe wa
kamati kwa kupendekeza na kuunga mkono pale
mjumbe aliyependekezwa anaoonekana anafaa.
Kimsingi,
wajumbe wa kamati wanapaswa kuwa na uzoefu na /au stadi za uongozi. Watabeba
wajibu wa kuhakikisha shughuli za
kikundi zinatekelezwa, kutatua migogoro au tofauti na kukipa dira kikundi. Wataweza mkazo katika kutekeleza shughuli mbalimbali
kwa maslahi ya kikundi, siyo kwa maslahi binafsi.
Watakusaidia
kutimiza majukumu yako. Kadri kikundi
kitakavyoendelea na shughuli zake, wajumbe wa kamati wanaweza pia kusaidia uwezeshaji
wa baadhi ya mikutano kama unakuwa hupo.
Masuala ya
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 1
·
Rejesta inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wajumbe wangapi
walihudhuria,wanawake walikua wangapi, wangapi walikua na ujauzito?
·
Mkutano uliendeleaje – mafanikio
yoyote au matatizo?
·
Wajumbe
wa kamati ya uongozi ni nani ?
·
Ni
kanuni gani ambazo zimewekwa kwa ajili ya uendeshaji wa mikutano?
Nini kifanyike
baada ya mkutano wa kwanza
Unapaswa
kuwaorodhesha wote waliohudhuria katika
rejesta ya kikundi. Yote yakienda
vizuri, kuanzia mkutano unaofuata hii itakuwa kazi ya katibu ambaye
atachuguliwa wakati wa mkutano huu.
MKUTANO WA 2 – WANAWAKE VIJANA (WENYE UMRI MDOGO) KUBAINI MATATIZO YA AFYA YA AKINAMAMA
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 2?
Mchakato wa Tushikamane unahusu kuzuia vifo vya kusikitisha vya wanawake
na watoto wachanga, hasusan vinavyohusiana na uzazi. Hivyo, wanawake walio katika
umri wa uzazi wanapaswa kuwa ndiyo washiriki wakuu wa mkutano huu wa 2, ili waweze kuanza kubainisha matatizo ya
msingi yanayosababisha vifo hivyo.
Uanachama katika kikundi
utaamuliwa na wanawake hao wenyewe. Hata hivyo,wanapaswa kuhimizwa kuwapa kipaumbele
wajawazito na akinamama ambao ndiyo wameanza uzazi, pamoja na wanawake ambao
wameolewa hivi karibuni na wasichana balehe.
Wanapaswa pia kukumbushwa kuhakikisha kuwa wanawake wenye hali duni na ambao
wametengwa kwa vigezo mbalimbali wanaalikwa
kuhudhuria.
Wakunga wa Jadi, kwa umuhimu wa pekee, wanapaswa kualikwa kuwa sehemu ya
mchakato huu kuanzia mwanzoni.
Kama Mfanyakazi wa Afya Kiijijini ni mwanamke na anajiona sehemu ya
jamii, basi naye anapaswa kuhudhuria. Kama
mfanyakazi huyu, mathalan, ni mwanaume mwenye umri mkubwa ambaye haishi kwenye
kitongoji husika, basi wanawake wanaweza kupenda kumshirikisha kwenye mchakato
baadaye.
Hata hivyo, ni muhimu kulegeza masharti ya uanachama kwenye kikundi, mathalan, kuwaruhusu
wanawake maarufu wenye umri mkubwa, na
viongozi wa dini ambao wanaweza kushawishi jamii kuviunga mkono
vikundi vya Tushikamane na
shughuli zake.
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 2
Tembelea
watu maarufu kwenye kitongoji waliohudhuria mkutano wa 1. Wafanye wajisikie ni jambo muhimu
kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika
umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na
watoto wachanga.
Kadri
mkutano utakapokaribia, wakumbushe watu tarehe na muda wa mkutano, na mahali
utakapofanyika, na kuwahimiza kuhudhuria. Kwa kuwa ni vigumu kutunza muda,
chagua muda mwafaka, ili kuwarahisishia
wanawake kuhudhuria.
Ajenda ya Mkutano wa 2
1. Makaribisho;
utambulisho; na kupitia mhutasari wa kikao kilichopita.
2.
Kukubaliana ni katika hatua gani
wanawake wangehitaji wanaume na watu wengine maarufu kwenye kitongoji kujiunga
na mchakato huo. Muda utakaopendekezwa kuwashirikisha watu hao uwe baada ya
Mkutano wa 8. Kabla ya hapo, wanawake watakuwa wanajadili
masuala ya ndani ya kike, na pia wakijaribu kutafuta ufumbuzi unaowezekana
miongoni mwao, pasipo mijadala hiyo
kugubikwa na wingu wa wanaume.
Mkutano wa 8 ndiyo mkutano mahali ambapo mrejesho juu ya maendeleo wa mchakato
hutolewa kwa jamii. Baada ya hapo, ni jambo zuri kupanua wigo wa kikundi na
kuwaingiza watu wengine ambao wanaweza kuchangia kupunguza matukio ya vifo vya
mama wakati wa kujifungua, na kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Baada ya hapo, kikundi kitahitaji kuzingatia mila na desturi; lakini mikutano inaweza kuwahusisha pia wafanyakazi
wa afya vijijini au aina yoyote ile ya wafanyakazi wa afya; viongozi
wa jamii; waalimu; wenzi wa wanawake au wasichana balehe kwenye kikundi;
wafanyakazi wa serikali au mashirika ya misaada; na yeyote ambaye angependa
kuchangia kuboresha afya ya mama na watoto.
3. Kuwasilisha
malengo ya mkutano:
·
Kujadili hali halisi ya matunzo ya mama nyumbani kuhusiana na uzazi na akinamama huwa wanafanya
nini wanapohitaji huduma zingine za afya.
·
Kubainisha matatizo ya afya
yanayowakabili wanawake wakati wa ujauzito, wanapojifungua, na baada ya
kujifungua.
4. Kujadili
namna akinamama hujipanga kwa ajili ya
ujauzito wao na kujifungua - ni wakati gani na katika mazingira gani huamua kutafuta huduma na misaada ya kiafya. Pia
mkutano utajadili ni katika mazingira
gani wanapojifungulia nyumbani.
5. Kujadili
umuhimu wa kubainisha matatizo – Wakumbushe wanawake kwamba ni muhimu
kubainisha matatizo yanayowakumba akinamama kuhusiana na uzazi na watoto wachanga kwa sababu:
·
Wanawake
wengi huugua na kufariki kila mwaka kuhusiana na uzazi, na baadhi ya vifo hivi
vinaweza kuzuiwa na jamii zao.
·
Matatizo
ya afya yanapaswa kubainishwa kabla ufumbuzi haujatafutwa
·
Wanajamii,
hususan wanawake, na wana haki na wapo katika nafasi nzuri zaidi
kubainisha matatizo ya afya yanayowaathiri (ingawa wanaume pia wana wajibu muhimu na
wanapaswa kusikilizwa na hata kushirikishwa katika mipango hiyo).
6. Kuongeza
uelewa juu ya matatizo muhimu ya afya ya mama na watoto wachanga ambayo
huwakabili akinamama wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua, na baada ya
kujifungua na njia muhimu za kupunguza matatizo hayo. Tumia kadi za picha za
matatizo kusaidia(Matatizo makuu ni kutokwa damu nyingi; mtoto kushindwa kupita
kwenye mfupa wa pango la nyonga wakati wakuzaliwa; kondo la nyuma kuchelewa
kutoka baada ya mtoto kuzaliwa; malaria; anemia ambayo huzidisha matatizo
mengine; na mkao mbaya wa mtoto katika tumbo la uzazi wakati wa uchungu wa
uzazi.)
7.
Shughuli
kuu za mkutano: Wezesha wanawake katika kikundi hicho kubainisha matatizo
ambayo yanawaathiri wanawake katika jamii hiyo wakati wa ujauzito, wakati wa
kujifungua, na baada ya kujifungua. Mara
hii tena, tumia kadi za picha za matatizo.
8. Toa
majumlisho ya mkutano na chunguza iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya
nini katika mkutano ujao?
9. Karibisha
maswali.
10. Panga tarehe ya mkutano ujao.
Jinsi ya
kuwezesha mjadala juu ya matatizo ya afya ya akinamama
Taarifa kuhusiana na matatizo ya afya ya akinamama zinaweza
kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vikiwemo: uzoefu binafsi na shuhuda; vifaa vya
kampeni za afya kwa umma; vituo vya kutolea huduma za afya;na kutoka watu
tofauti mathalan wanume na wanawake kitongojini, wakunga wa jadi, wafanyakazi
wa afya vijijini, na watalaam wa afya wengine.
Eleza kwamba matatizo ya afya yanayolengwa ni yale
yanayowaathiri wanawake na watoto wachanga na kusababisha kuugua au hata vifo. Inaweza
kuwa rahisi kuyajadili matatizo hayo kwa kufikiria zile hatua 4 ambapo matatizo hayo kujitokeza: wakati wa
ujauzito, mara baada ya kujifungua na hadi mwezi 1 baada ya mtoto kuzaliwa.
Hivyo unaweza kuanza kwa kukiuliza kikundi juu ya matatizo ambayo hujitokeza kabla ya
kujifungua. Tumia kadi za picha za matatizo kuibua mawazo. Tunza kumbukumbu ya mambo
muhimu kutokana na mjadala.
Kumbuka, hakuna majibu yasiyo sahihi. Kikundi
kinapaswa kuhimizwa kuorodhesha matatizo yote ya afya watakayofikiria. Baadhi
ya matatizo yamejificha, yakiwemo ukatili wa kingono(ubakaji) na virusi vya UKIMWI(VVU). Wahimize
wanawake binafsi kuomba msaada kama
matatizo ambayo wanataka kueleza yanahitaji faragha.
Baada ya mkutano, kikundi kinaweza kuendelea
kuongeza kwenye orodha matatizo mengine zaidi kadri yatapokuwa yakibainishwa.
Kwa kila tatizo, hakikisha linafafanuliwa kwa
ukamilifu hadi kikundi kiweze kukubali kuwa ni tatizo au la.
Masuala
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 2
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi
walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa na mafanikio au changamoto zozote?
·
Matatizo gani ya afya ya akinamama yalibainishwa?
Nini cha
kufanya baada ya Mkutano wa 2
Makatibu
wanapaswa kuorodhesha washiriki wote
kwenye rejesta ya kikundi.
Unapaswa
kukamilisha ripoti ya mkutano, ikiwa na
kumbukumbu ya matatizo yote yaliyoibuliwa. Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano.
MKUTANO
WA 3 – WANAWAKE VIJANA ( WENYE UMRI
MDOGO) KUBAINISHA MATATIZO YA AFYA KABLA MTOTO HAJAZALIWA
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya mkutano wa 3
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu muhimu kwenye kitongoji ambao
walihudhuria mkutano wa 2. Wafanye
wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu:
kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga namna ya
kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.
Wakumbushe
wanawake kuwa mkutano unaokuja unakusudia kujadili matatizo yanayohusiana na vifo vya watoto.
Mkutano
utapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha wale
walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 3 ?
Wanawake
wote waliohudhuria mkutano wa 2 wanapaswa
kuhudhuria kama wanaweza. Pia, kwa vile sasa wana uelewa zaidi juu ya mchakato
huu, unaweza kushawishi wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa
sana kwenye kitongoji, na wana
uwezo wa kuwashawishi wengine.
Ajenda ya Mkutano wa 3
1. Makaribisho,
utambulisho na mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita.
2. Wasilisha
malengo ya mkutano:
·
Kujadili hali halisi ya matunzo
ya watoto wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, ikijumuisha wakati wanapojifungulia
nyumbani; na mazingira ambamo akinamama hutafuta misaada ya kiafya kwa ajili ya
watoto wao wachanga.
·
Kubainisha
matatizo ya kiafya yanayowakumba watoto
wachanga wakati wa ujauzito, wanapokuwa wanazaliwa na baada ya kuzaliwa.
3.
Kujadili hali halisi ya matunzo
ya watoto wachanga wakati na baada ya kuzaliwa.
4.
Kujadili umuhimu wa kubainisha
matatizo-kumbuka ni muhimu kubainisha matatizo yanayowaathiri mama na watoto
wachanga kwa sababu:
·
Watoto
wengi wanaotoka kuzaliwa huugua na kufariki kila mwaka na baadhi ya vifo hivyo
vinaweza kuzuiwa na jamii zao.
