Kalibu
wageni wetu
Tunguli
ni kata yetu
Mmefika
hapa kwetu
Mjisikie
nyumbani
Pole
nyingi tunatoa
Kwa
safali yenye njia
Mpate
kutupa nia
Mola
atawajlia
Afya
uzazi salama
Na
utoaji huduma
Ni
elimu iso koma
Kwa
vijana kina mama
Hongela kwa viongozi
Nanyie wetu walezi
Mladi wetu azizi
Kwa pamoja tunaweza
Ni mengi tunajifunza
Elimu tunaongeza
Ila mengi yatukwanza
Machache tunayataja
Vifo vya wajawazito
Pamoja na watoto
Nayo magonjwa mazito
Kina mama twateseka
Usafili nitatinzo
Upewapo na lufaa
Hapa mbali na belega
Uhai umashakani
Huduma upasuaji
Haha kwetu ndio ngumu
Maji kama alimasi
Visima tunakesha
Hali ngumu ya maisha
Huchagia vya kutosha
Magonjwa yatuchokesha
Kinamama na watoto
Tushikamane pamoja
Kuzikidhi zetu haja
Nisisi ndio wateja
Mladi huu twaweza
Wananchi viongozi
Na wadau wote kazi
Tubolesheni uzazi
Twatamka wazi wazi
Hapa mwisho tunatua
Asante twasubilia
Mtupe zenu nasaha
Nazo shida zetu pia
Utenzi huu umetungwa na kikundi cha asante kitogoji
cha mjuini
Na
kusomwa na
1. Amina omaly mgaya
2. Subila azizi mbaluku
3. Maliam athumani kilago
4. Ziada mwedipando
Could there be a recording of this on YouTube ? (Even to me, totally unversed in the language, it seems musical even without that.
ReplyDelete