·
Matatizo
ya afya yanahitaji kubainishwa kabla ufumbuzi haujatafutwa.
·
Wanajamii,
hususan, wanawake, wako katika nafasi nzuri zaidi na wana haki ya kubainisha matatizo
yanayowaathiri watoto wao wachanga, (ingawa wanaume nao wana jukumu na
wanapaswa kushirikishwa).
5. Kuongeza
uelewa juu ya matatizo makuu ambayo yanawaathiri watoto wachanga wakati wa
ujauzito, wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, na njia za ufumbuzi.
Tumia kadi za picha za matatizo.
Matatizo makuu ni pamoja na: baridi -watoto wachanga kukosa joto la kutosha; utapiamlo; sepsisi-maambukizi
kutokana na sumu kwenye damu; kifafa cha mimba; matatizo ya
kupumua kwa mtoto mara baada ya kuzaliwa; kuhara; malaria; maambukizi katika
mfumo wa kupumua ; -homa ya manjano; na kuzaliwa
kabla ya kutimiza muda wake.
6.
Shughuli
kuu za mkutano: Wawezeshe wanawake kubainisha matatizo yanayowaathiri watoto
wachanga kwenye jamii wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa, na baada ya kuzaliwa. Tumia kadi za picha za
matatizo.
7. Fanya
majumlisho ya mkutano na kuhakiki iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya
nini katika mkutano ujao?
8. Himiza
washiriki kuuliza maswali.
9.
Panga tarehe ya mkutano ujao.
Masuala
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 3
• Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa
muhtasari: wangapi walihudhuria,
wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
•
Mkutano uliendaje – je kulikuwa na
mafanikio au changamoto zozote?
•
Matatizo gani ya afya ya watoto ambao hawajazaliwa yalibainishwa?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 3
·
Makatibu wanapaswa kuorodhesha waliohudhuria wote kwenye rejesta ya
kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano.
MKUTANO WA 4
– KUAINISHA MATATIZO YATAKAYOPEWA
KIPAUMBELE
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 4
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu muhimu kwenye kitongoji ambao
walihudhuria mkutano wa 3. Wafanye
wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu:
kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya
kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.
Wakumbushe
wanawake kuwa mkutano unaokuja unakusudia kujadili
jinsi ya kuyapa kipaumbele matatizo ya vifo vya mama na watoto wachanga,
na kuandaa orodha ya mambo muhimu yakufanya ili kukabiliana na matatizo hayo.
Mkutano
utakapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa ili kuwezesha wale
walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 4 ?
Wanawake
wote waliohudhuria mkutano wa 3
wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Pia, kwa vile sasa wana uelewa zaidi juu ya
mchakato, unaweza kushawishi wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria – hususan wale ambao unafikiria wanasikilizwa
sana kwenye kitongoji, na ambao wana
uwezo wa kuwashawishi wengine.
Angalia
iwapo Wakunga wa Jadi wote wameshirikishwa na vuzuri zaidi wanapanga kuhudhuria kila mkutano.
Ajenda kwa
ajili ya Mkutano wa 4
1.
Makaribisho, utambulisho na mapitio ya mhutasari ya mkutano uliopita.
2.
Wasilisha lengo ya mkutano: Kuainisha matatizo makuu 4 ya afya ya mama
na watoto wachanga ambayo yatashughulikiwa katika mzunguko huu.
3.
Kujadili umuhimu wa kuanisha matatizo yatakayopewa kipaumbele. Ni
muhimu kuanisha matatizo yatakayopewa kipaumbele kwa sababu:
·
Kuliko kujaribu kushughulikia matatizo yote ya afya kwa mpigo, ni bora
kuanza na matatizo muhimu machache.
·
Ni bora zaidi kuanza na matatizo
ambayo jamii inahisi kuwa ndiyo muhimu zaidi.
·
Siku za usoni, baada ya matatizo haya ya kwanza kushughulikiwa,
kikundi kinaweza kurudi nyuma na kushughulikia
matatizo mengine yaliyobainishwa.
4.
Shughuli kuu za mkutano: Wezesha
wanawake ndani ya kikundi kuainisha matatizo makuu 4 yanayohusiana na vifo vya
mama na /au watoto wachanga ambayo yatashughulikiwa katika mzunguko huu. Tumia
kadi za picha za matatizo.
Angalia
MAELEZO chini jinsi ya kuuendesha mkutano.
5. Fanya majumlisho ya mkutano: Fanya
uchambuzi iwapo malengo ya mkutano yamefanikiwa vya kutosha. Kama
hayajafanikiwa, unaweza kurudi nyuma na kurudia vipengele vyote au baadhi ya vipengele vya mkutano. Angalia iwapo umejumlisha kwa
usahihi. Nani atafanya nini kabla ya
mkutano unaofuata?
6. Himiza washiriki kuuliza
maswali.
7. Panga tarehe ya mkutano ujao.
MAELEZO JUU YA NAMNA YA KUKIWEZESHA KIKUNDI
KUAINISHA MATATIZO YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE
1.
Panga
kwenye misitari 2 kadi za picha au michoro ya matatizo yote yaliobainishwa: msitari
wa kadi za picha zikionesha matatizo ya akinamama, na msitari mwingine wa kadi
za picha zikionesha matatizo ya watoto
wachanga.
2.
Wezesha
kikundi kujadili sababu tofauti kwa nini tatizola afya linaweza kuchukuliwa kuwa muhimu. (Tatizo linaweza kuchukuliwa kuwa muhimu kwa sababu: ni
tatizo kubwa; au siyo kubwa lakini
limeenea; au kwa sababu lina athari zenye wigo mpana – huathiri nyanja zingine
za maisha zaidi ya afya. Hata kama tatizo
siyo kubwa au halijaenea sana, linaweza kuchukuliwa kuwa muhimu kwa sababu, mathalan,
linakera kwa kuonekana haliwezi kutatuliwa.)
3.
Omba
kila mwanakikundi kuja mbele kwenye misitari ya picha, mmoja mmoja, na kuweka
jiwe karibu na tatizo linalowaathiri akinamama ambalo anadhani ndiyo muhimu zaidi, na lingine linaoathiri watoto wachanga ambalo
anadhani ndiyo muhimu zaidi.
Wambie kuwa hakuna jibu lisilo sahihi-majibu yote ni sahihi ! Vyovyote
anavyofikiri ndiyo muhimu zaidi kwetu kujua.
4.
Hesabu
idadi ya mawe pembeni ya kila tatizo na kuyapanga kwa kuzingatia umuhimu (idadi
kubwa ya mawe inamaanisha muhimu zaidi).
5.
Wezesha
kubainisha matatizo 2 muhimu zaidi ya akinamama, na matatizo 2 muhimu zaidi ya
watoto wachanga.
6.
Wezesha
kikundi kujadili kama wanadhani kuwa matatizo
makuu 4 yaliyotambuliwa yanaaksi ukweli wa hali katika jamii. Angalia
kama kikundi kinaafiki matatizo yaliyobainishwa
na wanawake ni matatizo
ambayo wanawake kwenye kikundi wanaamini kuwa ndiyo muhimu zaidi.
Mfano:
Wanawake ishirini katika kikundi cha Tushikamane, baada ya kubungua bongo, waliibua
matatizo 10 yafuatayo ambayo
yanasababisha vifo vya akinamama kuhusiana na uzazi. Baada ya hapo,
walipiga kura 1 kila mtu kwa tatizo ambalo walifikiri ndiyo baya zaidi. Kura
zilienda kama ifuatavyo:
1.
Kupoteza damu nyingi sana baada ya kujifungua
……… kura 6
2.
Mtoto kushindwa kupita kwenye pango la nyonga………..kura
4
3. Malaria………………………………………………………… kura 3
4.
Kifafa
cha mimba…………………………………………….. kura 2
5. Anemia…………………………………………………………kura 2
6. Matatizo yanayohusiana na kondo la nyuma
kuchelewa kutoka baada ya
mtoto kuzaliwa……………… kura 1
7. Maambukizi baada ya mimba
kuharibika ………………. kura1
8. Mkao mbaya wa mtoto katika tumbo la uzazi…………… kura 1
Kikundi kilifikiria kuwa matatizo
makuu muhimu zaidi ni: kupoteza damu nyingi baada ya
kujifungua, na mtoto kushindwa kupita
kwenye pango la nyonga.
Kura kwa matatizo ya watoto zilikuwa
kama ifuatavyo:
1.
Matatizo ya kupumua mara baada ya kuzaliwa …………kura 7
2. Malaria……………………………………….. kura 4
3. Maambukizi kwenye mfumo wa kupumua…. kura 4
4. Kuhara…………………………………………. kura 3
5. Sepsisi(maambukizi kwenye damu kutokanana sumu ) kura 1
6. Kuzaliwa kabla ya
kutimiza siku…………… kura1
7. Utapiamlo……………………………………….. kura 0
8.
Baridi-halijoto ya mwili kuwa chini ya kiwango
Cha kawaida
………………………… kura 0
9. Tetanasi( pepopunda)………………… kura 0
10. Homa ya manjano………………….
kura 0
Kama
mtaalam, unaweza kutokubaliana na vipaumbele vyao – unaweza mathalan kutaka kuweka
sepsisi(maambukizi ya sumu kwenye damu) na baridi-halijoto ya
mwili kuwa chini sana ya kiwango cha kawaida kwenye nafasi za juu katika orodha.
Inawezekana una taarifa au takwimu za vifo vya watoto
kutokana na matatizo hayo.
Hata
hivyo, dhamira ya mchakato wa Tushikamane ni kuishirikisha jamii na
kuihamasisha kukabiliana na matatizo
ambayo wanaamini ndiyo muhimu zaidi. Kwa njia hii, tunatarajia kutakuwepo na
shughuli nyingi zaidi, ushirikiano, shughuli hazitakwama, azma ya kufanikiwa na
undelevu wa matokeo ya mradi.
Hivyo, kikundi kimebainisha matatizo yafuatayo kupewa kipaumbele:
Kwa mama:
·
kupoteza damu nyingi baada ya kujifungua, na
·
mtoto kushindwa kupita
kwenye pango la nyonga;
Kwa watoto wachanga:
·
Matatizo ya kupumua mara baada ya kuzaliwa; na
·
Malaria.
Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako
ya mkutano wa 4
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa
kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi
walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wajawazito walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje – kulikuwa na mafanikio au changamoto zozote?
·
Orodha ya matatizo yalioainishwa kupewa
kipaumbele ikoje ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 4
·
Makatibu wanapaswa kuorodhesha wote waliohudhuria kwenye rejesta ya
kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wenzao ambao hawakuhudhuria juu ya mambo
yaliyojadiliwa kwenye mkutano.
MKUTANO WA 5
– KUBAINISHA MAMBO YANAYOCHANGIA MATATIZO
HAYO – MIZIZI YA MATATIZO
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 5
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu maarufu kwenye kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa 4. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu
kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika
umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na
watoto wachanga.
Wakumbushe
wanawake kuwa mkutano unaokuja utajaribu kubainisha mambo ambayo yanachangia
sana vifo vya mama na watoto wachanga.
Mkutano
unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha wale
walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 5?
Wanawake
wote waliohudhuria mkutano wa 4
wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Endelea kuwahimiza wanawake wengine katika umri wa uzazi
kuhudhuria – hususan wale ambao
unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao wana ushawishi.
Ajenda ya
Mkutano wa 5
1. Makaribisho,
utambulisho na mapitio ya mhutasari ya mkutano uliopita.
2.
Wasilisha lengo ya mkutano: kubainisha mambo ya msingi yanayosababisha matatizo
makuu yaliyotambuliwa ambayo yanahusiana na vifo vya mama na watoto
wachanga. Ni vigezo gani vinachangia matatizo hayo kuongezeka na /au kuwa na athari mbaya zaidi?
3.Wezesha
kikundi kujadili umuhimu wa kubainisha mambo yanayochangia matatizo yaliyotambuliwa.
Kumbuka ni muhimu kubainisha mambo ya msingi
yanayochangia kwa sababu:
·
Inawezekana kuzuia matatizo ya afya kuongezeka kwa kudhibiti mambo
hayo ambayo yanachangia.
·
Baadhi, siyo yote, ya matatizo ya afya yana mambo ambayo
yanayachochea, ambayo yanaweza kubainishwa.
·
Tatizo moja la afya linaweza kuwa
linachangiwa na mambo kadhaa.
4.
Shughuli kuu za mkutano: Wezesha
wanawake ndani ya kikundi kubainisha mambo ya msingi ambayo yanachangia yale
matatizo makuu 4 yanayohusiana na vifo vya mama na /au watoto wachanga
yaliyotambuliwa. Tumia kadi za picha za
matatizo na kadi za picha za mambo yayochangia matatizo hayo.
Angalia
MAELEZO yanayofuata namna ya kuendesha mkutano huo.
5. Fanya
majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani
atafanya nini kabla ya mkutano
unaofuata?
6. Fanya
uchambuzi iwapo malengo ya mkutano yamefanikiwa vya kutosha. Kama
hayajafanikiwa, unaweza kurudi nyuma na kurudia vipengele vyote au baadhi ya vipengele vya mkutano.
7.Himiza
washiriki kuuliza maswali
8.
Panga tarehe ya mkutano ujao.
MAELEZO
JUU YA NAMNA YA KUKIWEZESHA KIKUNDI KUBAINISHA MAMBO YA MSINGI AMBAYO
YANACHANGIA MATATIZO YALIYOTAMBULIWA
1.
Elezea kwamba mambo ya msingi
yanayochangia ni vile vigezo vya
kitabibu au kitiba, kijamii, na kiuchumi ambavyo husababisha matatizo ya afya
kutokea.
2.
Chora kwenye kipande kikubwa
cha karatasi picha ya mti ikionesha mizizi, shina na matawi.Shina la mti huwakilisha
tatizo. Mizizi huwakilisha matatizo yanayochangia-vile vigezo ambavyo
husababisha tatizo kukua. Matawi ya mti huwakilisha madhara na athari
zitokanazo na tatizo.
3. Weka
kadi ya picha ya tatizo kuu lililotambuliwa(mfano malaria) kwenye shina la mti.
4.
Wambie wanakikundi kutazama mizizi ya tatizo, (au mambo yanayochangia tatizo
hilo), na kuorodhesha mambo ambayo wanafikiri yanachangia tatizo la malaria
kuongezeka.
5.
Kadri kila jambo au kigezo ambacho kinachangia kinapobainishwa, weka kadi ya
picha ya kigezo hicho kwenye mizizi ya mti. ( Kama hakuna kadi yenye picha hiyo
unaweza kuchora jambo hilo au kuandika kigezo
hicho kwenye karatasi na kukiweka kwenye mizizi ya mti.)
Mathalan, kikundi kinaweza kubainisha mambo yanayochangia
kuongezeka kwa tatizo la malaria kuwa ni pamoja na: mbu wengi !; ukosefu wa maarifa kuzuia malaria; mazalia mengi ya mbu
yanayozunguka nyumba zenye maji yaliyotuama; kutolala chini ya kiandarua kila
siku; kutotibu vyandarua mara kwa mara
na dawa ya kufukuza mbu; kukosa fedha za kununua dawa unapogundua dalili za
ugonjwa huo; kutowahi kwenye kituo cha afya mara baada ya kuhisi dalili za
kwanza za ugonjwa huo.
Kama unafikiri
bado hujaifikia mizizi ya tatizo, basi endelea huhoji kwa kuuliza swali “kwa nini”. (mathalan “kwa nini unashindwa kwenda kwenye kituo cha
afya?” “Hatuna usafiri”, “kwa nini huna usafiri?” nk.
Jaribu kuhakikisha kuwa unapata mchanganyiko mzuri
wa mawazo juu ya mizizi ya tatizo, ambayo inajumuisha, kwa mfano, masuala ya
afya; miundombinu; umasikini; mila na desturi; hali ya kijamii; familia; na
elimu.
Hakuna majibu yasiyo sahihi na kikundi kinapaswa
kuhimizwa kuorodhesha mambo yote ambayo yanachangia, na madhara au athari zake
ambazo wanaweza kufikiria.
6. Rudia
hatua 3 hadi 5 kwa ajili ya matatizo
mengine 3 makuu yaliyotambuliwa.
Masuala
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 5
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari:
wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa
wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje –
je kulikuwa na mafanikio au changamoto gani
?
·
Mambo gani ambayo yanayochangia matatizo yameibuliwa kwa kila tatizo ambalo limetambuliwa ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 5
·
Makatibu wanapaswa kuorodhesha watu wotewaliohudhuria kwenye rejesta ya kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wenzao ambao hawakuhudhuria
juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
AWAMU
YA 2: KUPANGA NJIA ZA UFUMBUZI PAMOJA
Shabaha
ya Awamu ya 2 ya mzunguko wa mikutano ya Tushikamane ni
kwa ajili ya vikundi vya Tushikamane kupanga njia za ufumbuzi
au utatuzi wa matatizo ambayo husababisha vifo vya mama na watoto wachanga.
Awamu hii ina mikutano 3 ambayo
itafuatana hivi:
·
Mkutano wa 6: Kubainisha shughuli za kuzuia na kusimamia
matatizo hayo
·
Mkutano wa 7: Kubainisha njia za ufumbuzi au utatuzi wa
matatizo yaliyotambuliwa
·
Mkutano wa 8: Kuwasilisha maendeleo ya mchakato huu kwa wanajamii
MKUTANO WA 6 – KUBAINISHA SHUGHULI ZA KUZUIA NA KUSIMAMIA
MATATIZO HAYO
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 6
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu maarufu kwenye kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa 5. Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu
kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu: kuwapa wanawake walio katika
umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na
watoto wachanga.
Wakumbushe
wanawake kuwa mkutano unaokuja utajaribu kubainisha shughuli za kuzuia vifo vya mama na watoto wachanga.
Mkutano
unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha wale
walitoa mchango muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.
Hakikisha
kuwa unazo kadi za picha za matatizo makuu yote 4; na kadi za picha za mambo
yanayochangia kila tatizo.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 6 ?
Wanawake
wote waliohudhuria mkutano wa 5
wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Endelea kuwahimiza wanawake wengine katika umri wa uzazi
kuhudhuria – hususan wale ambao
unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao wana uwezo
wa kuwashawishi wengine.
Ajenda ya 6
1. Makaribisho,
mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita na utambulisho
2. Kuwasilisha
malengo: Kikundi kimechagua matatizo makuu 4 ya kushughulikia – 2 ya akinamama,
na 2 ya watoto wachanga. Katika mkutano
huu, lengo ni kuibua shughuli ambazo zinaweza:
·
Kuzuia matatizo hayo yasitokee.
·
Kusimamia (kukabiliana) na matatizo
hayo iwapo yatajitokeza.
Mifano ya uzuiaji na usimamizi kama tatizo ni malaria:
Shughuli
za uzuiaji
·
Kuongeza uelewa juu ya uzuiaji wa malaria.
·
Kuondoa mazalia ya mbu yanayozunguka nyumba.
·
Kuwashawishi wafanyakazi wa afya kutoa vyandarua kwenye kliniki za
mama wajawazito.
·
Kuwashawishi viongozi na wasimamizi wa idara husika kuhakikisha
kuwepo akiba ya vyandarua vya kutosha na
kupunguza rushwa.
·
Kulala chini ya chandarua kila
siku.
·
Kutibu vyandarua na dawa ya kuua
mbu kila baada ya muda kama itakavyoshauriwa.
·
Wajawazito kujifungulia kwenye
kituo cha afya chini ya chandarua.
·
Kuboresha lishe ya mama ili
kuimarisha kinga yake dhidi ya magonjwa.
Shughuli
za usimamizi malaria
·
Kutumia vidonge vya malaria, (kama
vinapatikana) kama itakavyoelekezwa na mfanyakazi wa afya.
·
Kumwahisha mgonjwa kwenye kituo
cha afya cha karibu kama ana dalili za
malaria. kama vile homa, kuhisi baridi kali, maumivu ya kichwa, au maumivu ya
viungo.
3. Kujadili
umuhimu wa kuibua shughuli za uzuiaji na
usimamizi wa matatizo hayo:
·
Kama mambo yanayochangia matatizo
makuu yaliyotambuliwa yapo ndani ya
jamii husika, basi shughuli za uzuiaji zinaweza kuyasimamisha ili yasiendelee
kusababisha matatizo ya afya.
·
Hata kama matatizo haya makuu ya
afya yaliyotambuliwa yatajitokeza kwenye jamii, basi shughuli za usimamizi
zinaweza kusaidia kuyadhibiti ili
yasilete madhara au athari mbalimbali.
Jaribu kukifanya
kikundi kutambua kuwa mara nyingi tunaamua kuishi na matatizo bila kujitahidi
kukabiliana nayo vizuri mara yanapojitokeza, wala kushughulikia mizizi yake iliyojichimbia kwenye jamii zetu.
4.
Shughuli
kuu za mkutano: Kamata orodha ya matatizo makuu 4 yaliyotambuliwana kikundi. Wambie wanawake kwenye kikundi kufikiria
shughuli mbalimbali za uzuiaji na usimamizi wa matatizo hayo. Angalia
MAELEZO chini, na kutumia seti 4 za kadi za picha:
·
‘Kadi za picha za matatizo’;
·
‘Kadi
za picha za mambo yanayochangia matatizo hayo;
·
‘Kadi
za picha za shughuli za uzuiaji; na
·
‘Kadi za picha za shughuli za usimamizi wa matatizo hayo’.
5.
Fanya
majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani
atafanya nini kabla ya mkutano
unaofuata?
6. Fanya uchambuzi iwapo malengo
ya mkutano yamefanikiwa vya kutosha. Kama hayajafanikiwa, unaweza kurudia vipengele vyote au baadhi ya vipengele vya mkutano.
7. Himiza washiriki kuuliza
maswali.
8. Panga tarehe ya mkutano ujao.
MAELEZO JUU YA KUBAINISHA SHUGHULI MBALIMBALI
KWA AJILI YA KUZUIA NA KUSIMAMIA
MATATIZO MAKUU YANAPOJITOKEZA
1. Eleza
kwamba shughuli za uzuiaji ni zile shughuli ambazo zinaweza kuzuia mambo
yanayochangia matatizo ya afya kutokea na hivyo kusimamisha au kuzuia matatizo
hayo ya afya yasiibuke.
2. Eleza
kwamba shughuli za usimamizi ni zile shughuli ambazo zinaweza kuzuia matatizo
ya afya yasisababishe madhara au athari.
3.
Weka chini kadi ya picha ya tatizo kuu la afya lililotambuliwa.
4.
Katika mkutano wa 5, kikundi
kilibainisha mambo ambayo yanachangia tatizo hili kuibuka. Kama mlivyofanya
kwenye mkutano wa kwanza, chora chini picha ya mti, na kuweka tatizo katikati ya
mti. Halafu weka kadi za picha ya mambo yanayochangia kwenye mizizi.
5.
Himiza wanakikundi kuweka shabaha kwenye shughuli za uzuiaji ambazo
husaidia kuzuia mambo yanayochangia yasiibuke. Tumia kadi za picha za uzuiaji,
(au tengeneza za kwako kama kikundi hakitapata mbadala).
Usisahau zile
shughuli za uzuiaji kama vile mabadiliko ya mila na desturi hatarishi ili watu
waweze kutafuta msaada wa kiafya mapema; au kuwaweka wanajamii pamoja
kushinikiza maboresho huduma za afya; au kufanya mambo ambayo husaidia
kuhakikisha kuwa mabadiliko yaliyoahidiwa yatapatikana.
Kusanya pamoja kadi zote za picha ambazo wanawake
wamechagua kuwa zinaelekeza jinsi ya kutatua mizizi ya matatizo ili kuyazuia
kutokea.
6.
Halafu badilisha shabaha ya kikundi ielekee kwenye shughuli za
usimamizi wa matatizo yaliyobainishwa. Himiza kikundi kulenga shughuli ambazo husaidia kusimamisha tatizo
lililobainishwa kutosabisha vifo au uharibifu mwingine. Tumia kadi za picha za
shughuli za usimamizi (au tengeneza za kwako kama kikundi hakiwezi kutoa
mbadala wa kadi ya picha ambayo umekosa).
Majibu yote ni sahihi ! Usifadhaike iwapo utaona
mjadala unapanuka sana na kutoka kwenye shabaha. Lakini kumbuka kuwarudisha kwenye kipengele husika- kuchagua kadi za
picha ambazo zinawakilisha njia mbalimbali
za kutatua tatizo husika,au angalau
zitalizuia tatizo kutosababisha vifo.
Kusanya pamoja kadi zote zenye picha ambazo wanawake
wamechagua kuwa zinaonesha jinsi ya kusimamia tatizo ili kuzuia lisisababishe
vifo.
Rudia hatua 1 hadi
6 kwa yale matataizo mengine makuu 3. Mwisho
wa mchakato huu, utakuwa na seti ya kadi
za picha za uzuiaji, na seti za kadi za picha za usimamizi,ambazo zinaelezea
njia zote zinazoweza kuchukuliwa na kikundi kusimamisha vifo kutokea.
Masuala muhimu kwa
ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 6
·
Rejesta
ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi,
wangapi walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa na mafanikio au changamoto zozote?
·
Ni
shughuli gani za uzuiaji na usimamizi ziliibuliwa kwa ajili ya kila tatizo ambalo limepewa kipaumbele ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 6
·
Makatibu wanapaswa kuorodhesha wahudhuriaji wote kwenye rejesta ya
kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
MKUTANO WA 7 – KUANDAA MIPANGO
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 7
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu maarufu kwenye kitongoji ambao
walihudhuria mkutano wa 5. Wafanye
wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu:
kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa ajili ya
kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.
Wakumbushe
wanawake kuwa mkutano unaokuja utajaribu kutafakari mipango inayostahili na
kubainisha njia za ufumbuzi. Hii itakuwa
fursa maalum kwa wanawake kutoa maoni yao na mawazo yao kusikika.
Mkutano
utakapokaribia, wakumbushe wanakitongoji tarehe, muda na mahali mkutano utakapofanyika,
na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha wale walitoa mchango
muhimu katika mkutano uliopita kuwepo.
Kusanya
pamoja kadi zote za picha kutokana na mkutano uliopita:
·
Kadi
za picha za matatizo yote 4
·
Kadi
za picha zenye mizizi ya kila tatizo- mambo yanayochangia tatizo hilo;
·
Kadi
za picha walizochagua wanawake ambazo
zinaonesha shughuli za kuzuia tatizo
husika; na
·
Kadi
za picha walizochagua wanawake ambazo zinaonesha shughuli
zitakazofanyika kuzuia vifo, iwapo
tatizo husika litajitokeza.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 7 ?
Wanawake
wote waliohudhuria mkutano wa 6
wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza. Endelea kuwahimiza wanawake wengine katika umri wa uzazi
kuhudhuria – hususan wale ambao
unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao huwa wana uwezo wa kuwashawishi .
Ajenda kwa
ajili ya Mkutano wa 7
1. Makaribisho, mapitio ya mhutasari wa mkutano
uliopita na utambulisho
2.
Kuwasilisha lengo la mkutano: mkutano huu unalenga kuweka pamoja
mawazo kutokana na mikutano kadhaa ambayo imefanyika, na kuyageuza kuwa mipango
na ufumbuzi wa kukabiliana na matatizo makuu 4 yaliyotambuliwa, au vizuri zaidi,
kuweza kupambana na mizizi ya matatizo
hayo. Baada ya hapo, unaweza kuendelea kujadili jinsi gani njia hizi za
ufumbuzi zinaweza kufanikishwa.
Siku ya mkutano huo ni siku ya kugeuza mijadala iliyofanyika huko
nyuma kuwa mapendekezo kamili kwa kitongoji kizima.
3. Shughuli
kuu za mkutano: Chagua tatizo kuu mojawapo – vizuri zaidi lile ambalo kila mtu
anataka ndiyo litatuliwe haraka. Katika mikutano 3 iliopita, wanawake watakua
walikwisha kutafakari mizizi ya tatizo,
na kuibua mawazo mbalimbali namna ya kukabiliana na tatizo hilo ili lisisababishe vifo, na pia
namna ya kushughulikia mizizi yake.
Tandaza chini kadi ya picha ya tatizo; kadi za picha
ya mambo yanayochangia; kadi za picha za
shughuli za uzuiaji; na kadi za picha za shughuli za usimamizi wa tatizo. Unaweza
kutaka kuendelea na zana ya mti na
mizizi yake, na kuuweka mti kama tatizo, mambo yanayochangia kama mizizi, na kuweka kadi za picha za shughuli za uzuiaji na
usimamizi wa tatizo kuzunguka mti- zikiwa ndiyo shughuli zitakazofanyika
kukabiliana na tatizo hilo.
Sasa unaweza kuyageuza haya yote kuwa mipango ya
awali. Mipango halisi itakamilishwa wakati kikundi kitakapopanuliwa na
kujumuisha wanaume na wale wote ambao watahitaji kujiunga na kikundi. Lakini
mkutano huu unahusu kuwawezesha wanawake
kutoa mawazo yao kwanza.
Waulize wanawake mambo gani hasa wangependa wayaone yakitekelezwa, kwani
sasa wamekwisha kutafakari kwa kina juu ya
tatizo. Katika hatua hii, usijisumbue sana na masuala ya fedha na vipengele vyote vidogo
vidogo ndani ya mipango hii. Tunachotaka ni orodha ya mambo
ambayo wanawake hasa wangependa kuona yakifanyika, na baada ya hapo tunaweza
kuangalia uwezekano wa kutekeleza
na kufanikisha njia mbalimbali za
ufumbuzi ambazo zimechaguliwa.
Kama matatizo yote 4 ambayo yamechaguliwa ni, mfano:
kwa akinamama, kupoteza damu nyingi baada ya kujifungua na mtoto kushindwa
kupita kwenye pango la nyonga; kwa watoto wachanga, maambukizi (yakiwemo malaria), na kuhara. Kikundi kitakuwa
kinafikiria siyo tu wafanye nini wakati
tayari mama au mtoto ana tatizo hilo, lakini pia jinsi ya kuzuia tatizo hilo
kutokea.
Unataka kutumia yote hayo kutengeneza orodha ya njia za
ufumbuzi wa tatizo ambazo zinawezekana. Wanaweza
kuibua orodha kama ifuatayo:
·
Mafunzo kwa wakunga
wa jadi ili waweze kukabiliana na matatizo, kuzuia yasitokee, na kuwafikisha wajawazito haraka hospitalini kupata msaada zaidi.
·
Shughuli mbalimbali za uzalishaji pato ili kupunguza
umasikini na utapimalo.
·
Kuboresha huduma ya maji safi na salama kupitia
juhudi za jamii yenyewe.
·
Kuanzisha bustani za kikundi za mbogamboga ambazo zitatoa chakula cha ziada kwa wajawazito wenye mahitaji.
·
Kuanzisha kampeni ndani ya kitongoji kwa ajili ya
kusafisha mazalia ya mbu. Kuazisha juhudi za kuwapatia akinamama wote na watoto vyandarua.
·
Kuanzisha juhudi za kutibu vyandarua vyote na dawa
ya kuua au kufukuza mbu kadri itakavyoelekezwa na wataalam.
·
Kuhakikisha wajawazito wanahudhuria kliniki, hasa
kuanzia mwezi 6 – 7, wakati afya zao zinatakiwa kupimwa, (mathalan kwa ajili ya
anemia), na hatari ya kupata matatizo
wakati wa kujifungua inaweza kujadiliwa. Mathalan msichana wa miaka 15 mwenye umbo dogo yuko katika
hatari zaidi ya kushindwa kumpitisha mtoto
kwenye pango la nyonga kuliko yule ambaye tayari amezaa watoto kadhaa.
·
Kutafuta baisikeli au pikipiki maalum ya
wagonjwa kwa ajili ya kuwawahisha
wanawake na watoto wachanga kwenye kituo cha afya kilichoko karibu.
·
Programu ya elimu ya afya kwa akinamama juu ya kulinda
watoto wachanga wasipatwe na maambukizi makali,
na namna ya kuwahudumia ili wasipoteze maisha kama watapata maambukizi.
·
Kuanzisha mfuko wa kikundi wa dharura kwa ajili ya
usafiri.
·
Kuanzisha
utaratibu wa kuwaita wanaume kutoa
msaada kwa ajili ya kuwapeleka wanawake kwenye kituo cha afya au hospitalini
wakati wa dharura.
Katika
hatua hii ya mchakato wa Tushikamane,huhitaji kutafuta vipaumbele- kuchagua
hili au lile. Hii itakuja baada ya mikutano kadhaa inayofuata.
4.Fanya majumlisho ya mkutano na
kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini kabla ya mkutano unaofuata?
5. Pima kama umepata orodha nzuri
ya mipango na njia za ufumbuzi za kuanzia. Kama hili halijafikiwa, unaweza
kurudi nyuma na kurudia baadhi ya vipengele
vya mkutano au vipengele vyote.
6. Himiza washiriki kuuliza
maswali
7. Panga tarehe ya mkutano ujao.
Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako
ya Mkutano wa
7
·
Rejesta ya
mahudhurioinapaswakukamilishwa kwa muhtasari:wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi,
wajawazito walikuwa wangapi ?
·
Mkutano uliendaje – je, kulikuwa na mafanikio au changamoto zozote?
·
Ulitoka na orodha gani ya mwisho ya mipango na njia za ufumbuzi?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 7
·
Makatibu wanapaswa kuwaorodhesha washiriki wote kwenye rejesta ya kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·
Jaribu kujenga hamasa ndani ya kitongoji kizima juu ya mkutano ujao,
ambao unatarajiwa kupeleka mchakato mbele
kwenye hatua nyingine.
MKUTANO WA 8 – KUWASILISHA MAENDELEO YA MCHAKATO KWA JAMII
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 8
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Hasa,
wewe na kikundi, kwa msaada wa Alex, Wilbard na Mchungaji Isaac, mnatakiwa
kufanya mazoezi ya kazi itakayowasilishwa kwenye mkutano.
Tembelea
watu maarufu kwenye kitongoji
waliohudhuria mkutano wa 5.
Wafanye wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la
programu: kuwapa wanawake walio katika umri wa uzazi sauti katika kupanga kwa
ajili ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.
Wakumbushe
wanawake kuwa mkutano unaokuja utajaribu kutafakari mipango na kubainisha njia
za ufumbuzi, na hiyo itakuwa fursa ya pekee
kwa wanawake kutoa maoni yao na mawazo yao kusikika.
Mkutano
unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu
wote maarufu kwenye kitongoji kuhudhuria.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 8?
Mkutano wa 8 ni mkutano
mahali ambapo ripoti juu ya maendeleo ya
mchakato wa Tushikamane itawasilishwa kwa jamii. Kuanzia hatua hii, itakuwa
bora kupanua uanachama kujumuisha wale wote ambao wanaweza kuchangia, kwa namna
moja au nyingine, kupunguza vifo vya akinamama wakati wa kujifungua, na vifo vya watoto wachanga.
Uanachama katika kikundi utahitaji kuzingatia mila
na desturi, lakini vikundi vinaweza kujumuisha wafanyakazi wa afya vijijini au wafanyakazi
wengine wa afya; viongozi wa jamii; walimu;
wenzi wa wanawake na wasichana balehe walioko kwenye kikundi; wafanyakazi wa
ugani au wa mashirika ya misaada ambao wanashughulikia matatizo haya; na yeyote
ambaye anaguswa na afya ya wanawake na watoto wao kwa ujumla.
Endelea
kuwashawishi wanawake wote waliohudhuria mkutano wa 7
kuhudhuria kama wanaweza. Endelea pia kuwahimiza wanawake wengine katika umri wa uzazi kuhudhuria
– hususan wale wenye sauti wanaosikilizwa
sana kwenye kitongoji, na wana ushawishi.
Kupanga
uwasilishaji wa ripoti kwa jamii katika mkutano wa 8
Unahitaji
kufanya mkutano rasmi na Msimamizi wako Alex, na Kiongozi wa Mradi, Wilbard
Mrase, kupanga jinsi gani Kikundi cha Tushikamane kutakaivyowasilisha ripoti ya
maendeleo kwa wanakitongoji. Mnaweza kuamua pamoja kuwa na mkutano mwingine
kutoa mawazo yenu kwa Mwenyekiti wa Mradi, Mchungaji Isaac Mgego, ili kupitia mipango yenu na kuiboresha zaidi.
Wewe Alex na Wilbard, kwa ushauriano na Kikundi cha Tushikamane, mnahitaji kutoka na mwafaka jinsi gani mkutano utakavyoendeshwa. Mnahitaji
kuamua mtasema nini juu ya mambo yafuatayo, na jinsi ya kuyasema. Mnaweza
kuamua kugawana majukumu – kwa mfano Kiongozi wa Mradi kutoa utambulisho na malengo ya mkutano; Msimamizi kueleza
jinsi programu inavyofanya kazi; na wewe kueleza mafanikio gani yamepatikana.
Ili
kufanya shughuli kuwa changamfu na
kuvuta umakini na matumaini ya watu wengi, unaweza kuingiza kwenye ripoti yako ya maendeleo, baadhi
ya michango ya wanawake kutoka kikundi hicho – mathalan igizo dhima dogo au mziki au wimbo.
Usisahau
kutumia kadi za picha kukusaidia kuwasilisha ujumbe.
Baada
ya kufanya mkutano na Kiongozi wa Mradi, Msimamizi, na ikiwezekana Mwenyekiti, unapaswa
kuwa na picha kamili jinsi kila kipengele cha mkutano kitakavyoshughulikiwa:
·
Ajenda na malengo ya mkutano – mathalan kuwasilishwa na Kiongozi wa
Mradi Wilbard Mrase.
·
Taarifa za msingi juu ya
programu ya Tushikamane na jinsi inavyofanya kazi – mathalan
kuwasilishwa na Alex Gongwe.
·
Taarifa ya maendeleo ya Kikundi
kuwasilishwa na wewe, pamoja na wanawake kutoka Tushikamane watakaoteuliwa.
Pamoja, mnaweza kueleza kwa nini na namna gani mmechagua matatizo hayo makuu 4;
kueleza mizizi yake; kueleza mambo ambayo yanaweza kuwa yanachangia matatizo
hayo au mizizi yake; na kutoka na orodha ya mipango na njia za ufumbuzi.
·
Zoezi la maswali, maoni na mawazo kutoka kwa washiriki linaweza kuongozwa na Alex au Wilbard.
Kuandaa mwaliko kwa jamii kuhudhuria Mkutano wa 8
Katika
mkutano wako wa kuandaa mpango wa mwaliko na Alex na Wilbard, unahitaji pia kuamua nani
wataalikwa na kwa njia gani. Watu ambao mnaweza kualika wameorodheshwa juu.
Wataalikwaje
? Kwa mfano, kwenda nyumba mmoja hadi
nyingine; kupitia matangazo kanisani; kwa njia ya barua; kuwaomba wanawake
kwenye kikundi kuja na watu nk.
Kuendesha wa
Mkutano 8 – kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya kikundi cha Tushikamane
1. Makaribisho
na utambulisho.
2. Kuwasilisha
malengo ya mkutano:Kutoa mrejesho juu ya mijadala, yakiwemo matatizo makuu
yaliyobainishwa na njia za ufumbuzi, kwa wanajamii wote ili kupata maoni yao; mawazo
yao; na kupata misaada ya hali na mali
kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za
ufumbuzi.
3. Mambo ya
msingi juu ya Mradi wa Tushikamane na jinsi unavyofanya kazi.
4. Shughuli
kuu za mkutano: Kutumia njia zilizopangwa mapema, kuwasilisha kwa jamii taarifa
ya maendeleo ya kikundi hadi sasa. Shirikisha wanawake kutoka kwenye kikundi
kukusaidia katika zoezi hili.Tumia njia zingine shirikishi –mathalan nyimbo, kucheza
ngoma, kuigiza, kadi za picha nk.
Malizia kwa
kuwasilisha kwa washiriki orodha ya mipango na njia za ufumbuzi ambazo wanawake
walipendekeza. Hadi hatua hii, kitongoji kizima kinapaswa kuwa na uelewa kwamba
ili kukabiliana na vifo vya akinamama na watoto wachanga, wanapaswa kukabiliana
na mizizi ya matatizo yanayosababisha vifo hivyo.
5. Fungua
mjadala kwa wanajamii kubadilishana mawazo. Majadiliano yanaweza kuchukua
mkondo wowote ule lakini katikati warudishe washiriki kwenye msitari ili
wakubaliane kwa pamoja kuchagua wafanye nini, na namna gani.
6. Fanya
majumlisho ya mkutano, na tafuta mwafaka kutoka kwa washiriki kuwa ndivyo mkutano
ulivyokuwa. Nani atafanya nini kabla ya mkutano unaofuata?
7.
Panga tarehe ya mkutano ujao.
Masuala
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 8
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari:
wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa
wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa
na mafanikio au changamoto zozote?
·
Taarifa gani, maswali na mawazo gani yaliibuliwa na wanajamii ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 8
·
Makatibu wanapaswa kuorodhesha wote waliohudhuria kwenye rejesta ya
kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·
Jaribu kupata maoni ya viongozi na watu wengine ambayo yanaweza
kusaidia kupima umuhimu wa juhudi inayoendelea kwenye kitongoji, na
kushiriki angalau katika mkutano 1 au 2, ili waweze kuona kama
wangependa kushiriki katika programu ya Tushikamane.
AWAMU
YA 3: KUTEKELEZA NJIA ZA UFUMBUZI PAMOJA
Shabaha
ya Awamu ya 3 ya mzunguko wa mikutano ni
kwa vikundi vya Tushikamane kutekeleza njia za ufumbuzi zilizobainishwa katika kukabiliana
na matatizo ambayo yanasababisha vifo vya mama na watoto wao wachanga.
Awamu ya 3 ina mikutano 3:
·
Mkutano wa 9: Kupanga ufumbuzi: ambapo jamii itaunda
kamati mbalimbali – kamati 1 kwa ajili
ya kila njia ya ufumbuzi ambayo wanapanga kutekeleza.
·
Mkutano wa 10: Kukusanya rasilimali: kila kamati kufanya
kazi na mbia au asasi ambayo Tushikamane itasaidia kutafuta, kukusanya
rasilimali ambazo watahitaji kutekeleza ufumbuzi uliopangwa.
·
Mkutano wa 11: Kubuni zana za ufuatiliaji: ili tuweze
kujua iwapo njia za ufumbuzi ambazo
zinatekelezwa zinazaa matunda.
Baada ya hapo, kutakuwa na muda kabla ya Awamu ya 4 – mikutano 3 ya mwisho – ili njia za
ufumbuzi ziweze kutekelezwa, na shughuli
zilizopangwa kufuatiliwa vizuri. Muda huu unaweza kuwa takriban kati ya miezi 3 na 6.
MKUTANO WA 9 – KUPANGA NJIA ZA UFUMBUZI
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 9
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Hasa,
wewe na kikundi, kwa msaada wa Alex, Wilbard na Mchungaji Isaac, mnatakiwa
kufanya mazoezi ya kazi itakayowasilishwa kwenye mkutano.
Tembelea
watu muhimu kwenye kitongoji ambao
walihudhuria mkutano wa 8. Wafanye
wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu:
kutekeleza mipango ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga.
Eleza
bayana kwamba programu ya Tushikamane haitagharamia ufumbuzi, lakini itasaidia kuunganisha
kitongoji na wadau au asasi zingine ambazo zinaweza kuwaunga mkono kufanikisha
njia za ufumbuzi walizopanga. Ni rahisi zaidi kupata msaada-kwa mfano kutoka
idara za serikali au mashirika ya misaada-pale ambapo kuna mipango ambayo imetokana
mchakato makini shirikishi, ambao
umewashirikisha kwa ukamilifu wanawake walio katika umri wa uzazi.
Mkutano
unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu wote
maarufu kwenye kitongoji kushiriki.
Watu
wanaostahili kwenye jamii sasa wanaweza kujiunga na kikundi cha Tushikamane. Hivyo, kutakuwa fursa nzuri zaidi za kutafuta msaada
na kuunganisha nguvu na juhudi za jamii. Hii italeta mabadiliko makubwa katika
juhudi za kuzuia vifo.
Wakumbushe
watu maarufu katika kitongoji kwamba mkutano ujao utajaribu kubainisha njia za
ufumbuzi ambazo zinatarajiwa kuendelezwa,
na mkutano huo utakuwa wakati maalum kwa
mawazo yao kusikika, yakiongzea yale
ambayo wanawake watakuwa tayari
wamejadili.
Mkutano
utapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu
wote maarufu kwenye kitongoji kushiriki.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 9 ?
Wanawake
wote waliohudhuria Awamu ya 1 na 2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza.
Pia,
kikundi kitakuwa kimebaini watu maarufu kupitia mikutano iliyopita, ambao
ushiriki wao utasaidia kikundi kufanya kazi vizuri na kuongeza uwezekano wa
kufanikiwa.
Watu
kama hao ni pamoja na Wenyeviti wa Vijiji, Wafanyakazi wa Afya Vijijini,
wafanyakazi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, nk.
Endelea
kuwahimiza wanawake wengine katika umri
wa uzazi kuhudhuria – hususan wale ambao
unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao huwa wana uwezo wa kuwashawishi wengine.
Ajenda ya Mkutano wa 9
1. Makaribisho,
utambulisho, na taarifa fupi ya mchakato wa Tushikamane hadi ulipofikia sasa,
na wapi unaelekea.
2.
Hasa wakaribishe wanakikundi wapya, hususan wanaume.
Sisitiza kwamba wana wajibu muhimu ambao wanapaswa kutimiza. Wana wajibu wa kutoa ushauri na msaada
pale unapohitajika, ili kufanikisha lengo la kupunguza vifo vya mama na watoto
wachanga. Lakini kutokana na jinsi
kikundi kinavyofanya kazi, wanatarajiwa kusikiliza na kuheshimu mawazo na maoni
ya wanawake.
3. Wasilisha malengo ya mkutano:
·
Baada ya mkutano, kutoka na orodha
ya njia za ufumbuzi zilizopendekezwa ambazo jamii itakuwa ikitekeleza.
·
Kuunda kamati ya kufanikisha kila ufumbuzi uliopendekezwa.
·
Halafu kila kamati kukubaliana juu ya mpango kazi wake kwa ajili
ya utekelezaji wa ufumbuzi waliopewa.
Eleza kwa nini mchakato
huu makini wa kupanga husaidia siyo tu
kuchagua matatizo sahihi ya kukabiliana nayo, na njia sahihi za kukabiliana
nayo, lakini pia huwaleta watu wote
kufanya kazi pamoja, kigezo ambacho huchangia uwezekano mkubwa wa kufanikiwa.
4.
Shughuli kuu za mkutano: Angalia kwenye orodha ya njia za ufumbuzi ambayo
imewasilishwa kwa jamii kwenye mkutano wa 8. Sasa unahitaji kupunguza orodha hii hadi shughuli
3 au 4 ambazo kikundi kitakabiliana nazo.
Andika
shughuli zilizochaguliwa (mfano shughuli 4) kwenye vipande vya karatasi, na
kuweka shughuli moja kwenye kila kona ya chumba, au kama ni mduara weka nje ya mduara vipande 4 vya karatasi
vyenye majina ya shughuli hizo 4, kuzunguka mdwara ukiacha nafasi sawa katikati.
Wambie
wanakikundi kuinuka na kuelekea kwenye shughuli iliopangwa ambayo wangependa
kushiriki. (Kama wanataka kushiriki katika zaidi ya shughuli moja, basi
wawezeshe katika hatua hii kuchagua moja ambayo wanahisi ndiyo muhimu zaidi.)
Mchakato
huu unapaswa kuishia katika kukigawa
kikundi katika vikundi vidogo 3 au 4. Kila kikundi kidogo kinakuwa kamati ya
kusaidia utekelezaji wa shughuli iliopangwa ambayo wamechagua kushiriki.Kamati
zote zinapaswa kufanya kazi pamoja kwa takriban saa 1, na kutoka na mpango kazi
kwa ajili ya shughuli yao iliyopangwa kusaidia kutatua tatizo au matatizo
yaliyobainishwa.
Mwisho
wa mchakato huu, kikundi kizima
kitaungana tena, na kila kamati kutoa mrejesho kwa kikundi kikubwa
inayojumuisha mambo yafuatayo:
·
Jina
la shughuli iliopangwa ambayo wamechagua kushiriki ili kusaidia kuzuia vifo vya
mama na watoto wadogo.
·
Jina
la mwenyekiti wa kamati, ambaye atatunza kumbukumbu za kila kinachoendelea na
kutoa taarifa katika mkutano ujao.
·
Hatua
zinofuata – watafanya nini; na ifikapo
lini?
·
Nani
hasa atafanya nini ?
7. Fanya majumlisho ya mkutano na
kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini
kabla ya mkutano unaofuata?
8. Pima
kama malengo ya mkutano yamefikiwa vya kutosha. Kama hapana, unaweza kurudi
nyuma na kurudia baadhi au vipengele
vyote vya mkutano.
9.
Himiza washiriki kuuliza maswali
10.
Panga tarehe ya mkutano ujao.
Masuala
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 9
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari:
wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa
wangapi, wajawazito walikua wangapi ?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa
na mafanikio au changamoto zozote?
·
Kwa kila njia ya ufumbuzi iliyobainishwa, wamekubaliana nini juu ya
kamati, kanuni na mpango kazi ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 9
·
Makatibu wanapaswa kuorodhesha waliohudhuria wote kwenye rejesta ya
kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·
Jaribu kupata maoni ya viongozi na watu wengine ambayo yanaweza
kusaidia kupima umuhimu wa juhudi inayoendelea kwenye kitongoji, na
kushiriki angalau katika mkutano 1 au 2, ili waweze kuona kama
wangependa kushiriki katika programu ya Tushikamane.
·
Tembelea kila mwenyekiti wa kamati, pamoja na watu wengine maarufu
ambao ungependa washiriki. Washawishi kuchukua hatua, na kuwauliza wangehitaji
msaada gani ili waweze kufanikisha
shughuli zao.
·
Jadiliana mambo haya na msimamizi wako, na kuyaleta kwenye mkutano wa
kila mwezi na Kiongozi wa Mradi na Mwenyekiti wa Mradi. Katika hatua hii ya
mchakato wa Tushikamane, huu ndiyo
wakati wa kuanza kuvisaidia vikundi
kuwasiliana na wadau wengine ambao
wanaweza kutoa misaada ya hali na mali kufanikisha shughuli za kikundi.
Ili
kuweza kuwaunganisha na wadau husika, watahitaji picha halisi ya
kinachoendelea, na nini hasa kila kamati inatafuta.
MKUTANO WA 10 – KUKUSANYA
RASILIMALI
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 10
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Hasa,
wewe na kikundi, kwa msaada wa Alex, Wilbard na Mchungaji Isaac, mnatakiwa kuifanya
mazoezi kazi itakayowasilishwa kwenye mkutano.
Tembelea
watu muhimu kwenye kitongoji ambao
walihudhuria mkutano wa 9. Wafanye
wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha kusudio la programu:
kupanga kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga. Hii hatimaye itavutia
misaada ya hali na mali kutoka nje ya kitongoji ambayo itaunganishwa na juhudi
za jamii, na kuleta msukumo mkubwa katika kuzuia vifo hivyo vya kusikitisha.
Wakumbushe
watu maarufu kwenye kitongoji kwamba
mkutano unaokuja utajaribu kubainisha rasilimali zinazohitajika na wapi pa
kuzipata, na wao wenyewe wanaweza kuwa na chochote cha kuchangia.
Mkutano
unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu
wote maarufu kwenye kitongoji kuwepo.
Nani anapaswa kuhudhuria Mkutano
wa 10 ?
Wanawake
wote waliohudhuria Awamu ya 1 na 2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza, na wengine wapya waliohudhuria mkutano wa 9.
Pia,
kikundi kitakuwa kimetambua watu maarufu
kupitia mikutano iliyopita ambao ushiriki wao utasaidia kikundi kufanya kazi
vizuri na kuongeza uwezekano wa kufanikiwa.
Watu
kama hao ni pamoja na wenyeviti wa vijiji, wafanyakazi wa afya vijijini,
wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, nk.
Endelea
kuwahimiza wanawake wengine katika umri
wa uzazi kuhudhuria – hususan wale ambao
unafikiria wanasikilizwa sana kwenye kitongoji, na ambao huwa wana uwezo wa kuwashawishi wengine.
Ajenda ya Mkutano wa 10
1. Makaribisho,
mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita na utambulisho.
2. Kuwasilisha
lengo la mkutano: kupanga jinsi ya kukusanya rasimali ambazo zinahitajika kwa
ajili ya utekelezaji wa ufumbuzi kwa matatizo yaliyobainishwa.
3.
Shughuli
kuu za mkutano: kupanga jinsi ya kukusanya rasilimali kwa ajili ya kufanikisha
ufumbuzi. Ingawa kikundi sasa kina, kwa mfano kamati 4, kila moja ikijaribu
kutekeleza ufumbuzi wake uliopangwa, bado ni bora kufanya zoezi la leo la
kupanga kwa pamoja. Sababu ni kwamba inawezekana wanakikundi wengine ndani ya Tushikamane wamepata mawazo zaidi ambayo
yanaweza kusaidia. Pia, kuna uwezekano kwamba baadhi ya kamati zinaweza
kuwa zinashughulikia tatizo lenye mahitaji yanayofanana – mfano kuhusiana na
usafiri au miundombinu.
Kila
mwenyekiti wa kamati atawasilisha kwa kikundi kizima ufumbuzi au shughuli
ambayo kikundi chake kidogo kinapanga. Atawasilisha
taarifa ya kazi iliyofanyika hadi sasa.
Kikundi
kizima cha Tushikamane baada ya hapo kitajadili rasilimali ambazo zinaweza
kuhitajika ili ufumbuzi huo uweze kutekelezwa vizuri. Baada ya mjadala wa
dakika 10 au 15, watakuwa na orodha ya rasilimali ambazo watahitaji.
Kwa
ajili ya kila rasilimali, watahitaji sasa kufikiria vyanzo vyake – watazipata kutoka wapi au kwa nani ?
Mfano
Mathalan, ufumbuzi
unaweza kuwa mafunzo kwa wakunga wa jadi.
Rasilimali ambazo
watahitaji ni:
·
mtu wa kutoa mafunzo kwa wakunga
wa jadi;
·
kiongozi cha mafunzo kutoka kwa
watu wenye uzoefu katika kufundisha wakunga wa jadi;
·
sehemu ya kufanyia mafunzo hayo;
·
pengine zana au vitendea kazi ambavyo wakunga wa jadi watahitaji baada ya mafunzo
hayo kama vile mashine ya kupima presha;
·
nyenzo au utaratibu wa kuwasafirisha akinamama kwenda
hospitalini pale itakapohitajika.
Baada ya hapo wataanza kufikiria
vyanzo vya mahitaji hayo:
Mtu wa kutoa mafunzo kwa waganga wa jadi – watamuomba nani?
Je kuna mtu yeyote ambaye atawasaidia kutatua suala
hili? Hii ndiyo aina ya rasilimali ambayo wewe, kama Mwezeshaji wa Tushikamane, unaweza kuwasaidia.
Je vipi kuhusu vifaa vya mafunzo? Hapa tena unaweza kusaidia.
Sehemu ya kufanyia mafunzo: watahitaji kufikiria
nani wa kumuomba kuwasaidia kupata sehemu inayofaa. Nani ataongea naye?
Huenda kuna juhudi au huduma za serikali
ambazo zinaweza kuwasaidia. Nani
atafuatilia?
Kwa vitu ambavyo hugharimu fedha, usikurupuke kutoa ahadi ya kusaidia kuwatafutia shirika
la misaada. Lakini kwa vyovyote vile, wasaidie kuliandikia shirika la misaada ambalo linaweza
kuwa linafanya kazi katika eneo hilo au wilaya hiyo, kuelezea yale yote ambayo tayari
wamefanya hadi kufikia hatua hii ya kuhitaji fedha za kusaidia kuzuia vifo vya
mama na watoto wachanga.
Mashirika mengi ya misaada yanaweza kuitikia vizuri
maombi ya jamii ambazo zimeonesha azma na ushirikishaji wa kiwango hiki, na
ambazo zimesikiliza sauti za wanawake. Nani ataongoza juhudi hii?
Mwisho
wa mchakato huu, kamati itakuwa na orodha ya rasilimali zilizopendekezwa ambazo
wanaweza kuhitaji kufanikisha mipango yao. Watakuwa na wazo pia kuhusu mahali
wanaweza kwenda kutafuta rasilimali hizi, na pia wazo juu ya nani atafanya nini kabla ya
mkutano ujao.
4. Rudia mchakato huu kwa kila kamati. Kila kamati itawasilisha ufumbuzi wao au shughuli yao
iliyopangwa, na kikundi kizima baada ya hapo kitachangia katika utambuzi wa rasilimali zinazohitajika, na wapi rasilimali
hizo zinaweza kupatikana.
5. Fanya majumlisho ya mkutano na
kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini kabla ya mkutano unaofuata?
6. Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa
vya kutosha. Kama hapana, unaweza kurudi nyuma na kurudia baadhi au vipengele vyote vya mkutano.
7.Himiza washiriki kuuliza maswali.
8. Panga tarehe ya mkutano ujao.
Masuala
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 10
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari:
wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa
wangapi, wajawazito walikua wangapi ?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa
na mafanikio au changamoto zozote?
·
Kwa kila njia ya ufumbuzi iliyobainishwa, wamekubaliana nini juu ya
kamati, kanuni na mpango kazi ?
·
Kila kamati itachukua hatua gani
zinazofuata kutafuta mahitaji ya kufanikisha mipango yao? Unahitaji kuwa na
kumbukumbu ya mambo waliyokubaliana, ili uweze kuwakumbusha walichokisema…na
kusaidia kukifanikisha.
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 10
·
Makatibu wanapaswa kuorodhesha wahudhuriaji wote kwenye rejesta ya
kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·
Jaribu kupata maoni ya viongozi na watu wengine ambayo yanaweza
kusaidia kupima umuhimu wa juhudi inayoendelea kwenye kitongoji, na
kushiriki angalau katika mkutano 1 au 2, ili waweze kuona kama
wangependa kushiriki katika programu ya Tushikamane.
·
Tembelea kila mwenyekiti wa kamati, pamoja na watu wengine maarufu
ambao ungependa washiriki. Washawishi kuchukua hatua, na kuwauliza wangehitaji
msaada gani ili shughuli hizo ziweze
kufanikiwa.
·
Jadili mambo haya na msimamizi wako, na kuyaleta kwenye mkutano wa
kila mwezi na Kiongozi wa Mradi na Mwenyekiti wa Mradi. Katika hatua hii ya
mchakato wa Tushikamane, wanahitaji
kuanza kuvisaidia vikundi kuwasiliana na wadau
wengine ambao wanaweza kutoa misaada ya hali na mali kufanikisha
shughuli za kikundi.
Ili
kuweza kusaidia, wadau watahitaji picha halisi ya kinachoendelea, na nini hasa
kila kamati inatafuta.
MKUTANO WA 11 – KUTENGENEZA MIFUMO YA UFUATILIAJI
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 11
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu muhimu kwenye kitongoji ambao
walihudhuria mkutano wa 10. Wafanye
wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha programu inapoelekea: kuwapa wanawake walio
katika umri wa uzazi sauti katika maandalizi ya mipango ya kupunguza vifo vya mama na watoto
wachanga. Hii itasaidia kuvutia misaada ya hali na mali kutoka nje ya kitongoji
ambayo itaunganishwa na juhudi za jamii, na kuleta msukumo mkubwa katika kuzuia
vifo hivyo vya kusikitisha.
Wakumbushe
watu maarufu kwenye kitongoji kwamba
mkutano ujao utajaribu kubuni njia za kusaidia kujua iwapo mchakato wa
Tushikamane unafanya kazi, na wao wenyewe wanaweza kuwa na chochote cha
kuchangia.
Waeleze
bayana kwamba hili siyo jambo ambalo kitongoji kinataka kwa ajili tu ya
kujipatia ari zaidi. Lakini zaidi ya ari, wadau wengine nje ya mchakato ambao wangependa
kusaidia watataka kujua kama kweli mchakato huu unasaidia. Mashirika ya misaada
kama vile Mission Morogoro, AMREF, na asasi nyingine zenye uwezo zinaweza kusaidia
mchakato au programu kama
watajua upo utaratibu wa kufuatilia na kupima mafanikio yake.
Mkutano
utapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu
maarufu wote kwenye kitongoji kuwepo.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 11 ?
Wanawake
wote waliohudhuria Awamu ya 1 na 2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza, na wengine wapya waliohudhuria mkutano wa 10.
Pia, kikundi kitakuwa kimebaini watu maarufu kupitia mikutano iliyopita ambao
ushiriki wao utasaidia kikundi kufanya kazi vizuri na kuongeza uwezekano wa
kufanikiwa.
Fikiria
watu wengine mmoja mmoja ambao ni muhimu
kuhudhuria-kwa mfano mtu yeyote mwenye uzoefu katika ufuatiliaji. Watu kama hao
ni pamoja na wafanyakazi wa afya vijijini,
lakini pia baadhi ya wenyeviti wa vijiji, waalimu, nk.
Ajenda ya Mkutano wa 11
1. Makaribisho,
mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita na utambulisho
2. Kuwasilisha
lengo la mkutano: kupanga jinsi ya kufuatilia utekelezaji wa njia za ufumbuzi.
Jadili kwa nini ni muhimu kufuatilia utekelezaji wa njia za ufumbuzi: kusherekhea mafanikio na
kubainisha changamoto zozote, ili muweze kupanga jinsi ya kuzishughulikia.
3.
Shughuli
kuu za mkutano: Kupanga jinsi ya
kufuatilia utekelezaji wa njia za ufumbuzi.
Kwa mfano, kuna kamati 4, na kila kamati inawajibika kufanya
ufuatiliaji ili kujua iwapo yale waliyopanga yanafanikiwa au la.
Anza na kamati mojawapo – mathalan kamati moja
inataka kuanzisha mafunzo kwa wakunga wa jadi.
Ili kupata jibu kwa jinsi gani mtafanya ufuatiliaji wa mpango huu,
ongoza kikundi cha Tushikamane kupitia
mchakato ufuatao:
A. Jadili na kukubaliana manufaa gani yatatokana na ufumbuzi huo? Kwa mfano, mama atapona
haraka baada ya kujifungua na hatapoteza maisha; wakunga wa jadi watakuwa na
ufanisi zaidi katika utendaji wao; wanawake watajisikia salama zaidi na hisia
kutengwa wanapokuwa wanajifungua kupungua; mahusiano imara zaidi yatajengwa
baina ya programu na vituo vya kutolea huduma za afya; nk.
B. Ulizia maoni yao juu ya nani atanufaika na matunda kutokana na ufumbuzi
huo? Kwa mfano, wanawake wote wanaojifungua; pia hospitali kwa sababu kazi
ya kushughulikia makosa ambayo yanatokana na utendaji wa wakunga wa jadi
itapungua; wakunga wajadi wenyewe ambao uwezo wao utaongezeka; jamii kwa sababu
mama atapona haraka zaidi baada ya kujifungua, nk.
C. Jadili na kukubaliana lini watu hao watanufaika na ufumbuzi huo. Kwa mfano, mara nyingi; mara moja kwa mwezi; mara
moja katika maisha; nk. Hakuna sababu ya kujaribu kufanya ufuatiliaji wa kitu
ambacho hutokea ghafla au kwa nadra.
D. Jadili na kukubaliana wapi watu watanufaika. Kwa
mfano, ni watu wa kitongoji hiki, au pia
watu kutoka vijiji vyote vya jirani ?.
E. Maswali hayo yatakupa msingi wa kujadili na
kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji ambao utakuambia iwapo njia ya ufumbuzi
inayotekelezwa inafanikiwa.
Kwa mfano, haishi kujua kwamba
mtu alikuja kutoa mafunzo kwa wakunga wa jadi. Tunaweza pia kutaka kujua, kwa
mfano, ni wakunga wa jadi wangapi wameanza mafunzo?; wangapi wamemaliza?; wameyatumia
mafunzo waliyoyapata namna gani ili kuleta mabadiliko?; Kituo cha Afya au
Hospitali imeona tofauti yoyote? Je jamii imeona mabadiliko yoyote?
Kamati itapataje majibu kwa
maswali haya? Watakapokuwa na majibu wanaweza kusherekhea mafanikio, na pia
kukabiliana na changamoto ambazo zitagundulika kuzuia shughuli au ufumbuzi kwenda vizuri.
Mchakato huu kwa kamati ya
kwanza utakapokamilika, na ufumbuzi wake uliopangwa, kikundi cha Tushikamane baada
ya hapo kitajadili mpango wa kufanya tathmini ya shughuli zingine zilizopangwa,
au kurudia hatua A hadi E juu.
4.Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia
tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini
kabla ya mkutano unaofuata?
5. Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa vya
kutosha. Kama hapana, unaweza
kurudia baadhi au vipengele vyote vya mkutano.
6.Himiza
washiriki kuuliza maswali
7.Panga
tarehe ya mkutano ujao, mfano miezi 3 hadi 6 kutoka sasa, tarehe ambayo
inaacha muda wa kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli
zilizopangwa.
Masuala
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 11
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari:
wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa
wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa
na mafanikio au changamoto zozote?
·
Ni mpango gani wa ufuatiliaji ambao umeandaliwa kwa kila ufumbuzi
uliopangwa ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 11
·
Makatibu wanapaswa kuwaorodhesha wahudhuriaji wote kwenye rejesta ya
kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
Baada ya mkutano wa 11, sasa ni
wakati wa kuanza utekelezaji.
Kila kamati inahitaji msaada wako na msaada wa timu nzima ya Tushikamane, kadri itakavyokuwa ikitekeleza
shughuli na ufumbuzi ambazo ilipanga.
·
Wamekwisha kutambua rasilimali
ambazo wanahitaji, na hatua zinapaswa kuwa zimechukuliwa katika kutafuta
rasilimali hizi.
·
Wana mpango kazi na wanajua nani anahusika kwa kufanya nini, na lini.
·
Wamekubaliana juu ya mfumo wa ufuatiliaji wa maendeleo ya shughuli zao.
·
Unapaswa kukutana na kamati mara kwa mara katika kipindi hiki, kupitia
maendeleo ya utekelezaji, kusherehkea mafanikio na kubainisha na kushughulikia
changamoto ambazo zitakuwa zimejitokeza.
Ratiba ya mikutano itaamuliwa na wanakikundi wenyewe.
AWAMU YA 4 – KUFANYA TATHMINI PAMOJA
Shabaha
ya Awamu ya 4 ya mzunguko wa mikutano ni
kutathmini matokeo ya njia za ufumbuzi
ambazo zinatekelezwa juu ya matatizo makuu yaliyobainishwa. Awamu hii ina mikutano 3:
Mkutano
wa 12: Maendeleo ya mchakato wa tathmini.
Baada ya mkutano, wanakikundi watahitaji kuwa na uhakika kuwa wanaendelea vizuri katika ukusanyaji wa taarifa wanazohitaji
kwa ajili ya kufanya tathmini ya matokeo
ya shughuli zao juu ya matatizo ambayo
wamekuwa wakikabiliana nayo.
Mkutano
wa 13: Kufanya tathmini ya kazi za kamati, kikundi cha Tushikamane na mchakato wa Tushikamane.
Mkutano
wa 14: Kupanga kwa ajili ya siku za
usoni.
MKUTANO WA 12 – MAENDELEO YA
MCHAKATO WA TATHMINI
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 12
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu muhimu kwenye kitongoji ambao
walihudhuria mkutano wa 11. Wafanye
wajisikie kuwa ni jambo muhimu kushiriki, na kuwakumbusha wapi programu inapoelekea: kuwapa sauti wanawake walio katika umri wa uzazi
katika mipango ya kupunguza vifo vya
mama na watoto wachanga. Hii hatimaye itavutia misaada ya hali na mali kutoka
nje ya kitongoji, ambayo itaunganishwa na juhudi za jamii, na kuleta msukumo
mkubwa katika kuzuia vifo hivyo vya kusikitisha.
Wakumbushe
watu maarufu kwenye kitongoji kwamba
mkutano ujao utajaribu kubuni njia mbalimbali za kusaidia kujua iwapo mchakato
wa Tushikamane unafanya kazi, na wao wenyewe wanaweza kuwa na chochote cha
kuchangia.
Endelea
kuwaeleza kwamba wadau wengine nje ya mchakato ambao
wangependa kusaidia watataka kujua kama kweli mchakato huu unafanya kazi
vizuri. Mashirika yenye rasilimali yanaweza
kusaidia
mchakato au programu kama watajua
programu hiyo ina utaratibu wa
kufuatilia na kupima mafanikio yake.
Mkutano
unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu
maarufu wote kwenye kitongoji kuwepo.
Mkumbushe Mwenyekiti wa kila kamati kwamba ataombwa kukitaarifu kikundi jinsi mchakato wa tathmini yao unavyokwenda !
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 12 ?
Wanawake
wote waliohudhuria Awamu ya 1 na 2 wanapaswa kuhudhuria kama wanaweza, na wengine wapya waliohudhuria mkutano wa 11.
Pia, kikundi kitakuwa kimebaini watu maarufu kupitia mikutano iliyopita ambao
ushiriki wao utasaidia kikundi kufanya kazi vizuri na kuongeza uwezekano wa
kufanikiwa.
Fikiria
watu wengine mmoja mmoja ambao wana umuhimu
kuhudhuria-kwa mfano mtu yeyote mwenye uzoefu katika ufuatiliaji. Watu kama hao
ni pamoja na wafanyakazi wa afya vijijini,
lakini pia baadhi ya wenyeviti wa vijiji, waalimu, nk.
Ajenda ya Mkutano wa 12
1. Makaribisho.
Utambulisho kama kuna washiriki wapya.
2. Mapitio
ya Awamu ya 3 na kuwakumbusha watu kiasi
gani tayari kimefanyika.
3. Kuwasilisha
malengo ya mkutano, ambayo ni kupata ari na utayari wa kufanya tathmini ya mradi. Jadili kwa nini tathmini ni muhimu,
na hasa sisitiza kuwa uwezekano wa kuvutia
misaada kutoka nje utakuwa mkubwa zaidi
kwa sababu jamii inaweza kuonesha kwamba siyo tu wanayashughulikia matatizo yao,
lakini pia wana utaratibu wa kupima matokeo.
Hadithi ifuatayo
inatoa njia moja wapo ya kukisaidia kikundi kuelewa kwa nini tathmini ya
ukweli inathaminiwa sana, hasa kwa sababu husaidia:
·
Kutazama nyuma na kuona maendeleo;
·
Kubainisha mambo ambayo
yalikwenda vizuri,na ambayo wanapaswa kuendeleza ;
·
Kubainisha
changamoto na kuona wapi hasa penye tatizo;
·
Kukabiliana
na tatizo sahihi kwa njia sahihi;
·
Kusherekhea mafanikio!
Wasomee
hadithi hii: "Bibi. [weka jina], kutoka [weka jina la kijiji] , aliamua
kuwekeza katika biashara ya kutengeneza mikate. Aliajiri wafanyakazi 3 ambao
walimsaidia katika ujenzi wa jiko la bekari hiyo, kuanzisha kiduka kidogo cha
rejareja, na kutengeneza mikate yenyewe.
Mzunguko
wa kwanza wa uzalishaji wa mikate midogo ya skonzi ulitoa mikate yenye kiwango cha chini.
Hivyo alipata shillingi 2,000 tu.
Bibi [weka jina] alisikitika na kufikiria kuwa kiwango kidogo cha bidhaa
zake kilitokana na malighafi aliyoitumia. Hivyo, aliamua kununua malighafi
tofauti na kuitumia kutengeneza mzunguko wa pili wa skonzi.
Hata
hivyo, skonzi zilizozalishwa katika mzunguko wa pili zilikuwa mbaya hata kuliko za mzunguko wa
kwanza! Bibi. [weka jina] alisikitika tena na kuomba ushauri
kutoka kwa rafiki yake ambaye alikua akijishughulisha na ufugaji kuku. Ingawa
jamaa huyu alikuwa hajui chochote juu ya
kutengeneza mikate, alimwambia kuwa huenda wafanyakazi walikua wakimwibia
malighafi na kuwauzia wafanyabishara wengine wanaotengeneza mikate.
Bibi [weka jina] alikasirika sana na
wafanyakazi wake na kuwaamuru wafanye kazi miezi 3 bila mshahara.
Mzunguko
wa 3 walitengeneza skonzi za kiwango kile kile cha chini! Bibi [weka jina] alisikitika tena na kuamua kutafuta
ushauri kutoka kwa mtengenezaji mikate mwenzake. Mwanamke huyu alijua mambo
mengi juu ya biashara hiyo na kumwambia Bibi[weka jina] kwamba wafanyakazi wake
hawakuwa na utaalam wa kutengeneza mikate.Kabla ya hapo, walikuwa wanafanya
kazi kama walinzi kwenye bekari mmoja mjini. Hawakua na stadi zozote katika uokaji
mikate. Bibi [weka jina] aliamua kuajiri
wafanyakazi wapya wenye stadi za utengenezaji mikate na mzunguko wa 4 ulizalisha skonzi zenye ubora wa hali ya juu.
Wezesha
mjadala mfupi, kwa mfano kwa kuuliza maswali yafuatayo:
Tumesikia nini kwenye hadithi hii?
Mambo kama hayo huwa
yanatokea?
Kwa nini yanatokea?
Tumejifunza nini kutokana
na hadithi hii?
·
Katika mzunguko wa kwanza
wa kutengeneza skonzi, hakuajiri watu sahihi.
·
Katika mzunguko wa pili,
alifanya mabadiliko bila kuchunguza
tatizo lilikuwa nini.
·
Katika mzunguko wa 3, alipata
ushauri kutoka kwa mtu asiye na utaalam katika utengenezaji wa mikate.
·
Katika mkutano wa 4,
alipata ushauri kutoka kwa mtaalam na kutathmini tatizo kwa usahihi.
4. Shughuli kuu za mkutano: Kuangalia maendeleo ambayo yamefanyika katika
kutathmini kila mojawapo wa miradi 4(
kila kamati inatekeleza mradi wake).
Kila
moja wapo ya (mfano) kamati 4 inapaswa
kuwasilisha, moja baada ya nyingine, yaliyoamuliwa katika mkutano wa 11 juu ya ufuatiliaji wa mafanikio ya shughuli
yao. Wamefika hatua gani katika utekelezaji wa mifumo ya ufuatiliaji? Je
wameanza kupata mafanikio? Wamekumbana na matatizo yoyote katika utekelezaji wa
ufuatiliaji, na kama ndivyo, unaweza wewe au kikundi kusaidia kuyatatua matatizo?
Rudia
mchakato kwa kila kamati.
5.Fanya majumlisho ya mkutano na kuangalia
tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini kabla ya mkutano unaofuata?
6. Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa
vya kutosha. Kama hapana, unaweza kurudi nyuma na kurudia baadhi au vipengele vyote vya mkutano.
7.Himiza washiriki kuuliza maswali
8.Panga tarehe ya mkutano ujao ambayo
inatakiwa kuwapa watu nafasi ya kutosha
kutekeleza shughuli zilizopangwa-mfano miezi 3 hadi 6 kutoka sasa.
Masuala
muhimu kwa ajili ya ripoti yako ya Mkutano wa 12
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa kukamilishwa kwa muhtasari:
wangapi walihudhuria, wanawake walikuwa
wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa
na mafanikio au changamoto zozote?
·
Zoezi la tathmini limeonesha matokeo gani kwa kila tatizo kuu ambalo lilitambuliwa ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 12
·
Makatibu wanapaswa kuorodhesha wahudhuriaji wote kwenye rejesta ya
kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Pia wahimize wanakikundi kuwashirikisha wanakikundi wengine ambao
hawakuhudhuria juu ya mambo yaliyojadiliwa kwenye kikundi.
·
Tembelea kila mwenyekiti wa kamati, pamoja na watu wengine maarufu
ambao ungependa washirikishwe, au waliokubali kusaidia juhudi hiyo. Wahimize
kuuboresha mfumo wa tathmini ya mradi
wao, na kuwauliza msaada gani wangehitaji ili kufanikisha kazi hii.
·
Jadili mambo haya na msimamizi wako, na kuyaleta pia kwenye mkutano wa
kila mwezi na Kiongozi wa Mradi na Mwenyekiti wa Mradi. Ili kusaidia kulifanikisha hili, watahitaji kuwa
na ufahamu bayana wa changamoto ambazo kamati zinakabiliana nazo, na nini hasa
kila kamati inatafuta.
MKUTANO WA 13 – KUFANYA TATHMINI YA MATOKEO YA MIRADI YA TUSHIKAMANE NA TUSHIKAMANE YENYEWE
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 13
Soma
Kiongozi hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu maarufu kwenye kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa 11 na 12
.
Wakumbushe
watu maarufu kwenye kitongoji kwamba
mkutano ujao utajaribu kufanya tathmini ya mwisho kupima iwapo mchakato wa Tushikamane unafanya kazi. Wanaweza kuwa na
chochote cha kuchangia, lakini nao pia wangetaka
kujua matokeo.
Endelea
kuwaeleza kwamba wadau au asasi zenye uwezo wanaweza kusaidia
mchakato au programu yenye mafanikio, na ambayo inaweza kuthibitisha
au kuonesha mafanikio hayo.
Mkutano
unapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha watu waliotoa mchango mzuri katika mkutano uliopita
kuwepo.
Mkumbushe Mwenyekiti wa kila kamati kwamba atatakiwa
kutoa taarifa kwa kikundi jinsi zoezi lao
la tathmini linavyoendelea !!
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 13?
Wanawake
wote ambao wamekuwa wakishiriki kwa njia yeyote ile katika mchakato huu.
Wakumbushe
viongozi na watu maarufu kwenye jamii kwamba ni muhimu sana kuhudhuria mkutano
huu, ili waweze kujua iwapo mchakato wa Tushikamane ulifanikiwa au hapana.
Ajenda kwa
ajili ya Mkutano wa 13
1.
Makaribisho. Utambulisho kama kuna washiriki wapya.
2.
Mapitio
ya mkutano uliopita ambao ulikazia sana suala la tathmini.
3. Kuwasilisha
malengo ya mkutano:
·
Kufanya tathmini kupima jinsi
matatizo makuu yalivyoshughulikiwa.
·
Kufanya tathmini ya utendaji wa
kikundi.
·
Kupanga kwa ajili ya siku za usoni.
4. Shughuli kuu za mkutano: Kufanya tathmini ya mchakato mzima, mafanikio
na changamoto kuhusiana na mchakato wa Tushikamane, na kazi za kamati katika
kukabiliana na matatizo makuu yaliyobainishwa.
Muda wa
mkutano wa 13 utapokaribia, timu ya Tushikamane
itapanga jinsi gani watakaa pamoja kama
kikundi cha Tushikamane kufanya tathmini
hii.
Kinachotakiwa ni kutoka na picha iliyowazi ya
kiwango cha mafanikio katika maeneo yafuatayo:
·
Ushiriki katika vikundi na kwenye mikutano;
·
Kubainisha matatizo na mizizi yake;
·
Ufanisi wa kamati katika kushughulikia matatizo hayo na mizizi yake; kukiwa na maelezo mafupi juu ya mafanikio na changamoto muhimu.
·
Ubia au ufadhili na mahusiano muhimu na wadau wengine
ambayo yalianzishwa.
·
Uwezeshaji
na usimamizi wako;
·
Tathmini
ya mchakato wa Tushikamane – mzunguko wa mikutano 14 kama njia ya kusonga mbele.
Lingekuwa
jambo zuri kuweka alama halisi (mfano
kati ya 5) kwa kila eneo, pamoja na maelezo ya mafanikio na vikwazo.
5.
Jinsi
ya kuboresha zaidi shughuli za programu: kwa eneo au suala lolote katika tathmini ambalo lilipata alama chini ya
wastani, ongoza mjadala kwa lengo la kufanya eneo au mtu husika kufanya kazi
kwa ufanisi zaidi katika shughuli zijazo.
6. Fanya
majumlisho ya mkutano na kuangalia tena iwapo umejumlisha kwa usahihi. Nani atafanya nini kabla ya mkutano unaofuata?
7.
Pima kama malengo ya mkutano yamefikiwa vya kutosha. Kama hapana,
unaweza kurudi nyuma na kurudia baadhi
au vipengele vyote vya mkutano.
8. Himiza
washiriki kuuliza maswali.
9. Panga
tarehe ya mkutano ujao –mfano miezi 3 hadi 6 kutoka sasa, ili kuwapa watu muda
wa kutosha kutekeleza shughuli
zilizopangwa.
Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako
ya Mkutano wa
13
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa
kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi
walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa na mafanikio au changamoto gani?
·
Ni maendeleo, mafanikio, na
changamoto gani ambazo kikundi kizima kimepata, na kamati moja moja ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 13
·
Makatibu wanapaswa kuwaorodhesha washiriki wote kwenye rejesta ya kikundi.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Fanya mkutano wa nusu saa na timu nzima ya Tushikamane kujadili matokeo ya tathmini na kufanya
mapendekezo.
MKUTANO WA 14 – KUPANGA KWA AJILI
YA SIKU ZIJAZO
Jinsi ya
kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 14
Soma Kiongozi
hiki kabla ya mkutano na kuamua zana na vifaa ambavyo vinahitajika.
Tembelea
watu maarufu kwenye kitongoji ambao walihudhuria mkutano wa 13.
Wakumbushe
watu maarufu kwenye kitongoji kwamba
mkutano ujao ni kuamua nini cha kufanya baada ya hapo walipofikia. Kwa hivyo, mawazo
yao ni muhimu na yanahitaji kuzingatiwa. Wakumbushe wanawake ambao wametoa
mchango mkubwa katika mchakato huu kuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa sauti za wanawake zinaendelea
kusikilizwa.
Mkutano
utapokaribia, wakumbushe wanajamii tarehe, muda na mahali mkutano
utakapofanyika, na kuwahimiza kushiriki. Chagua muda unaofaa kuwezesha
watu waliotoa mchango mzuri katika
mkutano uliopita kuwepo.
Nani anapaswa
kuhudhuria Mkutano wa 14?
Huu ni
mkutano wa kitongoji kizima. Wakumbushe
viongozi na watu wengine maarufu kwamba
huu ni mkutano muhimu sana kuhudhuria, ili waweze kusaidia kupanga hatua
zitakazofuata.
Timu nzima ya Tushikamane inapaswa kuhudhuria – Mchungaji
Mgego, Mwenyekiti; Wilbard Mrase, Kiongozi wa Mradi; na Alex Gongwe, Msimamizi
wa Mradi.
Muhimu
zaidi, wanawake ambao wamekuwa wakishiriki katika mikutano yote ya Tushikamane wanaweza
kuja kusherekhea mafanikio – na kusaidia kuhakikisha kuwa wataendelea kusikilizwa, na kuchangia kuboresha afya ya baadaye ya dada zao na
mabinti zao – na watoto wao.
Ajenda kwa
ajili ya Mkutano wa 14
1.
Makaribisho, mapitio ya mhutasari wa mkutano uliopita, na utambulisho
2.
Kuwasilisha lengo la mkutano: Kuamua nini kifanyike na kikundi-hatima
ya kikundi.
3.
Kujadili kazi gani ambayo bado haijafanywa na kikundi
4. Kufanya
majumlisho ya mkutano
5. Kufanya
mipango ya baadaye!
6. Kupanga
tarehe kwa ajili ya mkutano unaofuata
Chagua
tatizo moja kuu na kukiongoza kikundi
kupitia mchakato wa maamuzi ufuatao:
1.Tatizo
kuu limeshughukiwa vya kutosha? Kama NDIYO: basi kikundi kinapaswa
kurudi kwenye Awamu ya 1 kubainisha na kuainisha matatizo mapya ambayo yatapewa kipaumbele.
2. Kama HAPANA:
Tatizo
sahihi ndiyo lililoshughulikiwa ? Kama hapana, rudi nyuma na kuchagua tatizo
lingine.
Huenda
lilikuwa tatizo sahihi, lakini ufumbuzi uliotekelezwa ndiyo haukuwa sahihi, kwa
sababu haukuikabili ipasavyo mizizi ya tatizo , au kuambatana na shughuli za uzuaji na /au usimamizi wa tatizo
hilo ?
Kama
hilo ndilo tatizo, basi kikundi kinaweza kurudi kwenye Awamu ya 2, na kuangalia tena mizizi ya tatizo, na
kupanga mikakati mbalimbali ya kutatua mizizi ya tatizo na kuzuia tatizo kutojitokeza.
Vinginevyo,
huenda tatizo lilikuwa sahihi na mipango ya ufumbuzi ilikuwa nzuri, lakini
haikufanikiwa. Kama sivyo , ni sababu gani zingine? Hii inaweza kurekebishwa?
Au ni
kwamba unahitaji muda zaidi ?
Masuala muhimu kwa ajili ya ripoti yako
ya Mkutano wa 14
·
Rejesta ya mahudhurio inapaswa
kukamilishwa kwa muhtasari: wangapi
walihudhuria, wanawake walikuwa wangapi, wangapi walikua wajawazito?
·
Mkutano uliendaje – je kulikuwa na mafanikio au changamoto zozote?
·
Ni hatua gani zitafuata ?
Nini
kifanyike baada ya Mkutano wa 14
·
Makatibu wanapaswa kuwaorodhesha kwenye rejesta ya kikundi washiriki wote.
·
Unapaswa kukamilisha ripoti ya mkutano kama ilivyoelekezwa juu.
·
Fanya mkutano wa timu nzima ya
Tushikamane, kujadili matokeo ya tathmini na kufanya mapendekezo.
No comments:
Post a Comment